Ameyasema hayo leo katika Jubilee inayofanyika Mkoani Kagera, ambayo pia imehudhuriwa na Mh Rais
===
skofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kutokubali kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile.
Amesema hayo leo Jumanne Februari 22, 2022 katika sherehe za Jubilee ya miaka yake 25 inayofanyika wilayani Ngara mkoani Kagera.
“Nikikuombea uwe na afya njema na uwe mnyenyekevu lakini pamoja na madaraka hayo makubwa uliyonayo usikubali kamwe kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile usikubali."
"Ninakumbuka sana Hayati Benjamini Mkapa najua huko mlikuwa mmezoea mtukufu rais, mtukufu rais alifika mahali akawa mkali kabisa mtukufu ni Mungu tu naomba hilo liwe neno kwako, " amesema Askofu Niwemuguzi.
Huku akiwa makini amesisitiza,"basi nakuombea Mungu akusaidie kukuza upendo kati ya Watanzania unaotuongoza, ukuze haki nayo haki izae amani na utulivu na kukuza demokrasia katika nchi yetu."
“Ukuze upendo na mshikamo wa Watanzania ili hatimaye utumishi wako utukuke na kuacha alama itakayoonwa kwa vizazi vingi.
Mungu akujalie hekima na uvumilivu wa kusikiliza hata yale yanayokela masikio yako, unajua sisi watoto wako tuko wakorofi, Mungu akujalie tu hekima na uvumulivu hasa pale unapokuwa ni ushauri wenye nia njema ya kulijenga Taifa letu liendelee kuheshimika ndani na nje.”
CCM kwa tabia yao ya kupenda kujipendekeza kwa viongozi wao ili wapewe vyeo ndio huwa wanamuita Rais majina yote ya kumtukuza ili wakumbukwe kwenye ufalme wao.
Bahati mbaya Rais akiwa mpenda sifa ndio atavimba kwa hayo majina anayoitwa mwishowe yanageuka tabia, kila Rais ajaye atatafutiwa majina yote ya kumpamba, tunahitaji Katiba Mpya ituondolee huu utumwa wa kifikra uliotawala vijana wa chama tawala.
CCM kwa tabia yao ya kupenda kujipendekeza kwa viongozi wao ili wapewe vyeo ndio huwa wanamuita Rais majina yote ya kumtukuza ili wakumbukwe kwenye ufalme wao...
hapa Tanzania ni vigumu ukiwa kiongozi ukatae misifa kwa sababu watu wengi wanafiki sana
hata Nyerere alisema kuna kipindi walimuingiza kingi, "Mwalimu ukistaafu nchi itabaki na nani ?"mwisho wa siku anasema aligundua walikuwa ni wachumia tumbo
Safi sana hadi leo anaitwa mwalimu Nyerer e na wala siyo mtukufu Nyerere....kwangu mm japo ni kizazi cha sasa lakn Mwalimu Nyerere ni raisi pekee aliyekuwa anajishusha na wala hakuwa mjivuni na hata udhibitisho upo kwa kuangalia jinsi familia yake inavyoishi hata leo hii.