Askofu Niwemugizi: Ripoti ya CAG imedhihirisha uongo wa watawala

Askofu wa Jimbo katoliki la Rulenge-Ngara, mhashamu Severine Niwemugizi amesema ripiti ya hivi karibuni ya CAG imedhihirisha uongo wa watawala.

Katika salaam zake za Pasaka, Askofu Niwemugizi amesema waumini wajifunze kuwa wakweli na kuepuka uongo kama Yesu alivyokubali kufa msalabani kwa kutetea ukweli.

Amesema watanzania waliaminishwa kuwa rushwa ma ubadhirifu umekomeshwa lakini ripoti hii inaonyesha uongo wa watawala.

"Mabilioni ya fedha yamepigwa serikalini, vyama vya siasa... mpaka wanaume wamejifungua, uongo huu haukubaliki" amesema.

Amesema ukweli lazima usemwe ingawa una gharama zake, unaweza kukamatwa, kupewa kesi ya uhujumu uchumi ili usipate dhamana, lakini lazima tujifunze kuutafuta, kuusema na kuutetea.

Amesema kauli ya mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde juu ya hali mbaya ya maisha wananchi kutokana kupanda kwa mafuta ni ukweli wa hali ilivyo mitaani.
Ok
 
JPM alikuwa mwizi wa kimataifa
 
Ni kweli, ila uzi huu ni kuhusu uongo wa dhalimu.
Hakuna cha dhalimu ww sema umelipwa tu na hii ni Ajira yako,kiongozi wa nchi Kesha lala lkn kila kukicha ni matusi Hili Lina baraka na mkono wa watawala wa sasa bila hivyo lisingewezekana, mwambieni boss wenu, marehemu hajitetei.
 
Hakuna hata mwaka mmja ripoti ya CAG uliwahi kuwa na ahueni..

Uozo ulifikia kilele ule mwaka Mwendazake akamtimua Assad 😂😂😂..

Alivyomteua Kichere akatoa ripoti ya kwanza wapigaji wa awamu ya 5 wakaanza kusema eti Mwendazake anachafuliwa 😬😬
 
Hakuna cha dhalimu ww sema umelipwa tu na hii ni Ajira yako,kiongozi wa nchi Kesha lala lkn kila kukicha ni matusi Hili Lina baraka na mkono wa watawala wa sasa bila hivyo lisingewezekana, mwambieni boss wenu, marehemu hajitetei.
Yule ni mwizi sana, anakaribia rekodi ya Sani Abacha na Mobutu Sese seko kuku ngbendu wa zabanga
 
Wewe watu walipiga hata enzi za mwalimu na kuua mashirika ya umma itakua leo?, Askofu awe mkweli, ubadhilifu haukianza enzi za jpm,,,
Watanzania wengi ni wezi,,
Mawe yanarushwa Sana kwa Magu kwa sababu alijifanya kuwa kwake hakukuwa na ufisadi na wapambe wake kama wewe mlikuwa mnapokea na kutuaminisha kuwa awamu ya tano hakukuwa na ufisadi,

Na baya zaidi yeyote aliyejaribu kuusema ufisadi alinyamazishwa kwa madhara makubwa.
 
Amesema watanzania waliaminishwa kuwa rushwa ma ubadhirifu umekomeshwa lakini ripoti hii inaonyesha uongo wa watawala.
Si vizuri kumbishia na kumsema "mtumishi" wa Mungu. Lakini katika kukua kwangu na kushuhudia awamu za utawala hapa nchini mpaka hawamu hii ya "5" ama ya 6. Sijawahi kusikia kiongozi wa serikali yeyote anasema Rushwa nchini, hivyo PCCB ikomeshwe na Mahakama ya Mafisadi ifungwe. Sasa Askofu Niwemgizi aliambiwa na nani kuwa watanzania wameaminishwa Rushwa na ubadhirifu vimekomeshwa? Wakati awamu za hivi Karibuni Vita dhidi ya ufisadi na Rushwa imepamba Moto kwa PCCB kupewa nyenzo zikiwemo majengo na rasilimali watu na Mahakama ya Mafisadi imeanzishwa.

Watu wadini hatutaki kabisa kuwabishia wala kuwakosoa. Hatupendi Hata kidogo, vinginevyo labda mmenukuliwa vibaya.
 
Uanaweza kuuficha, kufunika na kuukwepa ukweli kwa mda tu ila katika mda muafaka utadhihirika. Bila kuiondoa CCM madarakani nchi itabaki masikini maana wezi wanapokezana uongozi na wizi
Sawa kabisa. Hususan ni kuiondoa CCM na kubomoa kabisa mfumo wake wa ulaghai wa chama dola. Kisha hapo hapo kurejesha nguvu ya wananchi kuchagua na kuwajibisha viongozi wao kupitia chaguzi makini na mihimili huru ya kidemokrasia.

Katiba mpya haikwepeki.
 
Wapi Magufuli alisema hakuna wizi?

Wizi ulikuwepo ila alipambana nao, na aliupunguza sana.

Ni Magufuli ndio alisema hata CCM kuna wezi na mafisadi wamejaa, na ndio maana alipambana nao.
 
Hakuna cha dhalimu ww sema umelipwa tu na hii ni Ajira yako,kiongozi wa nchi Kesha lala lkn kila kukicha ni matusi Hili Lina baraka na mkono wa watawala wa sasa bila hivyo lisingewezekana, mwambieni boss wenu, marehemu hajitetei.

Alipokuwa hai alizuia haki ya watu kumsema, akawa anatumia kundi lake la watu wasiojulikana, sasa acha watu waendelee kumpa za moto akiwa huko huko ahera madukani.
 
Kama tunataka kuwa wa kweli, basi lazima tuseme ukweli.
RAIS ALIYEKO MADARAKANI PAMOJA NA MAKAMU WA RAIS HAWANA BUDI WAJIUZURU, kwani haya Madudu yanayoripotiwa na CAG walikuwa sehemu ya JPM. Watu wanapepesa macho sana namna ya kuwafanya watawala wetu wawajibike kwa makosa yao.
Hali ilivyo sasa ni kama kutaka kumwonyesha JPM ndiye aliyesababisha upotevu huu wa mali za taifa. Sipo kabisa upande wa hayati JPM, ila lazima viongozi wetu wajitadhimini na yaliyotokea katika kipindi ripoti hii ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG)
 
Back
Top Bottom