Askofu Niwe Mugizi jimbo Katoliki Rulenge Ngara Kagera, kuongoza kampeni ya kupinga katiba mpya

Mpeni Kaisari yaliyo ya kaisari, na mpeni Mungu yaliyo yake Mungu!! Ni nani anasema Maaskofu na Viongozi wa dini hawapaswi kuhamasisha watu kukataa katiba mpya?? Kama ni ya kibaguzi na imetokana na kundi la manyang'au waendelee kukaa kimya?? Naona kuna watu kama Chabruma mmeamua kujitoa fahama na kutetea ujinga!
 
lazma tujiandae kuingia mitaani kuwapa elimu wananchi kuipigia kura ya HAPANA rasimu ya ccm huu upuuzi ccm hauvumiliki tena
 
Askofu Niwemgizi wa jimbo Katoriki jimbo kuu Rulenge amesema ataongoza kampeni ya kura ya hapana kupinga katiba mpya.

Mimi ni mwislam ila napenda sana misimamo ya maaskofu ambayo haina unafiki na uoga wa mashehe! Tatizo mashehe wetu hawajasoma elimu inayoitwa ya dunia ndo chanzo cha uoga ila wangekuwa wasomi hakikawangekuwa waelewa na wasio na uoga wa kusugudia ccm. Tuko pamoja maaskofu
 
Mimi sijaelewa, hivi ASKOFU ndiyo ana ufahamu wa waumini mpaka awahamasishe waikatae Katiba? waumini wenyewe hawawezi kuisoma Katiba na kutambua kama inafaa kupigiwa kura ya ndiyo au hapana?
 

Ungekuwa muslamu sidhani kama ungewakosoa Mashehe wako kuwa hawana elimu, wewe muslamu kanjanja.
 
Kwa akili zako unadhani viongozi wa Kikristo ni miburura kama unavyotaka kuamini!. Kwa nini usiuoe ukweli kwamba akili ya mtu binafsi anayetumia kichwa kufikiria, inatosha kuuambia moyo katiba hii pandikizi ni ya kinyang'au bila kushawishiwa?

Hivi wewe kama ni binadamu wa kawaida, unataka kuniambia dhamira yako haikuonyeshi matatizo makubwa yaliyokwenye hiyo rasimu ya ccm?

Unafiki na ubinafsi usiofikiria kesho hata ya watoto wako, ni ufu!.


Kinachokera ni kuona viongozi hao wa kiroho wakitoa matamko baada ya kushinikizwa na mtu anayeutamani urais kwa udi na uvumba
 
Askofu Niwemgizi wa jimbo Katoriki jimbo kuu Rulenge amesema ataongoza kampeni ya kura ya hapana kupinga katiba mpya.

Niko mbele yako Askofu. Aluta continua..........................
 

Kiswahili cha kikenya kama sikosei,tuacheni tupumuwe jamani
 
Kumbe Chabruma ndiyo Paul Makonda? Ila pampja na yote nimefurahi kuona katika hili la katiba Wakristo na Waislamu walio wengi wameungana katika kuip[inga. Iko siku kina Makonda/Sitta tut`wafukuza makanisani
 
Mimi sijaelewa, hivi ASKOFU ndiyo ana ufahamu wa waumini mpaka awahamasishe waikatae Katiba? waumini wenyewe hawawezi kuisoma Katiba na kutambua kama inafaa kupigiwa kura ya ndiyo au hapana?

Mbona huhoji wanapofungua biblia na kuwasomea kisha kutafsri, wewe unadhani waumini hawawezi kusoma na kuelewa? Ni hivi jamani hiyo rasimu mliyopitisha kimabavu na kwa kutumia mtutu wa bunduki haikubaliki. Sio na hao maaskofu tu na wananchi walio wengi, hata hao mabalozi wa nchi mnazokimbilia wawape misaada nao wanaona mnachezea amani ya nchi kisha mtake maombi ya kinafiki ya amani na misaada toka kwao baada ya vita. Kwani shida iko wapi, kama watu wengi hawaridhiki ina maana hilo suala lisitishwe tuingie kwenye uchaguzi huru baada ya hapo tuanze upya na mchakato huu kwa kufuata sheria. Hebu jiulize, maoni ya wananchi yalikusanywa bila mtutu wa bunduki, Tume ya Jaji Warioba ikakabidhi rasimu bila mtutu wa bunduki, iweje hii yenu mpaka watu wanataka kuandamana kupinga, maaskofu, shura ya maimamu, na mabalozi wa kigeni wanaona haifai muendelee kulazimisha tena kwa mtutu wa bunduki!?
 
Kwahiyo Lowasa anapinga hii katiba pendekezwa?

