Askofu Mwamakula: Ole kwa Taifa lisilotenda HAKI kwa watu wake! Unamkamata mtu eti upelelezi haujakamilika karne hii?

awamu hii dhuruma ndo imeongezeka zaidi kwakweli
 
Hilo neno la kila mamlaka imetoka kwa Mungu ni tafsiri potofu ya maneno ya Kristo toka kwenye biblia ya Kigiriki. Tafsiri sahihi ni kuwa kila mamlaka Mungu ameiruhusu. Mamlaka ya utawala, Mungu anaweza kuruhusu kuwepo kwake kama adhabu kwa watawaliwa, yaani sawa kama alivyomruhusu shetani amjaribu Ayoub, au alivyoruhusu wana wa Israel wawekwe utumwani kutokana na kutoyatii maagizo yake.

Ni wakati wa kujiuliza sisi wananchi wa Tanzania, tumemkosea nini Mungu wetu hata akaruhusu tuwe chini ya mamlaka zenye kutenda dhuluma?

Neno la Mungu linasema, mtawala awe kama jabali lenye kutoa kivuli jangwani ambalo watu wake hujikinga dhidi ya jua. Pia linanena kuwa mfalme awe kama kijito cha maji kinachotiririka maji kati kati ya ardhi kame.

Mtawala hastahili kuwa chanzo cha mateso na dhuluma dhidi ya watu wake, bila ya kujali watu wake hao ni wadhambi au ni wenye haki.
 
Ndio.Ndio maana huwa tunapiga kura kuchagua madiwani na Wabunge ili wao wawakilishe mawazo yetu huko.mbele sisi tuendelee kuchapa kazi kwenye taaluma zetu
Hayo mawazo yenu wanayatoa wapi wakati ninyi hamsemi na mko bissy na kazi zenu za specialization?
 
Sidhani kama unajielewa, na hutakaa ujielewe kamwe. Tuko hapa tulipo kutoakana na watu kama wewe wasiojitambua.
 
Maaskofu wauza dawa za kulevya hawafai,hicho ni kivuli tu
 
Mkuu Kazi mojawapo ya kiongozi wa Dini ni kukemea maovu..

Mkemee Jiwe aliyegeuka kuwa pedeshee wakati siyo kazi yake.
 
Mbona hamlisemi lile kundi lenu CCM mliloliunda la Manabii na Mitume ambao kila kukicha wanazurula kwenye misafara ya Rais kumuombea tukiachilia mbali kanisa la mama Lwakatare kuwa tawi la CCM! Nyie ni watu wabaya sana mnaopenda dhuruma, manyanyaso na maonezi dhidi ya binaadamu wenzenu. Kheri ya anayekemea maovu kuliko anayegawa mapesa huku akitenda maovu.
 

Kwahiyo ukiona mahali haki haitendeki usiseme?
 
Hapo hoja yako ni nini ?!. Mbona aibu [emoji23][emoji1787]
 
Nje ya mada.

Nachikiona kwa sasa JF inaelekea kupoteza ule mvuto wake wa huko nyuma. Kuna makundi ya wafia vyama yameiteka JF, kazi yao kuu ni kuvuruga mijadala yote isiyowapendeza. Si ajabu kukuta mtu ametoa bandiko zuri lenye hoja kadhaa, lakini watakuja waCHADEMA et al na WaCCM watajikita kujadili kuhusu watoa hoja na si kujadili hoja husika kwa kuonesha ubora na udhaifu wake bali kwa lengo mahususi kuvuruga mjadala husika.

Kwa mtazamo wangu, YEHODAYA hapa amekuja kwa lengo la kuvuruga huu uzi na kuhamisha ajenda iliwekwa na mtoa mada si kwa bahati mbaya. Baba askofu ametoa mtazamo wake kwa hoja lakini wamekuja wafia vyama vyao wamehamisha kabisa hoja zilizopo kwa kuanzisha mjadala mwingine wa kitoto kabisa.
 
