Askofu Niwe Mugizi jimbo Katoliki Rulenge Ngara Kagera, kuongoza kampeni ya kupinga katiba mpya

Askofu Niwe Mugizi jimbo Katoliki Rulenge Ngara Kagera, kuongoza kampeni ya kupinga katiba mpya

Ningetamani na madhehebu au dini nyingine nao watoe matamko ya kuhamasisha waumini wao kukataa Jarida pendekezwa.
We handsomeboi endelea kufanya kazi zako za uhouseboi haya mambo ya katiba huyajui ndiyo maana unaongelea jarida pendekezwa. Sisi hatuna jarida pendekezwa tunaongolea Katiba Inayopendekezwa. Jitahidi kusoma Katiba Inayopendekezwa utafahamu mengi na utaipigia kura ya NDIYO
 
Askofu Niwemgizi wa jimbo Katoriki jimbo kuu Rulenge amesema ataongoza kampeni ya kura ya hapana kupinga katiba mpya.
Katika hili la kusema kuwa askofu niwemugizi wa jimbo la rulenge amesema ataongoza kampeni ya kupiga kura ya hapana,limenishangaza sana kwa kuwa kwanza nimeshangaa sana kwanza kiongozi huyu wa dini tunayemuheshimu sana anaingia katika mkumbo huu wa upotoshaji unaofanywa kwa kiasi kikubwa na watu wachache ambao hawana nia njema na nchi hii na wamekosa uzalendo na upendo kwa nchi yao,sasa najiuliza kiongozi huyu mkubwa katika kanisa katoliki anapogeuka mwanasiasa sisi waumini tunashika lipi? Siasa za askofu huyu? Au mafundisho ya kiroho? Tumesikitishwa sana na utaratibu huu wa viongozi wetu kuanza kazi ya siasa ndani ya kanisa.Sote tunatambua kuwa kanisa katoliki lilishajitenga na siasa na kubaki na jukumu la kuwajenga waumini wake kiroho,sasa katika hili nawashangaa sana maaskofu wangu hasa wewe askofu niwemugizi kuwa wito wako ni ukasisi au siasa? Tuambieni moja tujue kama kanisa letu ni chama cha siasa? Basi mbadili mfumo wa katoliki iwemoja ya vyama vya siasa.sisi waumini tuna akili timanu na tuna uwezo wa kujua mema na mabaya,hivyo tutaamua wenyewe na hamna haki nyie kama maaskofu kutuamulia au kutufanyia maamuzi eti tupige kura ya hapana kwa katiba inayopendekezwa.Kingine ni kuwa nyie viongozi wetu mnatuchanganya kwa kuwa inaonekana baadhi mna maslahi binafsi katika swala la katiba inayopendekezwa na hapa inaonekana mmejiunga na watu fulani fulani wenye siasa chafu,tuacheni waumini tuamue wenyewe kwani kuja kanisani huwa mnatupangia au ni kwautashi wetu na imani yetu,sasa iweje leo eti mnafanya kampeni za kutuhamasisha tupige kura ya hapana kwa katiba pendekezwa.Kauli ya kadinali pengo ilionyesha kuwa tunayo haki ya kuamua wenyewe kama waumini sasa haya madaraka yakuingia mpaka kwenye nyumba za waumini na kuwapangia kuwa pigeni kura ya hapana mmepewa na nani?hasa ww askofu niwemugizi,tuacheni waumini tuamue wenyewe.Nirudi kwa muandishi wa makala iliyozungumzia swala hili la askofu niwemugizi kufanya kampeni ya kutuhamasisha wakatoliki tupige kura ya hapana kwa katiba pendekezwa,ndg yangu isango nadhani umepotoka sana hivyo nakushauri urudi ukashike chaki au umwombe askofu wako akurudishe seminarini ukajipange tena,then ukafanye kazi ya utumishi kuliko kazi unayofanya sasa ya siasa za upotoshaji huku ukivaa koti la uandishi wa habari,hivi huu uandishi wa habari umesomea wapi? Tusaidiane kama sijakosea nadhani kwa taaluma ww ni mwalimu,sasa ww mwenyewe unalalamika kuhusu tatizo la walimu,siurudi singida ukafanye kazi ya ualimu,uliyosomea pale mwanza,Chonde chonde maaskofu tupeni uhuru wetu mnaotaka kuupora kwa nguvu eti kwa kuwa nyie viongozi wetu,hatutaki kuamuliwa,tutaamua wenyewe muda ukifika tuacheni jamani,
 
