Askofu Niwemugizi amuomba Rais Samia asikubali kufananishwa na Mungu

Askofu Niwemugizi amuomba Rais Samia asikubali kufananishwa na Mungu

Askodu Niwemugizi ka fumble leo,angeachana na haya ya kuitwa Mungu angemkumbusha masuala ya ukosefu wa haki kwa watz.
Kesi ya Mbowe ni ya mchongo
Mbona kumkumbusha!
[emoji116][emoji116]
Nayo haki izae amani na utulivu"
 
Ameyasema hayo leo katika Jubilee inayofanyika Mkoani Kagera, ambayo pia imehudhuriwa na Mh Rais...

Askofu severine kachanganyikiwa yeye kwanza ajitambue asimuite yesu mungu. anajua yesu hataki kuitwa mungu na ndani ya biblia yesu kawaeleza wazi kuwa mungu yupo.

Lakini askofu bado anamwita binadamu mungu halafu leo anakuja kusema mbele ya mama samia usifananishwe na mungu. binadamu hawezi kuumba mbingu wala hawezi kulipeleka jua au kulizuia jua lisitoke mnaenda kumuita mungu askofu sahihisha kwanza hapo
 
Huyu askofu ni mnafiki balaa yani,kipindi magufuli yupo hai alikua kimya
Kwa nini kila anayekosoa sasa mnasema kipindi Cha Magufuli alikua kimya?
Hata hivyo huyo hajawahi kuwa kimya ndio maana baada ya kukosoa sana alihojiwa na uhamiaji wakataka kusema sio raia
 
Raisi SSH hawezi kukubali kutukuzwa kama yule mwingine, lakini tatizo ni 'chawa'
Macho yangu huenda yanaona tofauti, hata yeye anapenda kutukuzwa.
Angalia jinsi wateule wake wanavyomsalimia utaona. Wanafunga mikono huku wakiinama
 
Hili lilisemwa sana wakati uliopita (previous regime)

Mtu akikufananisha na Mungu kimsingi anakuloga na ukikubali tu umeenda na maji na siku zako zinahesabika

Tahadhari pekee ni kutokubali kufananishwa na Mungu na kukataa kwa dhati sifa hizi za kijinga

Over!!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nyerere alitwa mtukufu rais mpk anang'atuka na hakuna lolote lililompata.

Ni unafiki wetu tu wanadamu tunaweza kutukuza kitu kwa mdomo lakini moyoni hakuna kitu.

Uzuri hilo neno liliisha ondolewa tangu awamu ya tatu.
Acha uwongo, Nyerere hata kuitwa muheshimiwa hakupenda... Kipindi chake tulizoea neno ndugu... hata bungeni hakukuwa na hii mambo ya uheshimiwa...
 
... kizazi cha lini wewe? Official salutation ya Nyerere ilikuwa Mwalimu or Ndugu or (rarely) Mheshimiwa na sio vingenevyo!
Na baadae akawaambia watu kama hampendi kumuita ndugu basi wamuite mwalimu...
 
Nyerere alitwa mtukufu rais mpk anang'atuka na hakuna lolote lililompata.

Ni unafiki wetu tu wanadamu tunaweza kutukuza kitu kwa mdomo lakini moyoni hakuna kitu.

Uzuri hilo neno liliisha ondolewa tangu awamu ya tatu.
Nyerere hakuitwa mtukufu.
Enzi za Nyerere viongozi na watu wote walikuwa wanaitwa Ndugu.
Mtukufu na waheshimiwa mlianza kipindi cha Mkapa.
 
Askofu Severini Niwemugizi,wa Jimbo Katoliki la Rulenge -Ngara,Mkoani Kagera ambaye leo hii tarehe 22 Februali 2022, anafanya Sherehe za Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu (1997-2022), Sherehe zilizofanyika ktk Viwanja vya Posta,Ngara mjini na kuhudhuriwa na Maaskofu kutoka majimbo mbalimbali Katoliki ya Ndani na nje ya nchi,Mapadre, waumini na Viongozi wa Dini kutoka madhehebu mbalimbali,pia Viongozi wa Serikali.Ambapo Mgeni rasmi katika Sherehe hizo alikuwa ni Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakati wa kutoa neno la shukrani, Askofu Severini Niwemugizi amemwambia Mheshimiwa Rais kuwa asikubali kifananishwa na MUNGU,nanukuu, "Mheshimiwa Rais Nakuombea Afya njema, nakuomba hata siku moja usikubali mtu yeyote akufananishe na Mungu,nina mkumbuka Rais Mkapa aliwahi kukataa hata kuwa mkali kwa watu waliomuita Mtukufu Rais, akisema Mtukufu ni MUNGU tu, nakuomba na Wewe mheshimiwa Rais usikubali kufananishwa na MUNGU".

