Kabende Msakila
JF-Expert Member
- Oct 7, 2020
- 1,809
- 1,692
Jfteam
Taifa tuna hazina kubwa ya watu wanaofaa kuwa washauri wa viongozi wakuu.
Katika taifa letu namlinganisha Askofu Niwemugizi wa Ngara - Tanzania na hayati Archbishop Desmond Tutu wa Africa ya Kusini. Ni watu wasiojua kula maneno, kujikomba wala kujipendekeza. Mara zote huongea hisia za jamii, hushauri kwa maslahi mapana ya jamii tofauti na wengine wanajiweka karibu ya viongozi ili wachonge mzinga.
Kutokana na hali hiyo nashauri mamlaka za nchi zisikie ushauri wake kwa heshima ya kufanyia kazi shauri zao zitakumbukwa na vizazi vijavyo. Mbele yetu kuna suala la katiba mpya, watu walioko mahabusu kwa hila, ufisadi kwa baadhi ya watendaji, tume huru ya uchaguzi, matumizi mabaya ya madaraka kwa baadhi ya watendaji, nk nk
Hivyo vyote vitampa heshima kubwa Rais SSH ikiwa atavitekeleza kwa watanzania. Watanzania tumezaliwa bila vyama vya siasa sasa Siasa haiwezekani ziligawe taifa. Mama wasikilize akina Niwemugizi utabarikiwa na nchi ulojaliwa kuitawala.
# SSH kazi iendelee
# Niwemugizi ushauri uendelee
# Watanzania tuwaombee viongozi wetu.
Msakila M Kabende
Kakonko / Bukoba