Maaskofu, tuko pamoja. Ha2taki hiyo katiba ya chama cha mbogax2!
 
Huyu nae Asubiri atakapo ambiwa siyo raia wa tz
 
Ana haki kwa sababu katiba pia inagusa masuala ya kijamii kwa hiyo sio ya wanasiasa peke yao.
 
Ana haki kwa sababu katiba pia inagusa masuala ya kijamii kwa hiyo sio ya wanasiasa peke yao.

Tumevamiwa hapa JF wapo wahuni? Oh! Ninalazimika kukusaidia tabia yako isiendane na jina la ID yako maana Wataaluma wa Saikolojia wanayaita majina haya kuwa ni "Psychological name" Angalia jina hilo lisije likaharibu tabia yako nawe ukawa hivyo hivyo. Sasa soma Katiba Inaypoendekezwa upate uelewa mzuri kwa uelewa wa kulijenga taifa lako.
 
Askofu Niwemgizi wa jimbo Katoriki jimbo kuu Rulenge amesema ataongoza kampeni ya kura ya hapana kupinga katiba mpya.
Nchi yetu tanzania imepiga hatua kubwa katika mchakato huu wa katiba inayopendekezwa kwa kuwa kilichobaki ni kupiga kura ya maoni ili hatimaye tuwe na katiba mpya ambayo itakuwa msingi ma maendeleo ya taifa letu.Hoja yangu kwa leo ni kuhusu hii kauli kuwa askofu wa jimbo katoliki la rulenge mhashamu niwemugizi amesema atawahamasisha wakatoliki wapige kura ya hapana dhidi ya katiba inayopendekezwa,sasa najiuliza kuwa tangu lini askofu huyu kasajiliwa kama chama cha siasa,coz naona ameanza siasa ndani ya kanisa katoliki,hivi anadhani wakatoliki ni wajinga kiasi hicho?Lahasha wakatoliki tunao uelewa wa kutosha na siku ya kupiga kura tutaamua wenyewe na si kwa shinikizo la maaskofu au lakwako mhashamu niwemugizi,najiuliza pia kuwa hivi kanisa katoliki limeongeza kipengele cha siasa katika shughuli zake? Sina uhakika nikiwa mkatoliki naomba maaskofu mtufafanulie hili ili tujue moja kuwa kanisa letu limeingiliwa au limefanya mabadiliko?Kimsingi navyofahamu kadiri ya historia kanisa lilishajitoa katika shughuli za kisiasa na kubaki na jukumu la kuwahudumia waamini kiroho zaidi na kijamii,sasa hili jambo la kutuambia eti tufuate hayo mnayoyasema ili hali ajenda yenu ya siri kuhusu hiyo kauli ya niwemugizi hatuijui,hatutaki kuamuliwa mambo tumechoka,tunao uwezo wa kufanya maamuzi sahihi wakati ukushafika.Acheni kutaka kutumia madaraka yenu kutuletea mgawanyiko eti kwa kuwa nyie viongozi wetu,kwanza naomba mtambue kuwa hamna haki ya kuingilia utashi wa waumini wenu.Jukumu lenu ni kutuelimisha kuhusu katiba inayopendekezwa na sio kupangia kuwa tukapige kura ya hapana,kwanini? Hii ndio ajenda yenu basi hatutaki na ndio maana kwa busara askofu mkuu wa jimbo katoliki la dsm akasema maaskofu hawana haki ya kuwaamulia wananchi au waumini wao juu ya kupiga kura ya ndio au ya hapana.Sasa askofu wa rulenge tukueleweje? Siasa na wito wa ukasisi haviendani kabisa ama sijaelewa nyie viongozi wetu wa kiroho mnatupeleka wapi jamani,hivi huu ndio wito wakuhamasisha watu wakapige kura ya hapana badala ya kuwaelimisha ili mwisho wafanye uamuzi wenyewe,du hii haikubaliki,tuacheni tuamue wenyewe.Tumieni muda wenu kutatua changamoto zinazolikabili kanisa hapa nchini Nirudi kwa ndg yangu isango umekuwa mseminari mahiri sana,sote tunajua hakuna ubishi kuhsu hilo,mara umeingia kwenye uandishi wa habari sielewi umesomea wapi hii taaluma ,najua umesoma falsafa,teolojia na ualimu,wasiwasi wangu ni pale unapoacha taaluma yako na kuvamia taaluma nyingine.Nakushauri urudi nyumbani sngd ukafundishe achana kabisa na siasa hizi mbovu.
 
