Makuku Rey
JF-Expert Member
- Dec 31, 2013
- 3,497
- 3,823
Baba Askofu mi na familia yangu tunaelewa mchango wako katika kulipigania taifa hili,uliyoongea hapo akiyafanyia kazi hakika ataongoza miaka 10 Ila akikengeuka anajua Mungu..........
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yeah watu waweza kuchangia kifo cha mtu. Kumsema vibaya wakimsema vibayaWalilifahamu hilo walipopendekeza jina 2015.
Yaonekana kila kitu kilipangwa na yaonekana hata yeye alikuwa akifahamu hilo.
Ila kashikashi za chuki kutoka pande zote za dunia ndizo zimechangia kwa kiasi kikubwa.
Wewe wasemaKwanini maaskofu na wachungaji wanaipambania sana Chadema?
Chadema ni chama cha Kikristo?
Na kawaacha masikini kweli kweli!
CCM msirudie hili kosa tena la kuleta mtu mwenye ugonjwa usiotibika.
Ogopa Sana kuombewa mabaya na mahakama ya Jamii. Watu wakikulaani Mungu hawezi kuwa upande wako. Baraka na laana ya mtu imo ndani ya ulimi wake.Yeah watu waweza kuchangia kifo cha mtu. Kumsema vibaya wakimsema vibaya
ZilipendwaKwa hii historia, Magufuli alirisk sana uhai wake kubeba jukumu la kuhudumia wananchi
Ni upendo
Usimsahau na Shekhe PondaKwanini maaskofu na wachungaji wanaipambania sana Chadema?
Chadema ni chama cha Kikristo?
Maandishi yako ni mazuri, lakini yanaelezea kitu kimoja tu: aongoze, asitawale, na afuate katiba na sheria za nchi. Marehemu alitawala kwa matakwa yake na kuisigina katiba. Suluhu upinzani wake mkuu ni CCM, chama kusichotaka aina yoyote ya mageuzi endelevu, kisicho simamia au kukubali siasa za ushindani.Mpendwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan!
Kama nilivyoandika hapo awali, ninapenda kuchukua tena nafasi hii kutoa salaam zangu za pole kwako wewe binafsi kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Hakika, hiki ni kipindi kigumu sana kwako wewe binafsi na kwa Tanzania kama Taifa na nchi.
Imenipasa katika kipindi hiki cha Maombolezo haya makubwa kushiriki katika kutoa maoni, maonyo na ushauri kuhusu mambo muhimu yaliyo na maslahi mapana kwa Taifa ambayo hayana budi kufanyika ili kuliweka Taifa pamoja. Ninaona ni muhimu haya kuyasema sasa wakati ambao pia nchi inajiandaa kupokea mabadiliko makubwa ya kiuongozi.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuanzia sasa wewe ndiye utakayekuwa Rais wa nchi kwa kipindi chote cha miaka minne na nusu iliyosalia. Ninaahidi kuendelea kukuombea wewe pamoja na Serikali yako katika jukumu hili zito.
Ni kwa sasabu hiyo, mimi Askofu Mwamakula, nisimamaye katika zamu yangu kama mtumishi wa Mungu katika zama hizi, ninao wajibu wa kukuangaliza mambo kadhaa lakini yaliyo ya muhimu ambayo itakupasa uyatafakari sana wakati huu unapoanza safari ya kuliongoza Taifa hili (Ezekieli 33:1-20)!
Ninapenda kukurejesha wewe pamoja na washauri wako katika tukio kama hili lililotukia miaka mingi iliyopita muda mfupi mara baada ya kifo cha Mfalme Sulemani ambapo mrithi wake alijikuta katika wakati mgumu kufuatia kukataa ushauri wa wazee na kufuata ushauri wa vijana wahuni. Tukio hilo limetunzwa vizuri kama kumbukumbu katika Biblia Takatifu katika Kitabu cha 1Wafalme 12:1-24 na Kitabu cha 2Mambo ya Nyakati 10:1-11:4.
Ni kwa sababu hiyo, mimi pamoja na wengine tunaona mambo yafuatayo ni ya muhimu sana kwa uongozi wako kuyarekebisha ili kuliunganisha Taifa lililogawanyika:
1. Tunashauri utawala mpya uondoe zuio la Vyama vya Siasa kufanya Siasa na hivyo mruhusu mikutano ya hadhara katika nchi nzima na mambo yote ya kisiasa yaliyoruhusiwa na Katiba ya Nchi.
