Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,917
Tarehe 7 Septemba 2020: Niliendelea kupaza sauti ili kutaka HAKI katika nchi. Nilionya na kutahadharisha kuhusu uwezekano wa kutokea kwa vurugu za kisiasa katika Visiwa vya Unguja na Pemba (Zanzibar) endapo Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) haitawarejesha Wagombea wa Upinzani walioenguliwa hasa kutoka Chama cha ACT Wazalendo kinachoongozwa na Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad ambacho ndio Chama Kikuu cha Upinzani Visiwani.
Niliyasema hayo nilipokuwa natoa nasaha za Kiaskofu kabla ya kutoa Sala katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Mheshimiwa Tundu Lissu. Mkutano huo ulifanyika katika Uwanja wa Kibanda Maiti, Unguja.
Baada ya kutoa nasaha niliwaongoza maelfu ya watu waliohudhuria katika kumuomba Mungu ili awakemee, awaaibishe na kuwafedhehesha wale wote watakaoendelea kuwahujumu Wagombea na wale watakaopanga, watakaofadhili na kutekeleza mikakati miovu ya kuiba au kupora kura na kisha kuwatangaza Wagombea ambao hawakushinda sio tu katika Zanzibar peke yake, bali hata kwa Tanzania nzima. Baada ya Mkutano kumalizika, nilipata fursa ya kubarizi na kunywa kahawa pamoja na Wazee wa Unguja kama ilivyo desturi na ukarimu wa Wazanzibari.
Tusipokemea hujuma na ukiukwaji wa haki sasa, tujiandae kushuhudia vurugu za kisiasa kutoka kwa makundi ya watu wenye hasira na hivyo kupelekea kuondoka kwa amani na utulivu katika nchi. Mimi nimetimiza wajibu wangu kwa Zanzibar na Tanzania yote kwa ujumla (Ezekieli 33:1-20).
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki