Niliwahi kueleza hapa jukwaani taarifa kutoka kwa Askofu mmoja kutoka inner circle ya Kanisa Katoliki. Mimi pia ni mkatoliki halisi wa imani aliyewahi kuhudumu ndani ya kanisa.
Askofu yile alieleza kuwa Kanisa Katoliki, baada ya waraka wa kwaresma, ulioeleza mapungufu mengi ya watawala wa awamu hii, uhusiano wake na mtawala mkuu ulififia sana kufikia hatua ya kujenga uadui. Inner circle ya Kanisa waliazimia kuurudisha uhusiano huo uliokuwa umezoeleka.
Hatua ya kwanza ilikuwa kumpata Rais wa TEC ambaye ana mahusiano binafsi ya karibu na mtawala, na huyo hakuwa mwingine bali huyu Rais wa TEC wa sasa. Hilo lilifanikiwa.
Na ninarudia tena, chini ya uongozi wa sasa wa TEC, msitegemee kauli yoyote ile kutoka TEC itakayokuwa kinyume na matakwa ya watawala. Kanisa, kama lilivyo bunge na mahakama, wamejumuishwa. Mark my words.
Mimi niliyasikia haya wakati wa kipindi cha kumpata Rais mpya wa TEC. Jambo la kujiuliza, hivi hizi dini zetu zipo kwaajili ya imani au maslahi fulani? Ni dini au watu fulani ndio wanaozifanya dini kuwa syndicate ya matakwa binafsi ya watu fulani?