Askofu Mwamakula: Mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan, mambo yafuatayo ni muhimu

Hivi Lissu hizo kejeli na dharau anazotoa atarudi Tz kweli na kuishi salama? Magu ana watu wengi wanaompenda wapo tayari kufanya lolote kutetea heshima yake, Lissu ajichunge sana, binadamu wote tutakufa ila ajue tu na yeye anatafutwa kwenye 18 saivi.
wewe ccm, jinga kabisa, kampeni akma Lisu hapendwi ulizoaje? shallow analysisi
 
Niache na shallow analysis yangu, ila mwambie arudi tuone kama atakaa kwa amani, yeye amekejeli na kushangilia kifo cha Magu, walimwengu watamfunza vyema.
 
Kwanini maaskofu na wachungaji wanaipambania sana Chadema?

Chadema ni chama cha Kikristo?
SIjaona kama imetajwa kwenye hilo andiko, zaidi Askofu Mwamakula kataja WAPINZANI, ambao ni zaidi ya Chadema.
 
Jifunzeni sasa kutoa kauli nzuri.
Tulia uone Magufuli alivyoandaa wasaidizi makini, hakua na ubaguzi na hakujali jinsia.... pale ikuluikulu tunae mama Samia na kule bungeni CHADEMA mnawakilishwa na wale wabunge wamama 20

Mwaka wa wamama huu

Mungu ibariki Tanzania
 
Acha uongo.
Makamu wa rais alisema ugonjwa ulikuwa ni atrial fibrillation,ambao ni either treatable or it's effects adjustable and the patient can live his life.
So ulitaka asife ama unataka kusemaje mkuu..

Ndugu yangu, watu wanaokufa kwa mgonjwa yanayotibika ni wengi zaidi, tumeambiwa ugonjwa kadumu nao zaidi ya miaka 10 hv.

Wakat umefika, hakuna ujanja katika hilo
 
Mpendwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan!

Kama nilivyoandika hapo awali, ninapenda kuchukua tena nafasi hii kutoa salaam zangu za pole kwako wewe binafsi kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Hakika, hiki ni kipindi kigumu sana kwako wewe binafsi na kwa Tanzania kama Taifa na nchi.

Imenipasa katika kipindi hiki cha Maombolezo haya makubwa kushiriki katika kutoa maoni, maonyo na ushauri kuhusu mambo muhimu yaliyo na maslahi mapana kwa Taifa ambayo hayana budi kufanyika ili kuliweka Taifa pamoja. Ninaona ni muhimu haya kuyasema sasa wakati ambao pia nchi inajiandaa kupokea mabadiliko makubwa ya kiuongozi.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuanzia sasa wewe ndiye utakayekuwa Rais wa nchi kwa kipindi chote cha miaka minne na nusu iliyosalia. Ninaahidi kuendelea kukuombea wewe pamoja na Serikali yako katika jukumu hili zito.

Ni kwa sasabu hiyo, mimi Askofu Mwamakula, nisimamaye katika zamu yangu kama mtumishi wa Mungu katika zama hizi, ninao wajibu wa kukuangaliza mambo kadhaa lakini yaliyo ya muhimu ambayo itakupasa uyatafakari sana wakati huu unapoanza safari ya kuliongoza Taifa hili (Ezekieli 33:1-20)!

Ninapenda kukurejesha wewe pamoja na washauri wako katika tukio kama hili lililotukia miaka mingi iliyopita muda mfupi mara baada ya kifo cha Mfalme Sulemani ambapo mrithi wake alijikuta katika wakati mgumu kufuatia kukataa ushauri wa wazee na kufuata ushauri wa vijana wahuni. Tukio hilo limetunzwa vizuri kama kumbukumbu katika Biblia Takatifu katika Kitabu cha 1Wafalme 12:1-24 na Kitabu cha 2Mambo ya Nyakati 10:1-11:4.

Ni kwa sababu hiyo, mimi pamoja na wengine tunaona mambo yafuatayo ni ya muhimu sana kwa uongozi wako kuyarekebisha ili kuliunganisha Taifa lililogawanyika:

1. Tunashauri utawala mpya uondoe zuio la Vyama vya Siasa kufanya Siasa na hivyo mruhusu mikutano ya hadhara katika nchi nzima na mambo yote ya kisiasa yaliyoruhusiwa na Katiba ya Nchi.

