Askofu Niwemugizi amuomba Rais Samia asikubali kufananishwa na Mungu

Askofu Niwemugizi amuomba Rais Samia asikubali kufananishwa na Mungu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Ameyasema hayo leo katika Jubilee inayofanyika Mkoani Kagera, ambayo pia imehudhuriwa na Mh Rais

===

skofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kutokubali kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile.

Amesema hayo leo Jumanne Februari 22, 2022 katika sherehe za Jubilee ya miaka yake 25 inayofanyika wilayani Ngara mkoani Kagera.

“Nikikuombea uwe na afya njema na uwe mnyenyekevu lakini pamoja na madaraka hayo makubwa uliyonayo usikubali kamwe kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile usikubali."

"Ninakumbuka sana Hayati Benjamini Mkapa najua huko mlikuwa mmezoea mtukufu rais, mtukufu rais alifika mahali akawa mkali kabisa mtukufu ni Mungu tu naomba hilo liwe neno kwako, " amesema Askofu Niwemuguzi.

Huku akiwa makini amesisitiza,"basi nakuombea Mungu akusaidie kukuza upendo kati ya Watanzania unaotuongoza, ukuze haki nayo haki izae amani na utulivu na kukuza demokrasia katika nchi yetu."

“Ukuze upendo na mshikamo wa Watanzania ili hatimaye utumishi wako utukuke na kuacha alama itakayoonwa kwa vizazi vingi.
Mungu akujalie hekima na uvumilivu wa kusikiliza hata yale yanayokela masikio yako, unajua sisi watoto wako tuko wakorofi, Mungu akujalie tu hekima na uvumulivu hasa pale unapokuwa ni ushauri wenye nia njema ya kulijenga Taifa letu liendelee kuheshimika ndani na nje.”

PIA SOMA
- Rais Samia akataa kutukuzwa, asema yeye hawezi kujilinganisha na Mungu

- Askofu Niwemugizi: Rais Samia sikiliza maoni ya watu hata yale yasiyokufurahisha

CCM kwa tabia yao ya kupenda kujipendekeza kwa viongozi wao ili wapewe vyeo ndio huwa wanamuita Rais majina yote ya kumtukuza ili wakumbukwe kwenye ufalme wao.

Bahati mbaya Rais akiwa mpenda sifa ndio atavimba kwa hayo majina anayoitwa mwishowe yanageuka tabia, kila Rais ajaye atatafutiwa majina yote ya kumpamba, tunahitaji Katiba Mpya ituondolee huu utumwa wa kifikra uliotawala vijana wa chama tawala.
 
Hili lilisemwa sana wakati uliopita (previous regime)

Mtu akikufananisha na Mungu kimsingi anakuloga na ukikubali tu umeenda na maji na siku zako zinahesabika

Tahadhari pekee ni kutokubali kufananishwa na Mungu na kukataa kwa dhati sifa hizi za kijinga

Over!!!
 
Amina
 
Mi mtu akiniita aite tu.

Mimi mwenyewe nitachagua cha kufanya.
 
Hili lilisemwa sana wakati uliopita (previous regime)

Mtu akikufananisha na Mungu kimsingi anakuloga na ukikubali tu umeenda na maji na siku zako zinahesabika

Tahadhari pekee ni kutokubali kufananishwa na Mungu na kukataa kwa dhati sifa hizi za kijinga

Over!!!
We huoni kila akisafiri wakati wa kurudi anaandaliwa mapokezi fake ya kumtukuza
 
Hili lilisemwa sana wakati uliopita (previous regime)

Mtu akikufananisha na Mungu kimsingi anakuloga na ukikubali tu umeenda na maji na siku zako zinahesabika

Tahadhari pekee ni kutokubali kufananishwa na Mungu na kukataa kwa dhati sifa hizi za kijinga

Over!!!
Nyerere alitwa mtukufu rais mpk anang'atuka na hakuna lolote lililompata.

Ni unafiki wetu tu wanadamu tunaweza kutukuza kitu kwa mdomo lakini moyoni hakuna kitu.

Uzuri hilo neno liliisha ondolewa tangu awamu ya tatu.
 
too late...tayari anajiona goddess na wanaccm wanamuona hivyo
 
Nyerere alitwa mtukufu rais mpk anang'atuka na hakuna lolote lililompata.

Ni unafiki wetu tu wanadamu tunaweza kutukuza kitu kwa mdomo lakini moyoni hakuna kitu.

Uzuri hilo neno liliisha ondolewa tangu awamu ya tatu.
... kizazi cha lini wewe? Official salutation ya Nyerere ilikuwa Mwalimu or Ndugu or (rarely) Mheshimiwa na sio vingenevyo!
 
... kizazi cha lini wewe? Official salutation ya Nyerere ilikuwa Mwalimu or Ndugu or (rarely) Mheshimiwa na sio vingenevyo!
Safi sana hadi leo anaitwa mwalimu Nyerer e na wala siyo mtukufu Nyerere....kwangu mm japo ni kizazi cha sasa lakn Mwalimu Nyerere ni raisi pekee aliyekuwa anajishusha na wala hakuwa mjivuni na hata udhibitisho upo kwa kuangalia jinsi familia yake inavyoishi hata leo hii.
 
Back
Top Bottom