Niwemugizi Yuko biased na haki. Chawa Kama wewe unachojua ni kutetea chama chako tu kilichojaa dhulma.
Sent from my Infinix X657 using
JamiiForums mobile app
Eliasmisizo!
Kwanza mimi sio chawa bali binadamu,sidhani kama kuna chawa Duniani anayeweza kusoma na kuandika kama binadamu.
Halafu usidhani wote tunaoandika humu ni wahuni...la khasha!
[emoji419]Pia tunaandika baada ya kujiridhisha.
Angejua haki asingemfanyia yale aliyomtendea askofu Mwoleka (R.I.P)!
Aliyekuwa Muamzilishi wa Jimbo hilo la Rulenge na muanzilishi wa jumuia ndogondigo.
Aliyemlea yeye
Niwemugizi mpaka kufikia kuupata huo uaskofu?
Alimnyima mstaafu huyo huduma muhimu,ikiwemo hata kumnyima magazeti ya habari.Pia akapambana kuziua zile jumuia ndogondogo alizokuwa amezianzisha mzee, hapo awali na hatimae
Mzee wa watu akakimbilia Jimbo la Morogoro na kutunzwa huko.
Na baadae wajerumani wakaamua kumchukua mpaka ujerumani.
Walikomtunza mpaka mauti yanamkuta.
Na hata Askofu Mwoleka (R.I.P) kwa hasira aliwahi kutoa kauli kwamba akifariki asizikwe Rulenge.bali Morogoro au huko huko Ujerumani.
Ingawa alibatilisha uamuzi wake siku za mwisho karibu na mauti yake.
Baadae akaanza kudeal na mkwe wake Padre Privatus Karugendo (R.I.P)mpaka akamuondoa kwenye upadri,na Rulenge kwa ujumla.
Huyo
Niwemugizi hana haki yoyote anayoitetea zaidi ya kuichukia pale serikali ya JPM ilipozuia vifaa vya taasisi za kidini kuingia nchini bila kulipiwa Ushuru au Kodi.
Alikuwa amezoea kuingiza vitu free ikiwemo madawa na kisha kuyasogeza Burundi na kupiga hela.
Leo kamsifia SSH weee!
Akamalizia kwa kuomba free importation ya vifaa tiba na madawa,akidai kwamba wao hawatengenezi faida bali wanatoa huduma.
iIa SSH akamchomolea kidiplomasia.....
.....Kwamba sio taasisi yake pekee inayoomba hivyo,bali kuna taasisi nyingine nyingi za kidini nazo zimekwisha wasilisha maombi kama hayo....
....Hivyo awe na subira wakati
Serikali inafanya upembuzi na ufuatiliaji.
Ili kuona na kujiridhisha iwapo,vikiisha ingia vinatumikaje?....
Je!...ni kweli ni Non-profit kama alivyodai Niwemugizi leo?
Ukienda Pale Bugando kwa mfano,au hospitali na shule yoyote inayomilikiwa na taasisiza kidini,
Utakuta bei ya huduma ni ghali kama kwingine kote nchini.
Shule za Seminari zote nchini wazazi tunalipa ada kama kwingineko,pamoja na kwamba waumini kutoa baadhi ya sadaka kuchangia seminari kupitia makanisani.
Hivyo vifaa au madawa yakiishaingia mbona hatujawahi ona msaada wake kwenye jamii kwenye suala la upunguaji wa bei.[emoji626]