2. Tunashauri utawala mpya uwaachie huru wafungwa wote wa kisiasa na kufuta kesi pamoja na kuwaachilia huru Mahabusu wote wanaoshikiliwa katika Mahabusu na Magereza zote nchini kwa tuhuma za kisiasa ambazo zimepewa majina ya uchochezi, uhujumu uchumi, utakatishaji fedha, madawa ya kulevya nk.

3. Tunashauri utawala mpya ujenge mazingira ya kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi ili Chaguzi ndogo zote (by-elections) zinazofuata pamoja na Uchaguzi Mkuu ujao visimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi.

4. Tunashauri utawala mpya usikilize maoni ya makundi mbalimbali nchini yanayodai Katiba Mpya na ujenge mazingira ya kuanza upya kwa mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya ili Uchaguzi Mkuu ujao ufanyike chini ya Katiba Mpya.

5. Tunashauri utawala mpya uachie Vyombo vya Habari kufanya kazi zao kwa Uhuru pasipo kuingiliwa na dola.

6. Tunashauri utawala mpya uanzishe mazungumzo na Vyama vya Upinzani nchini ili kufanya maridhiano kuhusu namna ya kufanya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao uliharibiwa mwaka 2019.

7. Tunashauri utawala mpya uangalie na kurekebisha mazingira ya wafanyabiashara na Taasisi mbalimbali nchini ikiwemo kuzifungua Akaunti zilizozuiliwa kwa sababu mbalimbali hasa ambazo mazingira ya kufungiwa kwazo yalikuwa na harufu za kisiasa.

8. Tunashauri utawala mpya uache kutumia Vyombo vya Dola hasa Jeshi la Polisi katika kuhujumu vyama vya Upinzani na makundi mbalimbali yanayotetea Haki nchini.

9. Ikiwa njia ya maridhiano, tunashauri utawala mpya ufungue milango ya mazungumzo na maridhiano kwa kutoa mwaaliko kwa wanasiasa, wanaharakati na Wafanyabiashara walio uhamishoni warudi nchini.

10. Tunashauri utawala mpya ufungue majadiliano na maridhiano na viongozi wa Vyama vya Upinzani kuhusu malalamiko yao kufuatia Uchaguzi Mkuu uliopita.

11. Tunashauri utawala mpya uwapandishe madaraja Watumishi wa umma wanaostahili pamoja na kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wote.

Tunapenda kukuhakikishia kuwa sisi viongozi wa dini ambao tumejipambanua katika kutetea Haki na kusema kweli katika nchi hii tutatoa ushirikiano kwa utawala mpya kwa kila jema litakalofanywa kwa ajili ya kuweka upya na kuendeleza misingi ya Haki na Maridhiano katika nchi yetu.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfutate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani

View attachment 1729054
Mimi pia namshauri asiwe mpenda sifa. Tbc ambayo ni television ya umma, imefanya kazi kubwa sana ya kumsifu, kumtukuza mh. Magufuli, akiwa hai na baada ya kufariki. Hivi baada ya mazishi tbc itafanya kazi gani?
 
Hii ngoma mama hatoicheza tuwe wakweli...ni mwanamke mzanzibari mstaarabu sana,muungwana,mwenyehuruma,mpole mwenye sura na sauti laini mororo!! Hivi sio vigezo vya kuiongoza Tz
Tz hii yenye kina lissu,sugu,Lena,mdee,mnyika,mbowe,makonda,chenge,rostam,kigogo,mange,msigwa,nape,member,msukuma,KESSY, nk.
Yetu macho,wacha ngoma ianze natunaanza na bluzi/rnb kisha tutaingia rege afu turudi sasa mdundiko,mdumange,mchiriku,baikoko,mnanda,lizombe,singeli nk. Tunaomba azicheze bila kuchoka nshalaa!!
 
Mwamakula katoa maoni mema kabisa. Huyu amekuwa kiongozi wa kwanza mwenye maono mema. Lissu, Mzee Warioba, Butiku? Kikwete, Mwinyi? spent force), Roman Catholics authority and other elders of this country watoke watoe maono ya kulinusuru taifa.
Mkuu mbona maoni na kauli zao ziko kwenye katiba ya JMT
 
Askofu amesema yote, cha msingi ambacho mama anatakiwa kukiona mapema ni kuhusu viongozi almost wote waliofanya kazi na Hayati, wameonesha udhaifu mkubwa sana. Ni waongo wa wazi, wana dharau, wana viburi, ni wajeuri na wengi ni wasema hovyo, kwa ufupi hawana karama ya uongozi, labda wanafaa kuwa askari wanyamapori wakapambane na majangili, maana hakuna negotiation kati ya jangili na askari, au wakawe askari magereza napo nina wasiwasi kama hawatakandamiza haki za wafungwa.

