Askofu Kakobe: Kinachoendelea katika Bunge la Katiba ni uhuni

Askofu Kakobe: Kinachoendelea katika Bunge la Katiba ni uhuni

Kakobe ni mtumishi wa Mungu aliye hai, ahsante sana kwa ukweli huu mchungu na safari hii nikija dar itabidi nimwe muumini wa kanisa lake kabisa ili nichote maarifa.
 
Kakobe ni mtumishi wa Mungu aliye hai, ahsante sana kwa ukweli huu mchungu na safari hii nikija dar itabidi nimwe muumini wa kanisa lake kabisa ili nichote maarifa.

Watumishi wa Mungu wanajionyesha kwa vitendo vyao kwenye Jamii bila kujali Imani Au itikadi na si kwa kupigiwa debe na waumini wao wa makanisani ambao wanawaona Kama miungu.
 
Sitakaaa nimuamin huyu mchungaj kwan n mchonganishi sana na n mtu wa kuwagawa wananch ,ukiona mtu anatumia mwanvuli wa dini kuingia kwnye mambo ya siasa muogope kama ukoma kama sio kumpuuza

Hajatumia dini ila ww unamchukia kakobe.alichosema ni uhalali wa bunge la katiba kufanya wanachofanya sasa.
 
CCM wanachezea sana Tanzania halafu nazidi kushangaa watu wanawashangilia
 
Katika Maasikofu na Wachungaji waliomakini Tz amebaki Kakobe tu. Wengi wamebaki kutangaza michango tu bila kuwambia waumini wao ukweli.

Mwingine ambaye anaweza nena ni Mwingira zaidi ya hapo sijaona.

Dini zote ziseme kitu maana CCM inaua nchi.
 
Unawafanya watumishi wa Mungu kuwa waganga wa kienyeji wakati kuna Kingunge aliyetangazwa rasmi na Rais Kikwete kuwa ndiye kiongozi mkuu wa waganga/wachawi wote nchini? Nadhani mshirikina mwingne ni Kikwete ambaye Shekhe Yahaya alisema kuwa analimdwa na majini.

Huyu mganga wa kienyeji naye anyamaze tu asitusumbue kabisa na madawa yake ya jadi.
 
inaelekea hawa ukawa wameshikwa na kichaa wanaweweseka ovyo. inakuaje watu waliokua wanajidai wanataka katiba wanakimbia bmk. huo waraka wa makanisa ya wachumia tumbo hauwezi kubadilisha kitu. nani anatumia ubabe kati ya ccm na ukawa? tangu lini muafaka iwe wachache kulazimisha wengi? ccm kina ridhaa kubwa ya wananchi kina haki sera zake za kimsingi kuheshimiwa. sio kujidai kuongelea wananchi wakati kura zinaoyesha nani anawakilisha wananchi. endeleeni na kakobe kenu bunge linaendelea.
 
Ukweli tu ndo utakaoondoa uhuni km Huu ktk taifa hili tajiri la rasilimali lkn masikini wa mawazo
 
Namwamini Zachary Kakobe.

Lakini kwa nini asifute na ile kauli aliyotoa mwaka 2005 kuwa Kikwete ni Mteule wa Mungu? Sasa Kakobe amefunguka macho. Alikuwa kipofu hapo awali.
 
Kabla ya mahubiri ya Neno la Mungu katika Ibada Kuu ya leo Jumapili 7.9.2014, Mwenge, Dar-Es-Salaam; Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Zachary Kakobe, alianza kwanza kusoma kwa waumini wote Tamko zima la Jukwaa la Wakristo Tanzania kuhusu Mchakato wa Katiba. Alisema kwamba Kanisa la FGBF linaunga mkono tamko hilo, siyo kwa asilimia 100%, bali kwa asilimia 200%. "Tamko hili limekuwa likisomwa katika Makanisa ya Katoliki, KKKT, na mengineyo kuanzia Jumapili iliyopita, na leo nitalisoma kwenu, neno kwa neno. Wakati umepita wa Wakristo kugawanywa, ili Shetani atawale. Tofauti zetu Wakristo tunaziweka pembeni, tunaunganishwa na msalaba. Jukwaa la Wakristo Tanzania linawaunganisha wote wanaoamini juu ya msalaba - TEC, CPCT, CCT na SDA. Hivyo kauli ya Jukwaa la Wakristo Tanzania, ni kauli ya FGBF, kwa sababu sisi tuko ndani ya CPCT."

