Askofu Mwamakula kuongoza matembezi ya hiyari kuhamasisha Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi

Askofu Mwamakula kuongoza matembezi ya hiyari kuhamasisha Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
ASKOFU KUONGOZA MATEMBEZI YA HIARI YA RAIA KUHAMASISHA UUNDAJI WA TUME HURU YA UCHAGUZI NA UANDIKAJI WA KATIBA MPYA NCHINI TANZANIA!

Wapendwa Watanzania!

Tunapenda kuwajulisha kuwa Askofu Mwamakula, anakusudia kuongoza Matembezi ya Hiari ya Raia yasiyopungua umbali wa Kilometa 15 katika Mikoa mbalimbali nchini Tanzania na nje ya nchi. Watu watakaoshiriki Matembezi hayo watatokea kila kona za mji husika hadi sehemu ya kukutania ambapo watu wote watakusanyika kwa ajili ya kufikisha au kutolea ujumbe. Ili kuepusha usumbufu, watu watakuwa wanatembea kimakundi lakini kila kundi halitazidi watu 20 na kama watu watakuwa wengi kutokea njia moja kutakuwa na muachano au umbali wa kilomita moja kati ya kundi na kundi njiani!

Lengo la Matembezi hayo ni kuwahamasisha Watanzania umuhimu wa Kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na Kuandika Katiba Mpya kabla ya Mwaka 2025. Kwa mazingira yaliyopo sasa ambapo Bunge la Tanzania limekuwa ni Bunge la Chama kimoja ambacho katika Ilani yake hawana hoja ya Tume Huru na Katiba Mpya, hatuwezi kutegemea mambo hayo kuanzishwa na Bunge hili. Hata hivyo, watu wa makundi yote watahamasishwa kushiriki Matembezi hayo pasipo kujali vyama na itikadi zao.

Kila mkoa au mji utakuwa na Timu ya Uratibu ambayo itasaidia kuratibu na kuandaa Matembezi hayo. Wale watakaopenda kusaidia au kuwezesha Matembezi hayo wataelekezwa kuwasiliana na Timu ya Uratibu ya Kitaifa itakayosaidia Uratibu kwa niaba ya Askofu. Timu hiyo ya Uratibu wa Kitaifa sambamba na Timu za Mikoani zitatangazwa mapema kuanzia Januari 2021 baada ya kuundwa.

Kwa taarifa hii, tunaomba Watanzania wote wajiandae kushiriki Matembezi hayo katika kila Mkoa. Matembezi hayo yataanza mapema mwaka 2021 na tarehe ya kila Mkoa itatangazwa na utaratibu wote. Kuanzia Januari 2021, Askofu atatangaza rasmi utaratibu wa namna ya kushiriki ikiwemo Waratibu wa Matembezi katika kila Mkoa.

Kwa Watanzania walioko nje ya Tanzania, Askofu anaweza kufika katika nchi hizo endapo wataweza kuandaa mazingira.

Kwa sasa Askofu anamuomba kila mtu kusambaza ujumbe huu ili kuwaandaa Watanzania wote kwa matukio hayo ya kihistoria!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate.

Askof Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
 
Huyu mzee atulie asitafute matatizo na sirikali hauji kama hizo ndiyo silaha kubwa za sirikali kuwachapia wanyonge..

Vuta picha kuna tume huru ya uchaguzi ambayo ndani yake kuna viongozi waotokana na vyama vya siasa kila mmoja anapigania masirahi ya chama chake!

Vuta picha wakurugenzi siyo wasimamizi wakuu wa uchaguzi katika jmajimbo, makada watiifu.

Embe endelea kuvuta picha mwenyekiti na tume na mkurugenzi hawajateuliwa na mkuu wa kaya kulinda masirahi yake na badae kugonga mvinyo pamoja katika hafla fupi baada ya ushindi wa mezani

Vuta picha wanachi wanapata mamlaka ya kumwajibisha mbuge au diwani ambae hatekelezi majukumu yake kama alivyoahidi kwenye kampeni yani anaondolewa hata kabla ya mitano tena kuisha.

Embu vuta picha mkuu wa kitengo hana tena kinga ya kisheria anashitakiwa baadaya ya kutoka madarakani kwa matumizi mabaya ya ofisi na kukanyaga katiba

Endelea kuzoom picha mjongeo mtetezi wa wanawake aka kazi mdungaye hana tena kinga kikatiba anashitakiwa tu kama raia wengine..

Wataweza kweli kuleta katiba mpya?
 
Hili ndilo suala la msingi kabisa! Tena tumechelewa mnoo!

Katiba hii inaruhusu mtu au watu wawe juu ya sheria za nchi. Sababu kuu ni hakuna “accountability”

Katiba yeyote iatakayoandikwa Jiwe akiwa madarakani itakuwa Mbaya zaidi kwa ustawi wa nchi kuliko hii ya sasa!!! Tupate TUME HURU KWANZA itakayosimamia Uchaguzi uliokuwa huru na wabunge watakaopatikana ndio washiriki kuunda katiba ya wananchi!!! Penginepo watabaka tena matakwa ya wananchi kutaka katiba yao kama walivyofanya enzi ya Vasco Dagama!!! CCM ya Magufuli sio chama cha siasa bali ni CULT; atakalo yeye ndlo hakuna wa kupinga!!!
 
Tutaliona jeshi la polisi linaanza mazoezi mitaani kama lilivyofanya wakati wa uchaguzi.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom