Askofu Nyaisonga avishangaa Vyama vya Upinzani kususia uchaguzi. Ahimiza waumini kujitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi

Askofu Nyaisonga avishangaa Vyama vya Upinzani kususia uchaguzi. Ahimiza waumini kujitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi

Kumbuka Askofu Ruwaichi alitumiwa ndege kumchumkua huko KCMC Hospital na kumleta hapa Dar kupata matibabu kwa maelekezo ya rais. Katika mazingira hayo unategemea kanisa la Roma liwe upande wa haki au la wanaowalinda viongozi wake?
Umegonga penyewe Mkuu,kumbe!!!fadhira hizi zimeua msimamo wa kanisa baadhi ya maaskofu wanamambo ya ajabu sana.
 
Na ninarudia tena, chini ya uongozi wa sasa wa TEC, msitegemee kauli yoyote ile kutoka TEC itakayokuwa kinyume na matakwa ya watawala. Kanisa, kama lilivyo bunge na mahakama, wamejumuishwa. Mark my words.
Hakika nilikusoma vyema katika ile mada.
Lakini sasa inanibidi nianze kujiuliza, na kuwasihi nanyi wenzangu kukuna vichwa juu ya "ushawishi/nguvu" za huyu mtu mmoja anayeteka kila kitu.

Tunaelewa wazi hana uwezo wa kujenga mifumo ya kumsaidia aeneze mawazo yake kwa wengine, ila yeye njia yake kuu ni 'nguvu/mabavu.'

Kwa kutumia njia hii ameweza kuteka kila kitu - mihimili yote, Bunge na Mahakama. Kwa njia hiyo hiyo ameweza kuteka dini zote?; ingawaje mtu anaweza akasema njia hizo hazijatumika BAKWATA. Wao walichopewa na kuridhika nacho ni 'rushwa' ya kujengewa nyumba ya ibada. Alipofanya hivyo akawaziba midomo.

Amejaribu kutumia njia hizo hizo hata kwa raia.
Wasiokubaliana naye, kama vyama vya upinzani, suluhu ni mabavu. Upande wa wananchi, amefanya kila kitu aonekane anawajali wananchi zaidi - miradi mikubwa na hata rushwa za kugawa manoti mitaani.

Zaidi ya hapo, hajajenga chochote cha kuimarisha anayoyasimamia. CCM yenyewe ipo tu sasa hivi kama chombo chake cha kukitumia wakati wowote apendavyo yeye.

Kwa hiyo, yote haya yanafanyika kwa sababu anvyo vyombo vya kulazimisha watu wafuate anavyopenda yeye. Bila hivi vifaa, hana msingi wowote wa kumweka alipo.
 
Huyo askofu kweli ana akili timamu??

Hivi chama chako kinaenguliwa wagombea wako zaidi ya asilimia 95 na wapinzani wako CCM wagombea wake wote asilimia 100 wanaonekana kuwa ndiyo waliojaza sahihi hizo fomu!

Hivi huyo askofu anakuwa na ujasiri kweli wa kuvilaumu vyama vya upinzani kwa kususia huo UCHAFUZI??

Hakika katika awamu hii ya utawala, hata hao wanaojiita watumishi wa Mungu wamewekwa mfukoni!
Ni mwendelezo wa akili za yule Aliewahi kuvimbiwa maharage hadi anastaafu yeye ni kusifu serikali tu.
 
Viongozi wa Kanisa Katoliki wanastahili kupewa funzo wasiloweza kulisahau. Hii ni fursa ya pekee kwa waumini kutoa funzo hili mhimu sana.
1. Hakuna kutoa sadaka
2. Weka maoni kwenye sanduku la maoni

Sikutegemea kabisa kumwona Pengo mwingine mapema kiasi hiki baada ya kustaafu.
 
Niliwahi kueleza hapa jukwaani taarifa kutoka kwa Askofu mmoja kutoka inner circle ya Kanisa Katoliki. Mimi pia ni mkatoliki halisi wa imani aliyewahi kuhudumu ndani ya kanisa.

Askofu yile alieleza kuwa Kanisa Katoliki, baada ya waraka wa kwaresma, ulioeleza mapungufu mengi ya watawala wa awamu hii, uhusiano wake na mtawala mkuu ulififia sana kufikia hatua ya kujenga uadui. Inner circle ya Kanisa waliazimia kuurudisha uhusiano huo uliokuwa umezoeleka.

Hatua ya kwanza ilikuwa kumpata Rais wa TEC ambaye ana mahusiano binafsi ya karibu na mtawala, na huyo hakuwa mwingine bali huyu Rais wa TEC wa sasa. Hilo lilifanikiwa.

Na ninarudia tena, chini ya uongozi wa sasa wa TEC, msitegemee kauli yoyote ile kutoka TEC itakayokuwa kinyume na matakwa ya watawala. Kanisa, kama lilivyo bunge na mahakama, wamejumuishwa. Mark my words.

Mimi niliyasikia haya wakati wa kipindi cha kumpata Rais mpya wa TEC. Jambo la kujiuliza, hivi hizi dini zetu zipo kwaajili ya imani au maslahi fulani? Ni dini au watu fulani ndio wanaozifanya dini kuwa syndicate ya matakwa binafsi ya watu fulani?
Tutawasikiliza maaskofu wetu akina Kilaini hao ndo watu wenye hekima siyo hawa akina mapengo. Tumsifu Yesu Kristu na tukeshe tukiomba kwani muda haupo nasi. Lotote laweza tokea.
 