Aliendelea kusema,"Kama tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania linavyosema, Rasimu ya Pili ya Katiba ni Waraka halali na rasmi, na ndiyo mawazo ya Watanzania. Katiba ni ya Wananchi na inahitaji maridhiano, na siyo ubabe. Huu ndiyo pia msimamo wa Kanisa la FGBF. Kinachoendelea sasa katika Bunge Maalum la Katiba, ni uhuni tu wa mchwa wanaotafuna fedha za Watanzania bila huruma kwa wananchi wasio na uwezo hata wa kununua dawa ya Malaria", alisema Askofu Kakobe. Baada ya kusoma tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania, la Agosti 28, 2014, aliwauliza waumini,"Anayeunga mkono tamko hili asimame na kupunga mikono yake." Ndipo wote Kanisani maelfu kwa maelfu waliposimama na kupunga mikono yao huku wakishangilia. Kisha Kakobe akasema, "Pamoja na umuhimu wa maombi, haitoshi tu kuomba. Baada ya kufunga na kuomba, Esta alichukua hatua ya kumwambia ukweli Mfalme. Pamoja na maombi, hatua ya Jukwaa la Wakristo Tanzania kutoa sauti ya Kinabii kama hii, ni muhimu, ili mwenye masikio asikie."

Alimaliza kwa kusema,"Wapuuzeni watu wanaosema kwamba kufanya hivi ni kuchanganya dini na siasa! Katiba siyo siasa, ni zaidi ya siasa. Siasa imo ndani ya Katiba, lakini ndani ya Katiba kuna mambo mengi pia ambayo siyo siasa, kama vile Dini, Majeshi, Mahakama, Elimu, Kilimo, Ardhi, Ufugaji, Haki za binadamu n.k. Kwa ujasiri wote, kila Mkristo apaze sauti yake kukemea uhuni unaoendelea katika Bunge la Katiba, mpaka masikio ya walioko huko yazibuke!"
.................................................................................................................................................................
Ni kweli Kabisa hiki alichokisema Mheshimiwa Baba Askofu Kakobe.Naunga mkono kwa asilimia milioni kumi!.Wanaopinga ni wale tu wanaotetea matumbo yao tu lakini dhamiri zinawashtaki.Msema kweli bila unafiki wowote ataungana na ukweli huu.Kinachoendelea kwa sasa bunge maalumu la katiba ni uhuni uliopitiliza!
 
Kakobe ni askofu kanjanja.
kwa sababu kasoma tamko lililotolewa na baraza la wakristo? Bado waislamu nao watatoa tamko lao kuhusu kuchakachuliwa kwa maoni yao na maccm hasa swala la kadhi. Jiandae kubeba majeneza ya magamba kisiasa wee choo sijui cha kike

 
Tunaomba upande wa pili na nyinyi pazeni sauti hawa mahahafidhina waumbuke!

Washasema sanaa masheikh mpaka leo wengine wako ndani wanaadhalilishwa na ndochanzo cha kuibuka hiyo katiba inayojadiliwa
 
Namwamini Zachary Kakobe.

Lakini kwa nini asifute na ile kauli aliyotoa mwaka 2005 kuwa Kikwete ni Mteule wa Mungu? Sasa Kakobe amefunguka macho. Alikuwa kipofu hapo awali.

Eti Kakobe aliwahi kusema Kikwete ni mteule wa Mungu!!!!!???? NOP! Wewe hujamjua Kakobe !!!!
 
Zamani makanisa alikuwa yanatenga wanaohatarisha amani ya kanisa na watu wote. Kwa nini wasiwatenge hao wanaohujumu katiba ambayo ndio kila kitu katika maisha ya watz?
 
Back
Top Bottom