Askofu Mwingira kauliza swali. Karibuni kwa majibu

Aliyosema hapo ukimwendea atoe ushahidi, hatathubutu kutoa kwa sababu anajua ugomvi wake na huyo anayemdhihaki kwamba, naye ni tapeli wa mashamba huko Sumbawanga!
 
Uhai siyo ushindi na kifo siyo hasara, halaumiwi aliekufa wala hapongezwi alie hai kwakua hakuna alieamua kwa ujanja wake.

Na uovu wa kumwaga damu pia ni dhambi mbele ya Mwenyezi Mungu, ila kifo na uhai siyo kipimo cha ushindi au kushindwa.
 
Hebu tuwe wakweli hasa kwasisi waamini LISSU alipangiwa kifo cha risasi na wanadamu ambao walisahau mipango ya Mungu si ya mwanadamu!

Huwa tunaepushwa mengi kwa namna ya ajabu na ya kipekee mno na mwisho wa siku tunaishia kumshukuru Mungu maana huko tunakovuka si kwa utashi wala si kwa akili zetu
 
Huoni bado anaishi?
Mchungaji mwigura hiyo kauli kaitoa kisiasa, kuwapa mileage chama chake,, kwani Lisu kaanza kuishi leo?,
Reagan alipigwa risasi za kifua, akaishi, Kennedy alipigwa risasi za kichwa akafa,, kati yao mshindi ni nani, na mshindwa no nani? 😄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…