Kazi ya kiongozi wa dini sio kuongelea maovu Ni kuongelea mambo ya Mungu
Kwa akili zako ulitaka au unategemea siku Mungu ashuke aje azungumze aliyosema Askofu hapo juu?so Mungu hachukizwi na uvunjaji wa haki za wengine siyo?
 
Ndio.Ndio maana huwa tunapiga kura kuchagua madiwani na Wabunge ili wao wawakilishe mawazo yetu huko.mbele sisi tuendelee kuchapa kazi kwenye taaluma zetu
Mbona wewe kila wakati mtandaoni unaongelea Mbowe na mambo mengi ya siasa? Ongelea taaluma yako ndo tutakuelewa. Wewe kila kukicha ni Chadema kafanya hivi, Mbowe kafanya hivi, Lisu kawa hivi mpaka watu wanahisi una mimba ya Mbowe?
 
Wewe umedhulumiwa nini !?
Mbona unajitia wazimu ?!. Rais mwenyewe kaenda gerezani Butimba na kukemea ubambikaji kesi !!. Kuanzia kesho yake tuliona makumi ya maelfu ya watu wakitolewa magerezani !!. Anapotokea mtu (Askofu) anakemea sheria zenye elements za kikoloni unaumia, tukueleweJe ?!. Kwamba kwako watu wakiwekwa ndani kwa uonevu ndiyo Amani ?!. Wafuasi wa ccm na serikali mnatia aibu sana.
 
unabii wa kweli.
IPO SIKU MTU FLANI ATAANGUKA JUKWANI NA KUKAUKA.
 
Kazi ya kiongozi wa dini sio kuongelea maovu Ni kuongelea mambo ya Mungu

Aisee, unaonekana unajibu kitu usichokielewa na humwelewi hata Mungu aliyekuumba...!!

Mungu aliyetuumba ni wa HAKI na UPENDO. Huwezi kumhubiri Mungu muumba wetu bila kujua haya mambo mawili....

Na sasa hebu rudi kwenye andiko la. Askofu, lisome tena mwanzo mwisho kwa makini. Utagundua kuwa, mantiki ya andiko zima imejikita kwenye HAKI na UPENDO miongoni mwetu binadamu....

Hizi ndizo sifa kuu za MUNGU huyu aliyetuumba kwa mfano wake...

Umeshawahi kujiuliza ni kwanini YESU KRISTO pamoja na kujikita kuhubiri habari ya HAKI na UPENDO na watu kutubu dhambi zao na kumrejea Mungu, lakini watawala wa Rumi ya wakati ule walimchukia sana na kumuona ya kuwa anawaharibia mipango na dili zao?

Ndiyo. Ni kwa sababu (Wanasheria, Mafarisayo, Masadukayo, Watoza Ushuru - sawa na TRA ya kwetu na Watawala/viongozi) waliongozwa na kutawaliwa na unafiki uliozaa uvunjivu wa HAKI za watu kwa ajili ya manufaa yao tu na siyo Mungu sawaswa na ilivyo leo....

Yes, wakamkamata na kumshitaki kwa makosa ya uongo, wakamtesa na kumhukumu KIFO kwa hila tu pasipo HAKI....

Hayo yaliyofanyika nyakati hizo ndiyo yanayofanyika leo ktk tawala za kibinadamu duniani kote na lugha yao haina tofauti yoyote na ya nyakati zile....

Husema "......HUBIRINI DINI na SIASA TUACHIENI SISI WANASIASA.....!!" lengo likiwa watu wasifumbuliwe macho na masikio na fahamu zao kutambua kuwa wanaongozwa na viongozi waovu wasio na UPENDO wala kutenda HAKI....!


Hawa kiuhalisia hawaelewi hata maana ya SIASA kama tu ulivyo wewe.

Ndo kusema: SIASA ndiyo huzaa SERIKALI = UTAWALA/UONGOZI. Uongozi maana yake ni kuongoza watu kwenye NEEMA....

Huwezi kuifikia NEEMA pasipo kuustawisha UPENDO na kuiacha HAKI itamalaki miongoni mwa jamii (watu).....

Mimi nasema SIASA na DINI ni inseparable.....haviachani hata chembe wala nukta moja....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…