Kingine ambacho binafsi nimekiona kuwa ni tatizo ni hili la vipngozi wanaopewa nafasi za kisiasa wanaotokana na TISS, hawa pia wameprove failure kubwa sana labda kwa sababu ya nature ya kazi yao, "kureport na kutekeleza order". Kiutendaji hiki kinawaathiri hawawezi kuwa wabunifu zaidi ya kusubiri "maelekezo kutoka juu" kama ambavyo walivyozoea wakiwa huko.

Si kwa ubaya, nachotaka kieleweke hapa ni kuwa kila kazi ina "culture" yake, na culture hiyo inaweza kumuathiri mhusika akitolewa katika majukumu yake ya awali na kupewa kofia ya kisiasa. Hawa wanafaa waendelee kupenyezwa tu kama ilivyo ada, ili kukusanya taarifa za sehemu husika na kuzipeleka zinakotakiwa, wakipewa VITI wanatuchelewesha kwakua wamezoea kuishi kwa kufungwa mikono.

Apumzike kwa amani mzee wetu JPM.
Hivi binti kiziwi hadi leo wewe ni binti
 
Hili ni kati ya mawazo ya hovyo sana katika uongozi wa taifa kiuchumi. Kupandisha mishahara kunasababisha gharama za maisha pia zipande na inflation kuongezekaa nathamani ya shillingi kutelemka; ndiyo mambo yaliyovuruga thamani ya shilingi kutoka dola 1 kwa shilling 5 hadi kufikia leo dola 1 kwa shilingi ~2300+. Kenya wana curreny stable sana kwa sababu hawapandishipandishi mishahara yao kufurahisha wapiga debe.

Hata Marekani mishahara yao imekuwa hivi ilivyo kwa zaidi ya miaka 15; ile 1% -3.5% adjustement ya inflation inategemea sana na namba za iflation mwaka huo, siyo wanasiasa kusema tu kuwa wamepandisha mishahara ya watumishi wote.

Wakati wa Magufuli mishahara haikupanda, lakini pia inflation haikupanda, na hivyo thamani ya shillingi ikabaki pale pale kwa muda wote wa utawala wake hadi anatangulia mbele ya haki.
Mawazo yako tu, kwa nini sasa bidhaa kama za vyakula na material ya ujenzi yalipanda kiholela sana enzi yake ukilinganisha hata na enzi ya Mkapa ingawa mkapa alipandisha mishahara?????
 
Waovu siku zote hawajiamini waache chadema wanamatatizo makubwa basi tu ni rahisi kuona boriti kwenye jicho la mwenzako hivyo waache waendelee
Nawe ukaliona boriti jichoni mwa chadema!
 
Kumbe kiuno ni ub00, basi hata mie ninao
Kwenye biblia kuandikwa maneno kama 'kumjua' kumaanisha 'kufanya ngono' ni kawaida. Unawajua wanaume wangapi? Kama utatumia logic ya biblia hapo una body count ngapi
 
Kama wakati wa Magufuli waliufyata basi Waendelee kuufyata wamuache Mama afanye anavyojua. Akiwahitaji Kwa ushauri atawauliza..

Vidomodomo na kiherehere cha kushauri. Wangefanya wakati wa Magufuli..kama wanajua Sana kushauri
Magufuli alisema wazi hashauriki.
 
Mpendwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan!

Kama nilivyoandika hapo awali, ninapenda kuchukua tena nafasi hii kutoa salaam zangu za pole kwako wewe binafsi kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Hakika, hiki ni kipindi kigumu sana kwako wewe binafsi na kwa Tanzania kama Taifa na nchi.

Imenipasa katika kipindi hiki cha Maombolezo haya makubwa kushiriki katika kutoa maoni, maonyo na ushauri kuhusu mambo muhimu yaliyo na maslahi mapana kwa Taifa ambayo hayana budi kufanyika ili kuliweka Taifa pamoja. Ninaona ni muhimu haya kuyasema sasa wakati ambao pia nchi inajiandaa kupokea mabadiliko makubwa ya kiuongozi.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuanzia sasa wewe ndiye utakayekuwa Rais wa nchi kwa kipindi chote cha miaka minne na nusu iliyosalia. Ninaahidi kuendelea kukuombea wewe pamoja na Serikali yako katika jukumu hili zito.