2. Tunashauri utawala mpya uwaachie huru wafungwa wote wa kisiasa na kufuta kesi pamoja na kuwaachilia huru Mahabusu wote wanaoshikiliwa katika Mahabusu na Magereza zote nchini kwa tuhuma za kisiasa ambazo zimepewa majina ya uchochezi, uhujumu uchumi, utakatishaji fedha, madawa ya kulevya nk.
3. Tunashauri utawala mpya ujenge mazingira ya kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi ili Chaguzi ndogo zote (by-elections) zinazofuata pamoja na Uchaguzi Mkuu ujao visimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi.
4. Tunashauri utawala mpya usikilize maoni ya makundi mbalimbali nchini yanayodai Katiba Mpya na ujenge mazingira ya kuanza upya kwa mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya ili Uchaguzi Mkuu ujao ufanyike chini ya Katiba Mpya.
5. Tunashauri utawala mpya uachie Vyombo vya Habari kufanya kazi zao kwa Uhuru pasipo kuingiliwa na dola.
6. Tunashauri utawala mpya uanzishe mazungumzo na Vyama vya Upinzani nchini ili kufanya maridhiano kuhusu namna ya kufanya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao uliharibiwa mwaka 2019.
7. Tunashauri utawala mpya uangalie na kurekebisha mazingira ya wafanyabiashara na Taasisi mbalimbali nchini ikiwemo kuzifungua Akaunti zilizozuiliwa kwa sababu mbalimbali hasa ambazo mazingira ya kufungiwa kwazo yalikuwa na harufu za kisiasa.
8. Tunashauri utawala mpya uache kutumia Vyombo vya Dola hasa Jeshi la Polisi katika kuhujumu vyama vya Upinzani na makundi mbalimbali yanayotetea Haki nchini.
9. Ikiwa njia ya maridhiano, tunashauri utawala mpya ufungue milango ya mazungumzo na maridhiano kwa kutoa mwaaliko kwa wanasiasa, wanaharakati na Wafanyabiashara walio uhamishoni warudi nchini.
10. Tunashauri utawala mpya ufungue majadiliano na maridhiano na viongozi wa Vyama vya Upinzani kuhusu malalamiko yao kufuatia Uchaguzi Mkuu uliopita.
11. Tunashauri utawala mpya uwapandishe madaraja Watumishi wa umma wanaostahili pamoja na kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wote.
Tunapenda kukuhakikishia kuwa sisi viongozi wa dini ambao tumejipambanua katika kutetea Haki na kusema kweli katika nchi hii tutatoa ushirikiano kwa utawala mpya kwa kila jema litakalofanywa kwa ajili ya kuweka upya na kuendeleza misingi ya Haki na Maridhiano katika nchi yetu.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfutate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
View attachment 1729054
Hakuna kiongozi dhaifu, bali walikuwa chini ya kiongozi 'haambiliki' na wakabuni mbinu ya kuishi, ya kumsifia na kumpamba hata akiharibu.Askofu amesema yote, cha msingi ambacho mama anatakiwa kukiona mapema ni kuhusu viongozi almost wote waliofanya kazi na Hayati, wameonesha udhaifu mkubwa sana. Ni waongo wa wazi, wana dharau, wana viburi, ni wajeuri na wengi ni wasema hovyo, kwa ufupi hawana karama ya uongozi, labda wanafaa kuwa askari wanyamapori wakapambane na majangili, maana hakuna negotiation kati ya jangili na askari, au wakawe askari magereza napo nina wasiwasi kama hawatakandamiza haki za wafungwa.
Kingine ambacho binafsi nimekiona kuwa ni tatizo ni hili la vipngozi wanaopewa nafasi za kisiasa wanaotokana na TISS, hawa pia wameprove failure kubwa sana labda kwa sababu ya nature ya kazi yao, "kureport na kutekeleza order". Kiutendaji hiki kinawaathiri hawawezi kuwa wabunifu zaidi ya kusubiri "maelekezo kutoka juu" kama ambavyo walivyozoea wakiwa huko.
Si kwa ubaya, nachotaka kieleweke hapa ni kuwa kila kazi ina "culture" yake, na culture hiyo inaweza kumuathiri mhusika akitolewa katika majukumu yake ya awali na kupewa kofia ya kisiasa. Hawa wanafaa waendelee kupenyezwa tu kama ilivyo ada, ili kukusanya taarifa za sehemu husika na kuzipeleka zinakotakiwa, wakipewa VITI wanatuchelewesha kwakua wamezoea kuishi kwa kufungwa mikono.
Apumzike kwa amani mzee wetu JPM.