Nashangaa hata mimi, sababu nilisikia kwa sikio langu Lowasa akipiga kura ya Ndio sasa sijui ni kwanini anahusishwa na wanaohamasisha kura za hapana, back to the topic Nawaunga mkono Maaskofu
 
Mimi sijaelewa, hivi ASKOFU ndiyo ana ufahamu wa waumini mpaka awahamasishe waikatae Katiba? waumini wenyewe hawawezi kuisoma Katiba na kutambua kama inafaa kupigiwa kura ya ndiyo au hapana?
Tutaisoma wote hadi kanisani tutaijadili na tutaweka msimamo wa hapana!! usitupangie!!
 
Askofu atangaza kufia katiba
• Ni Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki
• Aahidi kuhamasisha waumini waipigie kura ya hapana

NA JOSEPHAT ISANGO

WAKATI Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Alli Mohamed Shein, wakitarajiwa kukabidhiwa Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalumu la Katiba, Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) ambaye pia ni Askofu wa Jimbo la Rulenge- Ngara, Mhashamu Severini Niwe Mugizi,amewataka Watanzania waikatae, na kwamba yupo tayari kufa kwa ajili ya kupigania katiba bora.

Askofu Niwe Mugizi amesema haungi mkono Katiba iliyopendekezwa kwa kuwa haina ukweli wala uadilifu.
“Wao walibadili kanuni ili kupata yanayowapendeza. Mimi nawasihi kwa unyoofu, ingawa najua sasa suala la kudai katiba mpya ni kelele ambayo haitaisha, tuwe na upendo na nchi yetu na viongozi wetu, lakini pale wakifanya yasiyofaa tuwaambie ukweli bila woga. Niko tayari kufa kwa ajili ya kusema ukweli kwa sababu tumetangaziwa vita,” alisema.

Akizungumza na mamia ya waumini wa Kanisa hilo kwenye Kituo cha Hija cha Katoke Jimbo la Rulenge-Ngara majuzi, Askofu huyo alisema kwa kuwa katiba hiyo imepitishwa kwa mabavu na hila, yeye hawezi kuhamasisha waumini wake waiunge mkono.

Ameifananaisha katiba hiyo inayopendekezwa na nyumba iliyoezekwa kwa dhahabu lakini imejengwa kwenye msingi wa mchanga. “Haiwezi kudumu,” alisema.

Aliwaeleza kuwa alishamwambia hata Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kwamba iwapo katiba mpya haitazingatia mambo ya msingi yaliyopendekezwa na Watanzania atawahamasisha waumini kupiga kura ya hapana
“Naawambia kabisa, katiba ile ni wazi walipaswa kuboresha, na ndiyo ilikuwa kazi yao. Kweli kuna vitu wameboresha, kuna vitu wameongeza ongeza pale, lakini kuna vitu vya msingi sana wameviondoa. Mimi binafsi siafiki kabisa,” alisema.

Alisema kwa mfano, katiba inayopendekezwa haitoi uthibitisho wa kulinda uhai wa kuishi tangu kutungwa mimba bali inasema kila mtu ana haki ya kuishi.
“Siafiki siafiki hata kidogo. Watu walipendekeza vitu fulani viwepo kwenye katiba, mfano mgombea binafsi watakwambia wameweka kwenye katiba lakini ukiangalia masharti yaliyowekwa ni magumu kiasi kwamba mgombea binafsi hawezi kufaulu.

“Nasema, sitaki kurefusha, na wameshasikia hadi imefika mahali sisi maaskofu tukaitwa wapuuzi tuliofanya kazi isiyo na utukufu, lakini tuwaambie kuwa sisi hatukutumwa na wanasiasa kufanya kazi tunayofanya. Pale ambapo ukweli na uadilifu vinakosekana hatupaswi kukaa kimya. Mchakato wote wa katiba haukuwa na uadilifu na ukweli, ndiyo maana mimi siafiki,” alisema.

Askofu huyo aliwashauri waumini kupiga kura wakiwa na dhamiri hai, huku akiwatahadharisha watakaopiga kura za ndiyo halafu mambo yakakwama siku za usoni wasilaumu kuwa askofu hakuwaambia.
 

paulo makondakta ni njaa tu inayo mpeleka peleka, amekuja na riwaya za kutumwa na mtoto wa mkulu kuja kumchafu Mamvi (Edo) humu lakini Zimegonga mwamba , sasa ana kuna na Ngonjera za Kuwatusi Maaskofu.
 


Big up avae! you have said it all!
 


Wewe na genge lako bado mnaishi Tanzania ya mwaka arobaini na saba; waTanzania wa leo sio wale mliokuwa mnawatishia NYAU, wamejitambua na wanajua kuwa ccm ndio adui yao mkubwa anayebaka maendeleo ya nchi yao!! Hizo propaganda zenu za kuwatisha watu hazitafanikiwa. Mungu anawaongoza waTanzania na uharamia wenu utashindwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…