Askofu Kakobe: Tanzania ni mpango wa shetani; Tanganyika inakuja!

Askofu Kakobe: Tanzania ni mpango wa shetani; Tanganyika inakuja!

Wakati akihubiri kwenye kanisa lake la FGBF, Mwenge jijini Dar es Salaam, Askofu Zakary Kakobe amesikika akisema kuwa Tanzania ni mpango wa shetani ndio maana kila mara hoja ya kuitaka Tanganyika inaibuka. Hebu msikilize wewe mwenyewe:

View attachment 2662050
MAONI YANGU
Askofu Kakobe ni miongoni mwa viongozi wa dini ninaowakubali sana hapa nchini. Hana unafiki na uchawa kama walivyo akina Geodavie, Kuhani Mussa na wengine, hasa linapokuja suala la kutetea maslahi mapana ya taifa na ustawi wa wananchi.

Marehemu Karume aliwahi kusema kuwa ikiwa koti linakubana ni vizuri ulivue na kulitupilia mbali. Kwa hali ilivyo sasa, naona koti la muungano tayari limebana. Hakuna faida zozote za muungano kwa watanganyika. Wazaznzibar ndio wananufaika zaidi na muungano huu. Wameona haitoshi wameamua kuuza bandari ya Tanganyika kwa waarabu. Wakati sasa umefika tuamue kunyoa hizi nywele chafu zilizojaa chawa kwa manufaa yetu na ya vizazi vijavyo.
Bahati mbaya kuvunjika kwa muungano kuna hasala kwa atakaevunja, hivi Hamkumsikia Lukuvi akizitaja? Kweli Mipango ya mwalimu Nyerere Leo yakutwezwa nakuitwa ya shetani? Kweli kanisa Katoliki halioni hili?
 
Just incase you live under the cage....👇

Swali.
Tanganyika ikarudi, nini tutapata zaidi?
Haya anayoyasema huyu chawa hayaweza kuhalalisha uuzwaji wa mali za Tanganyika kwa waarabu kwa bei ya kutupwa? Wao ndio wananufaika na muungano lakini kila siku wanatuletea chokochoko za kipuuzi. Wana nini lakini hawa wala urojo?
 
Ile meseji wanasambaza kila kanisa ili kuleta mtifuano ..

kwa nn msije na mkataba ukiwa na hints zake mkachambua mnakuja na hoja za hofu kitu ambacho hakipo.

Muungano hata ukivunjika hakuna mtu atakufa wala kupata hasara ,maisha yataendelea ila tambua hata sisi kikanda watu bado wanabaguana .
 
Katiba Mpya itakayo heshimiwa na wote ndiyo suluhisho badala ya sasa vigogo na watawala kuamua mambo kwa utashi binafsi bila kuzingatia katiba inayokubalika na wananchi wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar .

Maneno haya ya Askofu Kakobe ingawa ni ya miaka mingi kwa kufuatana digital footprint ya video clip hii kuwa ni ya muda mrefu uliopita lakini nao maneno yake yamedumu na leo 2023 kuna gumzo kubwa kuhusu mamlaka za Tanganyika na Zanzibar katika Muungano yanahojiwa, mipaka yake, haki zake n.k
 
Sauti ya viongozi wa Dini ni sauti ya Mungu watu na serikali!haya Marehem Camiillius alionywa na hawa hawa viongozi wa Dini nini kilitokea baada ya kushupaza shingo!!?

TEC WANAKUTANA,MAWAKILI MAHAKAMANI WANAENDA,HUKU WATUMISHI WA MUNGU NAO ROHO ALIOWASHUKIA ANANENA KWA LUGHA YA TANGANYIKA,

WALIOKARIBU NA MAMA WAMSHAURI SAWA SAWA!!!

