Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 29,909
- 32,414
“Juzi tumekuwa na janga pale Kariakoo, nchi imesimama kwa sababu ya janga la pale Kariakoo. Wote tumeguswa kwa ajili ya watu ambao tumetangaziwa 13 wamefariki, wale watu wamekufa wakati wanatafuta Maisha, wamekatishwa na kifusi kama Watanzania ni janga la kitaifa.”
“Lakini iweje mtu anachukuliwa, anachomolewa kwenye basi, anapigwa risasi au anauawa. Watu wanapotezwa, hili tunaliona kama sio janga la kitaifa. Kuna unafiki mkubwa sana katika nchi hii, hawa waliopotea wanatofauti gani na wale waliokufa pale Kariakoo, hawa waliopigwa risasi kuna tofauti gani na wale waliokufa pale Kariakoo. Iweje tubague maafa katika nchi hii. Utekaji unaendelea ambao ndio unatisha zaidi kuliko hata janga la Kariakoo.” – Askofu Mwamakula
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula ameeleza hayo leo Jumanne, Novemba 19, 2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Makazi ya Askofu yaliyoko mtaa wa Itunge/Iramba karibu na mtaa wa Ruaha eneo la Kituo cha Polisi, Rift Valley, Kimara Suka jijijni Dar es Salaam.
Mazungumzo ya Askofu Mwamakula yamejikita zaidi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, uchambuzi wa tamko la Baraza la Maaskofu wa Katoliki (TEC) na Tamko la Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), hali ya kisiasa ndani ya vyama vya siasa, tatizo la ajira nchini, utekaji, upotezwaji na mauaji ya wanasiasa na wakosoaji wa Serikali, maafa na uwezo wa Serikali kukabiliana nayo, mamlaka na uwezo wa Bunge katika kuisimamia Serikali; muelekeo na mustakabali wa madai ya Katiba Mpya, imani ya Watanzania kwa Serikali yao pamoja na imani yao kwa michakato ya chaguzi na demokrasia kwa ujumla.