Aidha Mhashamu Severini amemuomba Rais Samia kuwa mvumilivu wa kusikiliza hata yale yanayokera masikioni mwake ili mradi Yana Nia njema ya kujenga nchi.
 
Jamaa anazidi kula mishale akiwa hukohuko kaburini kweli watu walichukizwa sana na mtu yule.
 
Hawa kundi la wanafiki wakiongozwa na huyu Samia ndo maana umemuona ameenda huko kwa wanafiki wenzake huyu mama wa kuhurumia tu!
JPM alikuwa anahudhuria matukio kama haya ya leo kila mara, sidhani kama uliwahi kumuita mnafiki.
 
Nyerere alitwa mtukufu rais mpk anang'atuka na hakuna lolote lililompata.

Ni unafiki wetu tu wanadamu tunaweza kutukuza kitu kwa mdomo lakini moyoni hakuna kitu.

Uzuri hilo neno liliisha ondolewa tangu awamu ya tatu.
Nakemea kwa ukale kabisa, uache uwongo, uache unafiki. Wewe ni mwongo mkubwa. Mwaliku Nyerere hakukubali kabisa kuitwa mtukufu wala hakukubali kuitwa mheshimiwa. Alikiwa akiitwa "Ndugu Rais".

Neno mtukukufu Rais na Mheshimiwa Mbunge, yalianza kutumika wakati wa Mwinyi.

Wakati wa Mwalimu Nyerere, tulikiwa tunashangaa sana, tulipokuwa tukiwasikia wakenya wakimwita Mori, Mtukufu Rais Moi, tulikuwa tukiona kuwa ni kufuru kubwa, kwa sababu tuliamini "mtukufu ni kwaajili ya Mungu pekee".
 
Huyu askofu ni mnafiki balaa yani,kipindi magufuli yupo hai alikua kimya
Kwanini usiendelee kufuatilia singeli mkuu. Yani hujui Jiwe alivyokuwa anamchukia Askofu Niwemugizi mpaka akaitwa sio raia uhamiaji wakamchunguza. Tanzania hii kuna maaskofu wawili walikuwa strong ni Askofu Niwemugizi na Askofu Bagonza, wote majirani ila makanisa tofauti
 
Ameyasema hayo leo katika Jubilee inayofanyika Mkoani Kagera, ambayo pia imehudhuriwa na Mh Rais

===

skofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kutokubali kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile.

Amesema hayo leo Jumanne Februari 22, 2022 katika sherehe za Jubilee ya miaka yake 25 inayofanyika wilayani Ngara mkoani Kagera.

“Nikikuombea uwe na afya njema na uwe mnyenyekevu lakini pamoja na madaraka hayo makubwa uliyonayo usikubali kamwe kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile usikubali."

"Ninakumbuka sana Hayati Benjamini Mkapa najua huko mlikuwa mmezoea mtukufu rais, mtukufu rais alifika mahali akawa mkali kabisa mtukufu ni Mungu tu naomba hilo liwe neno kwako, " amesema Askofu Niwemuguzi.

Huku akiwa makini amesisitiza,"basi nakuombea Mungu akusaidie kukuza upendo kati ya Watanzania unaotuongoza, ukuze haki nayo haki izae amani na utulivu na kukuza demokrasia katika nchi yetu."

“Ukuze upendo na mshikamo wa Watanzania ili hatimaye utumishi wako utukuke na kuacha alama itakayoonwa kwa vizazi vingi.
Mungu akujalie hekima na uvumilivu wa kusikiliza hata yale yanayokela masikio yako, unajua sisi watoto wako tuko wakorofi, Mungu akujalie tu hekima na uvumulivu hasa pale unapokuwa ni ushauri wenye nia njema ya kulijenga Taifa letu liendelee kuheshimika ndani na nje.”

View attachment 2127421
Hakika ✔️ na ukikubal tu huo ukuu mazee huchukui round refer.. kifo cha mfalme Herode!!!
 
Ilo neno lao tukufu sijui wanatumia kwajili gani, Tukufu wakati changamoto ni nyingi nchini kuliko mafanikio, bora hata nchi zilizokwisha endelea walitumie kidogo italeta maana #Not personal 😅 #one love Tz
 
Back
Top Bottom