Mungu IBARIKI Tanzania nchi yetu niipendayo sana
 
Wakati akihubiri kwenye kanisa lake la FGBF, Mwenge jijini Dar es Salaam, Askofu Zakary Kakobe amesikika akisema kuwa Tanzania ni mpango wa shetani ndio maana kila mara hoja ya kuitaka Tanganyika inaibuka. Hebu msikilize wewe mwenyewe:

View attachment 2662050
MAONI YANGU
Askofu Kakobe ni miongoni mwa viongozi wa dini ninaowakubali sana hapa nchini. Hana unafiki na uchawa kama walivyo akina Geodavie, Kuhani Mussa na wengine, hasa linapokuja suala la kutetea maslahi mapana ya taifa na ustawi wa wananchi.

Marehemu Karume aliwahi kusema kuwa ikiwa koti linakubana ni vizuri ulivue na kulitupilia mbali. Kwa hali ilivyo sasa, naona koti la muungano tayari limebana. Hakuna faida zozote za muungano kwa watanganyika. Wazaznzibar ndio wananufaika zaidi na muungano huu. Wameona haitoshi wameamua kuuza bandari ya Tanganyika kwa waarabu. Wakati sasa umefika tuamue kunyoa hizi nywele chafu zilizojaa chawa kwa manufaa yetu na ya vizazi vijavyo.
Kama bandari ya sarama/bandari sarama imeuzwa na wazanzibar basi wazanzibari wameiuza bandari yao wasilaumiwe

Na Kama tutataka muungano uvunjike basi tuwaachie dar es laam yao tuwaachie na pwani yao pia ikiwemo na bandari yao ya dar esraam 😡😡
 
Kuuvunja Muungano ni kiu ya wazanzibar ya miaka mingi, Huenda watashukuru sana kwa tukio hilo.
Lakini Watanganyika kukataa Bandari kuendeshwa na Kampuni ya nje ni kujinyima fursa adhimu ya kuipaisha Tanganyika kiuchumi .
Kakobe anaendeshwa na hisia zake binafsi kwa kumchukia Raisi Mzanzibari , si vyengine. Ile Hijabu ya mama pale ikulu inawaumiza nyoyo watu hawa wa makanisa.
Kama raisi akiwa Mkatoliki (mkiristo na akfanya maamuzi kama hayo kwa Watanganyika hawa hawa watamsifu na kumpongeza).
Kwani Bandari hii hii ilikuwa chini ya kampuni ya TICS kwa miaka 20 iliyopita ilisainiwa na Mkapa. Ufanisi wake ulikuwa kwa kiasi lakni bado uko chini ya viwango tarajiwa ndio maana Mkataba ulipokwisha wakaona walete kampuni nyingine iliyo bora zaidi ili kuongeza ufanisi na kuendana na wakati.

To Hel,
wacha Muungano uvunjike,
kwani Mama yuko pale kutimiza wajibu wake kama Raisi wa nchi
Washuri wake 90% ni watanganyika. Mimi sijaona kasoro yoyote,.
Kwa mara ya kwanza Bunge limeshirikishwa kuridhia mkataba huu ili kutanua wigo wa ushirikishwaji.
Bado watu wanendelea kuchochea kuvunjwa kwa Muungano ili Samia Arudi Zenji.
Mbona hili liko wazi, Watanganyika wakifanya Mistake hii watatukamatia chumbe kwa Maendeleo .
Zanzibar imekwama kimaendeleo kwa miaka 60 sasa kwa sababu ya Dubwana hili Muungano ulio chini ya Tanganyika.

Any way
Tanganyika kwa sasa ni yetu sote, wacha wazanzibar wafaidi tunda la Muungano na
Zanzibar ni ya Wazanzibari pekeyao.Wanaofaidi ni wazanzibar pekeyao.
Wazanzibar hawawezi kuuvunja muungano kabla ya kuuza mali za Tanganyika kwa waarabu wenzao. Uuzaji huu wa mali za Tanganyika ni mwanzo wa kuvunjika kwa muungano. Watanganyika wasipochukua hatua, ipo siku nao watauzwa utumwani kwa waarabu.
 
Back
Top Bottom