Askofu Niwemugizi: Ripoti ya CAG imedhihirisha uongo wa watawala

Si vizuri kumbishia na kumsema "mtumishi" wa Mungu. Lakini katika kukua kwangu na kushuhudia awamu za utawala hapa nchini mpaka hawamu hii ya "5" ama ya 6. Sijawahi kusikia kiongozi wa serikali yeyote anasema Rushwa nchini, hivyo PCCB ikomeshwe na Mahakama ya Mafisadi ifungwe. Sasa Askofu Niwemgizi aliambiwa na nani kuwa watanzania wameaminishwa Rushwa na ubadhirifu vimekomeshwa? Wakati awamu za hivi Karibuni Vita dhidi ya ufisadi na Rushwa imepamba Moto kwa PCCB kupewa nyenzo zikiwemo majengo na rasilimali watu na Mahakama ya Mafisadi imeanzishwa.

Watu wadini hatutaki kabisa kuwabishia wala kuwakosoa. Hatupendi Hata kidogo, vinginevyo labda mmenukuliwa vibaya.
JP alikuwa mwizi sana
 
Askofu niwemugizi ni askofu wangu huyu halembi huwa nimsema kweli nimesoma shule yake inatwa SAINT ALFRED RULENGE SECONDARY MIAKA HIYO namkubali sana katika speech zake.
 
Ripoti za hivi kila mwaka zinatoka hivi hatua gani huwa zinachukuliwa Sasa?dhidi ya mamlaka zilizosababisha huo ufujaji ,kila saaa tunasoma comment tu askofu,sijui she he sijui mwanasiasa kaiponda serikali kwa ufisadi,halafu je baada ya hapo Nini Tena mafisadi wanaendelea kufuga vitambi tuuuuuuuuuuu!!!!!!! Ovyoooooooooooooo
 
Ukweli sio kwa watawala tu bali ni kwa wanaadamu wote hata madhabahuni ufisadi na ubadhilifu wa pesa unafanyika chini ya mwamvuli wa uongo.
Ila Uongo wa Magufuli ulizidi hata Malaika wa Ibilisi
 
Ukweli sio kwa watawala tu bali ni kwa wanaadamu wote hata madhabahuni ufisadi na ubadhilifu wa pesa unafanyika chini ya mwamvuli wa uongo.
Tayar dawa imekuingia kisawasawa 😂😂😂 naona unaanza tafuta justification!!
 
Siamini kama wakati wa awamu yoyote kutakuwa hakuna wizi. Kinachotakiwa, ni wizi na wevi kuwekwa wazi na watu wawe huru kuuzungumza na kuujadili huo wizi.

Awamu ya 5, ilikuwa ya hovyo sana kwa kuwafunga midomo watu, na kuwaficha mafisadi kwa kuwadanganya watu kuwa kwenye Serikali ya awamu hiyo hakukuwa na wizi, kumbe, huenda ndiyo awamu iliyoongoza kwa ufisadi. Mpaka leo 2.5 trillion haieleweki zilienda wapi!
Kikubwa zaidi cha kuzingatiwa ni kwamba tulishuhudia jitihada kubwa kupitiliza ikifanyika kuzuia ofisini ya umma ambayo kikatiba dhamana yake ni kuhakiki matumizi sahihi ya rasilmali za nchi ikidhibitiwa ili isitekeleze wajibu wake huo. Kwa maneno mengine badala ya kushughulika na ufujaji wa kodi zetu, uongozi wa nchi ulijielekeza kutumia vibaya mamlaka yake kuzuia ufujaji wa rasilmali za nchi kuwekwa hadharani kama sheria inavyoelekeza. Maana yake hasa ni kwamba sehemu ya ufujaji huu ulioanikwa na CAG uliidhinishwa na wakuu wa serikali wenyewe. Wakuu hao hao sasa wamebaki tu kumtupia lawama zote mtu mmoja badala ya kukubali uwajibikaji wa pamoja na kukiri makosa kwanza na kuomba radhi.
 
Askofu wa Jimbo katoliki la Rulenge-Ngara, mhashamu Severine Niwemugizi amesema ripiti ya hivi karibuni ya CAG imedhihirisha uongo wa watawala.

Katika salaam zake za Pasaka, Askofu Niwemugizi amesema waumini wajifunze kuwa wakweli na kuepuka uongo kama Yesu alivyokubali kufa msalabani kwa kutetea ukweli.

Amesema watanzania waliaminishwa kuwa rushwa ma ubadhirifu umekomeshwa lakini ripoti hii inaonyesha uongo wa watawala.

"Mabilioni ya fedha yamepigwa serikalini, vyama vya siasa... mpaka wanaume wamejifungua, uongo huu haukubaliki" amesema.

Amesema ukweli lazima usemwe ingawa una gharama zake, unaweza kukamatwa, kupewa kesi ya uhujumu uchumi ili usipate dhamana, lakini lazima tujifunze kuutafuta, kuusema na kuutetea.

Amesema kauli ya mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde juu ya hali mbaya ya maisha wananchi kutokana kupanda kwa mafuta ni ukweli wa hali ilivyo mitaani.
Uj7mbe wa Pasaka unatoa CAG?
 
Wawajibike wote maana amefatiki mmoja ila wengine waliokuwa nae wapo WATUJIBU.
 
Tunamsubiri na chui jike anafikiri upigaji utaisha. Tutakaanga wote pasipo kutazama mafuta yamepanda bei au laah
Yule kuanzia mwaka kesho Ripoti za CAG zitachujwa maana zitakuwa zinaanza kukagua awamu ya 6, watu wanasherekea ya awamu ya 5 ambayo ni serikali ileile iliyopo Hadi Leo imebadilisha jina tu
 
Kwani umezuiwa kuusema ukweli wa madhabahuni?

Uovu upo wakati wote na sehemu zote.

Uhovyo wa awamu ya 5 ni uwongo wa kuwaaminisha watu kuwa hakukuwa na wizi na ufisadi wakati wa awamu ya 5. Na utawala ule kwa namna ulivyokuwa na uovu mkubwa, kwa hofu ya watu kuujua ukweli, uliamua kuua uhuru wa maoni na uhuru wa vyombo vya habari.
Hii ni ngumi ya pua.

Cc NAWATAFUNA
 
Askofu wa Jimbo katoliki la Rulenge-Ngara, mhashamu Severine Niwemugizi amesema ripiti ya hivi karibuni ya CAG imedhihirisha uongo wa watawala.

Katika salaam zake za Pasaka, Askofu Niwemugizi amesema waumini wajifunze kuwa wakweli na kuepuka uongo kama Yesu alivyokubali kufa msalabani kwa kutetea ukweli.

Amesema watanzania waliaminishwa kuwa rushwa ma ubadhirifu umekomeshwa lakini ripoti hii inaonyesha uongo wa watawala.

"Mabilioni ya fedha yamepigwa serikalini, vyama vya siasa... mpaka wanaume wamejifungua, uongo huu haukubaliki" amesema.

Amesema ukweli lazima usemwe ingawa una gharama zake, unaweza kukamatwa, kupewa kesi ya uhujumu uchumi ili usipate dhamana, lakini lazima tujifunze kuutafuta, kuusema na kuutetea.

Amesema kauli ya mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde juu ya hali mbaya ya maisha wananchi kutokana kupanda kwa mafuta ni ukweli wa hali ilivyo mitaani.
Maaskofu wamecharuka. Full kusagia watu kunguni
 
Back
Top Bottom