Viongozi wa Kanisa Katoliki wanastahili kupewa funzo wasiloweza kulisahau. Hii ni fursa ya pekee kwa waumini kutoa funzo hili mhimu sana.
1. Hakuna kutoa sadaka
2. Weka maoni kwenye sanduku la maoni

Sikutegemea kabisa kumwona Pengo mwingine mapema kiasi hiki baada ya kustaafu.
Hawa ndo walinifanya niache kwenda kanisani nasali kwenye radio Kwizera basi. Hopeless kabisa walamba miguu.
 
" hawa wenzetu mbona" ndio kauli inayotumika awamu hii.

Magufuli angekuwa "Ustadhi" tungesikia matamko kila kona ya nchi.

Sisi Wakatoliki wakati mwingine ni Wanafiki tu.

Hongereni KKKT na Moravian Sauti zenu tunazisikia.
Hakuna Chama chochote kikubwa Cha upinzani kinachoongozwa na mkatoliki Wala muislamu wa Bakwata
Vyama vya upinzani vimejaa Protestants na Waislamu wa siasa Kali wasiopenda Bakwata
 
Nijuavyo mimi:

• Kanisa Katoliki huwa halifanyi mambo ili kumfurahisha mtu au kikundi cha watu.

• Kanisa Katoliki huwa halifanyi mambo kwa kufuata mkumbo wa watu.

• Kanisa Katoliki halifungamani na chama chochote cha siasa.

• Kanisa Katoliki halifanyi mambo ili kuongezea tatizo zaidi, bali huangalia namna nzuri ya kuleta umoja na mshikamano.

• Kanisa Katoliki halijawahi kuwa la kidemokrasia hata siku moja. Sikumbuki kama nilishalishuhudia au hata kusoma sehemu juu ya hili.

• Kanisa Katoliki hufanya mambo yake likizingatia misingi ya Ukristu likiamini hakuna mwanadamu mkamilifu.

Ninajaribu kujiuliza:

• Kuna sababu gani ya msingi ya kulifanya Kanisa Katoliki liunge mkono ususiaji wa uchaguzi?

• Sisi Watanzania, tukisusia uchaguzi, then what will be our next plan? What will we benefit from doing so? Will that change anything?

• Je, kususia uchaguzi ndio suluhusho pekee lililopo? Ndio CCM wata-retreat? Ndio kusema kuwa wataacha uonevu?

• Je, tukisusia uchaguzi, tutaleta umoja na mshikamano kama taifa, au ndio tutazidi kugawanyika?

Ninafikiri tunapaswa kutafuta suluhisho jingine. Hatuwezi kususia tu bila kuwa na reasonable plan nyingine.

Kanisa Katoliki lipo sahihi, kwa mtazamo wangu.
Fuatilia historia. Uliyoyaandika ni nadharia na siyo uhalisia.

Kanisa Katoliki limewahi kufanya mambo mengi ya hovyo. Limewahi hata kusababisha mauaji makubwa, acha haya ya karibuni ya Rwanda. Mimi ni mkatoliki hasa na nitaendelea kuwa mkatoliki lakini najua kuwa ndani ya Kanisa kuna watu wanapenyeza mambo yao binafsi ili kutimiza malengo yao. Ndani ya Kanisa Katoliki, kwa miaka mingi, wamekuwemo pia majasusi wa kitaifa na kimataifa - hawa hawana imani yoyote ya Kanisa Katoliki lakini wanalitumia Kanisa kutekeleza dhamira zao.

Ikumbukwe pia Askofu huyu amechaguliwa kuwa Rais wa TEC kwa sifa moja kubwa - uswahiba wake na mtawala.
 
Kanisa katoriki kama ambavyo linapotosha watu wake kwa maungamo ya kila wiki, litaungama katika hili pia,kama kawaida yake.
 
Viongozi wa Kanisa Katoliki wanastahili kupewa funzo wasiloweza kulisahau. Hii ni fursa ya pekee kwa waumini kutoa funzo hili mhimu sana.
1. Hakuna kutoa sadaka
2. Weka maoni kwenye sanduku la maoni

Sikutegemea kabisa kumwona Pengo mwingine mapema kiasi hiki baada ya kustaafu.
Mkuu Mimi na familia yangu yote tumelihama kanisa kwasababu limekuwa compromised na ibilisi
 
Anaempinga askofu huyo atakuwa ana mapepo si bule. Mi naamini kabisa askofu kaongozwa na roho mtakatifu kuwahubiria watu kweli, kabla ya kumshambulia hebu tujitafakari wapinzani wapi tumejikwaa. Ikifikia hatua tunawapinga viongozi watakatifu hiyo ni dalili ya laana
 
Mkuu Mimi na familia yangu yote tumelihama kanisa kwasababu limekuwa compromised na ibilisi
Kuhama sio suluhisho mwana hata huko alikohamia ibilisi ana visa ya kuingia huko na utakuta na stakupokea akionekana kama malaika wa nuru
 
Back
Top Bottom