Hili ni kati ya mawazo ya hovyo sana katika uongozi wa taifa kiuchumi. Kupandisha mishahara kunasababisha gharama za maisha pia zipande na inflation kuongezekaa nathamani ya shillingi kutelemka; ndiyo mambo yaliyovuruga thamani ya shilingi kutoka dola 1 kwa shilling 5 hadi kufikia leo dola 1 kwa shilingi ~2300+. Kenya wana curreny stable sana kwa sababu hawapandishipandishi mishahara yao kufurahisha wapiga debe.
Hata Marekani mishahara yao imekuwa hivi ilivyo kwa zaidi ya miaka 15; ile 1% -3.5% adjustement ya inflation inategemea sana na namba za iflation mwaka huo, siyo wanasiasa kusema tu kuwa wamepandisha mishahara ya watumishi wote.
Wakati wa Magufuli mishahara haikupanda, lakini pia inflation haikupanda, na hivyo thamani ya shillingi ikabaki pale pale kwa muda wote wa utawala wake hadi anatangulia mbele ya haki.