Maa dishi yako ni mazuri, lakini yanaelezea kitu kimoja tu: aongoze, asitawale, na afuate katiba na sheria za nchi. Marehemu alitawala kwa matakwa yake na kuisigina katiba. Suluhu upinzani wake mkuu ni CCM, chama kusichotaka aina yoyote ya mageuzi endelevu, kisicho simamia au kukubali siasa za ushindani.
Hakuna kiongozi dhaifu, bali walikuwa chini ya kiongozi 'haambiliki' na wakabuni mbinu ya kuishi, ya kumsifia na kumpamba hata akiharibu.
Na Majaliwa usimsahau, hakuwahi msaidia marehemu. Zama fulani mfalme aliugua kichaa. Aliamuru kuuwawa wazibua vyoo na mitaro, akidai hawana akili. Waziri mkuu alimwambia,' hewala mfalme, lakini nasi tujiandae kuuawa. Maadamu tunakula na kunya, vyoo na mitaro vitaziba, na kila azibuaye ata uawa, hatimae tutabaki sisi na atakaepangwa kuzibua nae atauawa' mfalme kichaa yakamwingia na kufuta amri. Majaliwa wetu hakuwahi kuthubutu, mpaka hatua ya mwisho kuongopa kuwa jpm ni mzima wa afya.Kitendo cha kutumia task force kuwapora wafanyabiashara mali zao pesa zao Madini yao na wengine kufungiwa Account zao biashara zao huku baadhi wakiikimbia Nchi mpaka sasa kilikuwa kitendo Hatari na huenda laana kubwa imetokea huko.
Viongozi waliopo wajifunze utawala bora. Ndugu wa jpm wana majonzi makubwa, masimango yanayo elekezwa kwa marehemu kwa utawala wa kidhalmu alio utekeleza yana watesa zaidi.Kwanini lakini aliamua kuwa katili kiasi kile?
I cry for him[emoji24]
Lakini sijapata sababu za msingi za kutunyima uhuru wetu kusema kweli.
Nakumbuka kabla hajawa rais nimepanda basi la Dar Tanga ,watu wanamkosoa rais bila kuogopa chochote na hakuna anayewatishia jela.
Kwanini lakini hiki kizazi cha vitisho kimefanya baadhi ya watu wafurahie msiba wa kiongozi mkubwa?
Kwanini imekuwa hivi?
Musiba anaweza tishia mtu yeyote uhai lakini bado akaonekana ni wa maana. KWANINI?[emoji24]
Ningependa Jembe lirudi lirekebishe yote haya.
Central line imefanyiwa ukarabati mkubwa. Hela ya SGR ingetumiwa kujenga madarasa na kuajiri walimu, leo ajira kwa kada hiyo ingekuwa historia. Na karibu 10% ya hela hiyo hurudi serikali I kama payee.Asisahau ajira kwa kada mbali mbali kama ualimu, udaktari na zinginezo ambazo wahitimu wake wamejazana mitaani bila kazi maalumu huku kukiwa na uhitaji mkubwa sana wa madaktari mahospitalini na walimu mashuleni.
Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Huyu kijana Sabaya watu wanavyomlaani vibaya, karma itamshugulikia kama ilivyomshugulikia baba yake aliyetangulia..Madame President ameanza kuonesha dalili nzuri za kulionganisha taifa na watu wake kuwa kitu kimoja, hata waliokua wakimpinga Marehemu Magufuli wameanza kuonesha dalili za kumuunga mkono Madame President. REF: Kigogo2014, Tundu Atipass Lissu, Askofu Mwamakula, Godbless Lema na wengine wapingaji katika mitandao kama JF/Twitter/Insta.
Nina amini, Madame President akitumia busara kama aliotumia Rais Hussein Mwinyi kuwaonganisha wazanzibari kuwa kitu kimoja licha ya itikadi zao za kichama na mengine, sambamba na kuto watetea viongozi na wasio na busara katika kazi zao (Viongozi wanao wachapa na kuwaonea raia kina Ole Sabaaya/Makonda/Cyprian Musiba, basi Madame atafaulu sana.
Muhimu, awakumbuke vijana wasio na ajira, wastaafu, wapinzani, waajiriwa wanao stahiki nyongeza ya mishahara na madaraja, wafanya biashara na waliofungwa kisiasa na visasi. Atafaulu katika utawala wake.
Atekeleze haya haraka iwezekanavyo ili tuweze kupunguza nyasi kwenye njia ya kuelekea msalani zilizomea kwa kipindi cha miaka takribani 6 iliyopita.
Awe kiongozi wa malaika watoa roho ama?Alijitoa, na tunamshukuru kwa hilo. Mungu akamfanye kiongozi wa malaika wake mbinguni.