johnmashilatu
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 841
- 909
Askofu wa Jimbo katoliki la Rulenge-Ngara, mhashamu Severine Niwemugizi amesema ripiti ya hivi karibuni ya CAG imedhihirisha uongo wa watawala.
Katika salaam zake za Pasaka, Askofu Niwemugizi amesema waumini wajifunze kuwa wakweli na kuepuka uongo kama Yesu alivyokubali kufa msalabani kwa kutetea ukweli.
Amesema watanzania waliaminishwa kuwa rushwa ma ubadhirifu umekomeshwa lakini ripoti hii inaonyesha uongo wa watawala.
"Mabilioni ya fedha yamepigwa serikalini, vyama vya siasa... mpaka wanaume wamejifungua, uongo huu haukubaliki" amesema.
Amesema ukweli lazima usemwe ingawa una gharama zake, unaweza kukamatwa, kupewa kesi ya uhujumu uchumi ili usipate dhamana, lakini lazima tujifunze kuutafuta, kuusema na kuutetea.
Amesema kauli ya mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde juu ya hali mbaya ya maisha wananchi kutokana kupanda kwa mafuta ni ukweli wa hali ilivyo mitaani.