Ni kwa sasabu hiyo, mimi Askofu Mwamakula, nisimamaye katika zamu yangu kama mtumishi wa Mungu katika zama hizi, ninao wajibu wa kukuangaliza mambo kadhaa lakini yaliyo ya muhimu ambayo itakupasa uyatafakari sana wakati huu unapoanza safari ya kuliongoza Taifa hili (Ezekieli 33:1-20)!

Ninapenda kukurejesha wewe pamoja na washauri wako katika tukio kama hili lililotukia miaka mingi iliyopita muda mfupi mara baada ya kifo cha Mfalme Sulemani ambapo mrithi wake alijikuta katika wakati mgumu kufuatia kukataa ushauri wa wazee na kufuata ushauri wa vijana wahuni. Tukio hilo limetunzwa vizuri kama kumbukumbu katika Biblia Takatifu katika Kitabu cha 1Wafalme 12:1-24 na Kitabu cha 2Mambo ya Nyakati 10:1-11:4.

Ni kwa sababu hiyo, mimi pamoja na wengine tunaona mambo yafuatayo ni ya muhimu sana kwa uongozi wako kuyarekebisha ili kuliunganisha Taifa lililogawanyika:

1. Tunashauri utawala mpya uondoe zuio la Vyama vya Siasa kufanya Siasa na hivyo mruhusu mikutano ya hadhara katika nchi nzima na mambo yote ya kisiasa yaliyoruhusiwa na Katiba ya Nchi.

2. Tunashauri utawala mpya uwaachie huru wafungwa wote wa kisiasa na kufuta kesi pamoja na kuwaachilia huru Mahabusu wote wanaoshikiliwa katika Mahabusu na Magereza zote nchini kwa tuhuma za kisiasa ambazo zimepewa majina ya uchochezi, uhujumu uchumi, utakatishaji fedha, madawa ya kulevya nk.

3. Tunashauri utawala mpya ujenge mazingira ya kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi ili Chaguzi ndogo zote (by-elections) zinazofuata pamoja na Uchaguzi Mkuu ujao visimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi.

4. Tunashauri utawala mpya usikilize maoni ya makundi mbalimbali nchini yanayodai Katiba Mpya na ujenge mazingira ya kuanza upya kwa mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya ili Uchaguzi Mkuu ujao ufanyike chini ya Katiba Mpya.

5. Tunashauri utawala mpya uachie Vyombo vya Habari kufanya kazi zao kwa Uhuru pasipo kuingiliwa na dola.

6. Tunashauri utawala mpya uanzishe mazungumzo na Vyama vya Upinzani nchini ili kufanya maridhiano kuhusu namna ya kufanya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao uliharibiwa mwaka 2019.

7. Tunashauri utawala mpya uangalie na kurekebisha mazingira ya wafanyabiashara na Taasisi mbalimbali nchini ikiwemo kuzifungua Akaunti zilizozuiliwa kwa sababu mbalimbali hasa ambazo mazingira ya kufungiwa kwazo yalikuwa na harufu za kisiasa.

8. Tunashauri utawala mpya uache kutumia Vyombo vya Dola hasa Jeshi la Polisi katika kuhujumu vyama vya Upinzani na makundi mbalimbali yanayotetea Haki nchini.

9. Ikiwa njia ya maridhiano, tunashauri utawala mpya ufungue milango ya mazungumzo na maridhiano kwa kutoa mwaaliko kwa wanasiasa, wanaharakati na Wafanyabiashara walio uhamishoni warudi nchini.

10. Tunashauri utawala mpya ufungue majadiliano na maridhiano na viongozi wa Vyama vya Upinzani kuhusu malalamiko yao kufuatia Uchaguzi Mkuu uliopita.

11. Tunashauri utawala mpya uwapandishe madaraja Watumishi wa umma wanaostahili pamoja na kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wote.

Tunapenda kukuhakikishia kuwa sisi viongozi wa dini ambao tumejipambanua katika kutetea Haki na kusema kweli katika nchi hii tutatoa ushirikiano kwa utawala mpya kwa kila jema litakalofanywa kwa ajili ya kuweka upya na kuendeleza misingi ya Haki na Maridhiano katika nchi yetu.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfutate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani

View attachment 1729054
Mzee kuna Masheikh wapo jela umesahau kuwasemea au kwakua wewe ni Askofu.
 
Kwanini maaskofu na wachungaji wanaipambania sana Chadema?

Chadema ni chama cha Kikristo?
Hii ni hulka ya binadamu kamili, akiona mtu anaadhibiwa hata kama ni mkosaji atasema asamehewe. Ndio maana Mungu anatuagiza tusamehe
 
Back
Top Bottom