Askofu Mkuu SPCT aitaka Serikali kusikiliza CHADEMA: Asema Maridhiano ni muhimu kwa Ustawi wa Taifa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Askofu Mkuu wa Makanisa ya SPCT na Rais wa Umoja wa Maaskofu, Wachungaji, Mitume, Manabii na Madhehebu ya Kikristo Tanzania, Askofu Mussa Mlawi, amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuangalia kwa makini mvutano unaoendelea kati ya Serikali na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akisema kuwa kuweka vikwazo vya kisiasa si jambo jema kwa ustawi wa taifa.

Askofu Mlawi amesema anaamini kuwa kupitia mazungumzo na usikivu, kila jambo linaweza kutatuliwa kwa njia ya amani, ikiwa Serikali itasikiliza maoni ya vyama vya upinzani na kuyashughulikia kwa hekima.

Aidha, ameeleza kuwa tayari amewahi kumwandikia Rais Samia barua za ushauri kuhusu masuala ya haki na maridhiano, akionya kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo, yasipotazamwa kwa makini, yanaweza kuathiri ustawi wa uongozi wake.

Chanzo: Jambo TV
 
View attachment 3358902
Chanzo: Jambo TV
Malasusa amelaaniwa!
 
Back
Top Bottom