Askofu Niwemugizi asikitishwa na Kauli ya Humphrey Polepole kuwafananisha Wapinzani na Corona

Angekuwa ashamtupia vilago tangu siku ametamka huu upuuzi
Remote,
Huyo Polepole anayafanya yote hayo kwa kumpendezesha bosi wao ambaye ni "sadist" mkubwa

Kama bosi wake hapendi siasa hizo za chuki, basi tutarajie akemee vikali

In God we Trust
 
Anadhania atadumu kwenye madaraka? Hata kama hatukuona sisi mabadiliko basi watoto wetu au wajukuu watalipa kisasi
Polepole amelewa madaraka!
"Nearly an old man can withstand adversity but if you want to test the man's character,give him power"!
Abraham Lincoln

In God we Trust
 
Kwahiyo nawewe unalipa kisasi?
Usiwe serious sana, kuna mwanachema mmoja humu alikuwa anaomba corona ije Tanzania..na bado alijetetea na lengo lake au mawazo yake ilikuwa CCM iathilike, kwa hiyo na huyu kuwafananisha CDM na corona hana tofauti na yule...au mm sijaelewa? Wote hawa wanafanya mzaha na Corona

In God we Trust
 
Elimu ndogo! Ukiona anayeamini viongozi wa dini ni kila kitu ujue ana matatizo kichwani, na hana sababu ya kusema amesoma.
Kipi walichoandika ambacho hakipo sahihi ewe maamuma!?
 
Nimesikitika sana kusoma maneno kwenye mtandao ambayo sijaamini yamesemwa kweli na mtu ambaye huko nyuma nilimheshimu sana, kwamba, tunaomba Mungu ugonjwa huu uondoke, Corona ni sawa na wapinzani nchini“.

Nikayakumbuka maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Anna Mgwira aliyosema jana kwenye salamu zake baada ya ibada ya kumsimika Askofu Ludovic Joseph Minde kuwa Askofu wa Moshi.

Alisema kwa kurudia rudia „tusaidieni (viongozi wa dini) kuwatengeneza watu wema wanaoheshimu utu wa watu na haki za watu“. Nimejiuliza hivi kweli hiyo ni siasa safi binadamu kumwona au kumuita mwenzake ni sawa na kirusi cha Corona?

Kumwona binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu ni tusi kubwa kwa Mungu mwenyewe kwamba Yeye Mungu naye ni sawa na kirusi cha Corona, kinachopaswa kuondoka!! Halafu unamwomba huyo Mungu aondoe Corona?!

Hapo ndipo tumefika Watanzania kweli!? Hiyo ndiyo sura ya, siasa ni uadui“. Mtu mnayetofautiana mtazamo au itikadi ni adui, ila kesho akibadili mtazamo akafuata wako anabadilika na kuwa lulu nzuri, rafiki, na binadamu kama wewe.

Jamani! Nawasihi Watanzania tujitahidi kupima maneno tunayozungumza hadharani kumhusu binadamu mwingine.

Mtakatifu Yakobo anasema „Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, anaweza kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu“ (Yak 3:2). Na tena, ulimi ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti“ (3:8).

Namshauri aliyesema Corona ni sawa na wapinzani katika nchi hii kama ni muungwana aombe radhi kwa kumdhalilisha Mungu aliyemuumba binadamu kwa sura na mfano wake (Mwa 1:26-27).

Kwa namna hiyo ataepusha mauti kwa heshima yake mwenyewe na na kwa siasa za kistaarabu.

Source: FB page yake

My take:
1. CCM kutokanusha kauli hii ni sawa na kubariki, ndio tuseme ni msimamo wa chama.
2. Tahadhari wasimtingishe tena askofu na zile saga za uraia na passport
CHAKUBANGA hapo ulipo vipi? Bado unafananisha CORONA na wapinzani?

kama NDIYO basi JIWE kakimbia WAPINZANI, aliposikia tu kuna cases za CORONA akajifanya anaenda kukagua daraja Ubungo then Morogoro na hapo baadae DODOMA na CHATO.
kajifungia na hatoki kabisa,
 
Pole pole akipata COVID-19 atangazwe hadharani

Nimesikitika sana kusoma maneno kwenye mtandao ambayo sijaamini yamesemwa kweli na mtu ambaye huko nyuma nilimheshimu sana, kwamba, tunaomba Mungu ugonjwa huu uondoke, Corona ni sawa na wapinzani nchini“.

Nikayakumbuka maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Anna Mgwira aliyosema jana kwenye salamu zake baada ya ibada ya kumsimika Askofu Ludovic Joseph Minde kuwa Askofu wa Moshi.

Alisema kwa kurudia rudia „tusaidieni (viongozi wa dini) kuwatengeneza watu wema wanaoheshimu utu wa watu na haki za watu“. Nimejiuliza hivi kweli hiyo ni siasa safi binadamu kumwona au kumuita mwenzake ni sawa na kirusi cha Corona?

Kumwona binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu ni tusi kubwa kwa Mungu mwenyewe kwamba Yeye Mungu naye ni sawa na kirusi cha Corona, kinachopaswa kuondoka!! Halafu unamwomba huyo Mungu aondoe Corona?!

Hapo ndipo tumefika Watanzania kweli!? Hiyo ndiyo sura ya, siasa ni uadui“. Mtu mnayetofautiana mtazamo au itikadi ni adui, ila kesho akibadili mtazamo akafuata wako anabadilika na kuwa lulu nzuri, rafiki, na binadamu kama wewe.

Jamani! Nawasihi Watanzania tujitahidi kupima maneno tunayozungumza hadharani kumhusu binadamu mwingine.

Mtakatifu Yakobo anasema „Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, anaweza kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu“ (Yak 3:2). Na tena, ulimi ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti“ (3:8).

Namshauri aliyesema Corona ni sawa na wapinzani katika nchi hii kama ni muungwana aombe radhi kwa kumdhalilisha Mungu aliyemuumba binadamu kwa sura na mfano wake (Mwa 1:26-27).

Kwa namna hiyo ataepusha mauti kwa heshima yake mwenyewe na na kwa siasa za kistaarabu.

Source: FB page yake

My take:
1. CCM kutokanusha kauli hii ni sawa na kubariki, ndio tuseme ni msimamo wa chama.
2. Tahadhari wasimtingishe tena askofu na zile saga za uraia na passport

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kumbe hiini habari ya zamani!! sikucheki date mwanzoni! i wasted my time!
 
Wacha weee!
Toka lini mtu mpumbavu akawa na hekima?
Huyu jamaa ni takataka,kwani kuwa mpinzani ni tatizo? Mbona hata ndani ya CCM kuna wapinzani...
Halafu akiongea anafikiri anaongea vitu vya maana kumbe ni ujinga mtupu...kwanza hana shule..
Personally siwezi kusikiliza nonsense..basically he has nothing upstairs..

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini aseme hovyo
... zamani mwezi mmoja uliopita?
jana tu ni zamani mkuu! au? ile lugha ya picha tu! yaani nadhani Slow2 kama kweli alisema maana ushahidi hamna hapa labda alimaanisha wapinzani kina DJ , Zana za Kilimo, European Mnyampaa na wengine ni mawakala wa mabeberu na ni hatari mno kwa ustawi wa taifa na ni wa kuogopa kama Corona nadhani ndo maana yake!
 
Acha kutetea ujinga
 
Back
Top Bottom