Askofu Kakobe: Kinachoendelea katika Bunge la Katiba ni uhuni

Tunaomba upande wa pili na nyinyi pazeni sauti hawa mahahafidhina waumbuke!
 
makanisa yanajitahidi sana kuhamasisha jamii kudai haki, mbona upande wa kushoto wako kimya hivyo??? ikipatikana katiba watasema katiba ya wakristo!

Waseme mara ngapi wao wamesema zamani na mpaka sasa ndo wameekwa ndani kwa kisingizio cha ugaidi. kwa kua dunia hii waislam hatuna haki kila tufanyalo system ikiona hailitaki bac ni ugaidi heri yenu nyinyi wenzetu ambao dunia inawathamini sasa ni wakati wenu kupaza sauti.
kazi hiyo waliifanya uamsho ccm wakaingiza wahuni kuchoma makanisa kupindisha ukweli na kutugawa watz.
Hongera jukwaa kwa kusimamia haki
 
Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu Dini zote kuu za Tanzania kuungana kumpinga dikteta CCM maana sasa dikteta huyu anaanza kuvuka mipaka ni lazima awahiwe kabla hajatumaliza.
 
mwisho wake wa siasa umefika

Wajanja wamemwingiza Sitta choo cha kike! Walimpamba sana kwamba hakuna Spika kama yeye, naye akaingia kichwakichwa. Sasa Sitta atapambanaje na mbaya wake Lowassa, wakati amedharaulika hivi?
 
simiyuYetu, Msalani, Lizaboni na wengineo mmeipata hiyo taarifa???
Safari hii janja yenu MaCCM imefikia mwisho watu wamechoka na upuuzi wenu na wizi!!
 
Last edited by a moderator:
Kabla ya mahubiri ya Neno la Mungu katika Ibada Kuu ya leo Jumapili 7.9.2014, Mwenge, Dar-Es-Salaam; Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Zachary Kakobe, alianza kwanza kusoma kwa waumini wote Tamko zima la Jukwaa la Wakristo Tanzania kuhusu Mchakato wa Katiba. Alisema kwamba Kanisa la FGBF linaunga mkono tamko hilo, siyo kwa asilimia 100%, bali kwa asilimia 200%. "Tamko hili limekuwa likisomwa katika Makanisa ya Katoliki, KKKT, na mengineyo kuanzia Jumapili iliyopita, na leo nitalisoma kwenu, neno kwa neno. Wakati umepita wa Wakristo kugawanywa, ili Shetani atawale. Tofauti zetu Wakristo tunaziweka pembeni, tunaunganishwa na msalaba. Jukwaa la Wakristo Tanzania linawaunganisha wote wanaoamini juu ya msalaba - TEC, CPCT, CCT na SDA. Hivyo kauli ya Jukwaa la Wakristo Tanzania, ni kauli ya FGBF, kwa sababu sisi tuko ndani ya CPCT."

Aliendelea kusema,"Kama tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania linavyosema, Rasimu ya Pili ya Katiba ni Waraka halali na rasmi, na ndiyo mawazo ya Watanzania. Katiba ni ya Wananchi na inahitaji maridhiano, na siyo ubabe. Huu ndiyo pia msimamo wa Kanisa la FGBF. Kinachoendelea sasa katika Bunge Maalum la Katiba, ni uhuni tu wa mchwa wanaotafuna fedha za Watanzania bila huruma kwa wananchi wasio na uwezo hata wa kununua dawa ya Malaria", alisema Askofu Kakobe. Baada ya kusoma tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania, la Agosti 28, 2014, aliwauliza waumini,"Anayeunga mkono tamko hili asimame na kupunga mikono yake." Ndipo wote Kanisani maelfu kwa maelfu waliposimama na kupunga mikono yao huku wakishangilia. Kisha Kakobe akasema, "Pamoja na umuhimu wa maombi, haitoshi tu kuomba. Baada ya kufunga na kuomba, Esta alichukua hatua ya kumwambia ukweli Mfalme. Pamoja na maombi, hatua ya Jukwaa la Wakristo Tanzania kutoa sauti ya Kinabii kama hii, ni muhimu, ili mwenye masikio asikie."

Alimaliza kwa kusema,"Wapuuzeni watu wanaosema kwamba kufanya hivi ni kuchanganya dini na siasa! Katiba siyo siasa, ni zaidi ya siasa. Siasa imo ndani ya Katiba, lakini ndani ya Katiba kuna mambo mengi pia ambayo siyo siasa, kama vile Dini, Majeshi, Mahakama, Elimu, Kilimo, Ardhi, Ufugaji, Haki za binadamu n.k. Kwa ujasiri wote, kila Mkristo apaze sauti yake kukemea uhuni unaoendelea katika Bunge la Katiba, mpaka masikio ya walioko huko yazibuke!"

Mwenyewe mhuni
 
Haya yanayoendelea Kwenye Bunge la Katiba ni matokeo ya Kiburi cha Kikwete!!
Juzi Kikwete amewakejeli viongozi wa dinio ati wamuombee !!!!!!!!!!!
Kikwete anatakiwa kutubu hadharani kwa kuliposha Taifa . Ni vema akatubu haraka kuliko kuchelewa maana huko mbele kuna aibu zaidi

Ukweli umeanza kujionyesha . JK alichakachua majina ya wajumbe halali na kuweka Wachawi wenye sura ya CCM leo tunaona kila mtu anawakataa!!!
Ameweka ndungu zake humo ndani ambao wameanza kugombania pesa
Uhuni huu una ambatana na kiburi !!
 
Utake usitake Kakobe ni mhuni na Kama wewe ni mmoja wa waumini wake wote ni walewale.
Tunataka uzungumzie Katiba na Kikwete , nini kinaendelea Bunge la katiba !!!
Kwa nini wajumbe wameanza kukanwa??
Kwa nini mwanasheria Znz amejitoa hapo ujue kuna uhuni ndani. !!
Toa hoja vinginevyo na wewe ni sehemu ya wahuni
 
Utake usitake Kakobe ni mhuni na Kama wewe ni mmoja wa waumini wake wote ni walewale.

mkuu kidogo umeshusha nidham kwa waumini wa kakabe bila sababu za maana;chuki yako ya kidini haifai mkuu.
 
Kakobe Mpinga Maendeleo na mbinafsi eti alitaka Umeme usipite kwenye kanisa lake. Kwani kule kwingine ulikopita hao si Watu isipokuwa Yeye na kanisa lake tu. Acha ubinafsi.
 
Askofu kanjanja ni Amos Joseph Mhagachi aliyeko katika Bunge hili la wahuni, ambaye alitoa tamko lake kupinga Tamko la Jukwaa la Wakristo, na CCT wakasema hawamtambui, ni Askofu wa CCM!
Yupo mwingine wanamwita Askof Pius Ikongo ana miliki wanawake wawili na ndo mshauri wa CCM ya Kikwete
 
Bora hata muache Kwenda kwenye Nyumba za Ibada Kama roho zenu zina kutu na ubinafsi unaopinga hata Maendeleo ya Watu wote.
 
Back
Top Bottom