Tusilaumu vyombo vya habariNitaanzia mbali sana bro!. Cardinal ni "Prince of Rome"...na limezaliwa kutoka, katika historia ya watu amba walikua wakichaguliwa kumsaidia Askofu wa Roma katika ushauri na uongozi katika utendaji wake. Na baadaye kundi hili likagawanywa katika vitengo mbali mbali...na hasa baadaye yakazaliwa makundi manne yaliyosimamia makanisa makuu manne ya Roma- yaani Kanisa la Kipapa ya Mt. Yohane wa Lateran ( Cathedral of Rome), Mt. Petro, Mt. Paulo na Maria Mkuu ( Mary Major)...haya makundi yakawa kama Cardinal Points, points of reference, na muongozo katika kumsaidia Askofu wa Rome ambaye ndio Baba Mtakatifu. Hivyo ndivyo likazaliwa neno "Cardinal"...ila maana halisi, anaye chaguliwa anakua "Prince of Rome" na anapata hadhi ya Ukasisi wa Jimbo la Roma, na hapo ndipo anapatiwa moja ya Kanisa Roma ama Parokia. Hawa Cardinals wanakua katika hadhi tatu; Cardinal Bishop, Cardinal Priest na Cardinal Deacon...ambazo ni hatua cardinal anapitia kulingana na muda, na kuundwa/ kufanywa kwake ( to be created ).
Hivyo basi, kardinali ni Tuzo anayopewa Askofu, Padre au Shemasi. Askofu Mkuu ni Askofu wa Jimbo Kuu, mathalani Tz yapo nane.
Nchi inaweza kuwa na makardinali hata wanne. Ukardinali ni tuzo sio cheo ktk mfumo wa ngazi ktk vyeo vya kanisa.
Makardinali ni wajumbe wa baraza(conclave) inayomchagua Papa kiti kikiwa wazi. Wao pia ni wagombea kwa maana Papa anachaguliwa miongoni mwa Makardinali.
Hawagombei kama kwenye siasa bali hufungiwa kila mmoja kwenye chumba chake bila kuonana na mwingine na kupigiana kura. Mshindi lazima apate theluthi mbili ya kura zote.... Askofu Mkuu au Askofu mwingine hana nafasi hiyo....Nchi kama Italy wanao 28, USA wako 11, German 5 wakati Rwanda hawakuwahi kuwa na cardinal mpaka walipompata last year.
Pia tuwekane sawa kuwa Kadinali siyo mkuu wa Kanisa KATOLIKI NCHINI, Lahasha, bali Rais/Mwenyekiti wa TEC ambaye kwasasa ni Askofu Gervas Nyaisongwa wa Jimbo Kuu la Mbeya. Hivyo Fr Kitima ni mtu mkubwa sana kwasasa kikanisa kama Katibu wa TEC. Mara kadhaa idara ya habari nchini imekuwa ikifanya haya makosa kwa kudhani Kadinali ni mkubwa kuliko maaskofu wengine. Big NO.
Hata wanasiasa na Makardinali wenyewe hujidhihirisha kuwa wao ni Wakubwa sana kuliko Rais wa TEC...hasa Mzee Pengo, kazingua sana wakati wake