Duh hawa jamaaa wakatoliki huwa ni noma, wakiamua jambo huwa hawarudi nyuma.

If you sideline the church hakika ypu are heading towards failure, thats for sure.

go go askofu Niwemugizi, tuko sote sawa. Tupo na wewe hatua zote![/QUOTE

Lane Unasema wakimua jambo ni noma hawarudi nyuma mbona sikuelewi?wakiamua nini?kwaninwao ni Mungu wasipingwe, hatua ya kuwaamulia watu kufanya maamuzi unaona ni sawa? mie ningekubaliana na wewe kama askofu huyo angeanzsha kampeni ya kupinga maovu kwa waumini wake ningemuelewa,kampeni ya watu kuachadhambi wamjue Mungu wa Kweli hapo ningemuunga mkono hata kwa maandamano, lakini hili la kuipinga Katiba mimi silikubali na hiyo siyo kazi yake anachepuka.
 
Katiba iliyopendekeza itapita hata kama watanzania wote watapiga kura ya hapana. Anayehesabu kura ndo anapitisha katiba. Hata hivyo wasioitaka lazima wapewe nafasi ya kusikilizwa na kutumia haki yao. Siku zijazo, serikali yetu itakuwa imejifunza madhara ya usanii ktk mambo ya msingi.
 
Askofu Niwemgizi wa jimbo Katoriki jimbo kuu Rulenge amesema ataongoza kampeni ya kura ya hapana kupinga katiba mpya.
Tanzania ni zaidi ya huyo askofu wa rulenge,kama ametumwa ss hatumuungi mkono hata kidogo,tutaamua wenyewe wakati wa kupiga kura,yeye akajipange kuimarisha uchungaji wa kondooo humo jimboni mwake,hatutaki tumechoka kuendeshwa na hawa viongozi wetu wa dinnika,asante
 
Hata kule Rwanda ni maaskofu ndio waliochochea mauaji ya kimbari

Pamoja na miaka yangu zaidi ya mitano niliyokaa Ngara sikuwa na habari kwamba hata Rulenge kulikuwa na mauaji ya kimbali, labda nifahamishwe vinginevyo
 
Pamoja na miaka yangu zaidi ya mitano niliyokaa Ngara sikuwa na habari kwamba hata Rulenge kulikuwa na mauaji ya kimbali, labda nifahamishwe vinginevyo

Ni vizuri kusema ila ni vigumu kuyaishi. Hayo Emmamkolomi unayoyasema hata najisikianvibaya kuyatamka tusiombe yatokee kwetu Tanzania maana hatutakuwa na wa kumlaumu zaidi yetu wenyewe. Kwanza Tanzania hakujatokea mauaji ya kimbari. Ee Mungu utuepushe na maneno hayo maana amani ya nchi yetu ipo kwa Watanzania wenyewe. Naamini tutailinda na kuitetea daima kwa misingi imara ya katiba yetu
 
Back
Top Bottom