MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Wakuu,
Askofu mkuu Jimbo Katoliki la Dar es Salaam anaongea na waandishi wa habari juu ya Pugu Marathoni lakini pia amegusia swala la maadili ya jamii. Amesema amefurahishwa na kauli dhabiti ya Rais Ruto wa Kenya juu ya kulinda maadili ya nchi hiyo na kupinga hadharani mambo ya ushoga.
Lakini pia Askofu Ruwaichi amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alitoa kauli dhabiti juu ya maadili lakini kiongozi mwenzake wa serikali akasema hiyo si kauli ya serikali! Ameuliza hapo kauli ya serikali ni ipi?
My take; Kwa nguvu na kasi ya msukumo juu ya ushoga unaoendelea duniani bila sisi kuchora mstari wa wazi na jamii ya kimataifa kuelewa msimamo wetu huko mbele tutapata shida kubwa hizo haki zitapoanza kudaiwa na watu potential bila woga hapa kwetu.
Mama yetu Mh Rais Samia pia aligusia umuhimu wa kulinda maadili yetu na kwa msimamo wake na dini yake nafahamu hawezi kuyumba kwenye hili na mfano mzuri ni serikali kupiga marufuku vitabu vya shule vinavyochochea hayo.
Nchi za wenzetu haya mambo yalianza kama mchezo na pengine hakuna aliyeamini itafikia hatua ya kuhalalishwa kisheria na hata kufundishwa mashuleni! Sasa tusisubiri tufike huko maana kijamii tunaanza kuzoeshwa tuone kawaida! Tunaona watangazaji maarufu, mastaa na hata shughuli mbalimbali za burudani jamii ya mashoga wanajitokeza wazi bila woga.
Tusipoziba ufa tutajenga ukuta! Tuanze kuchukua hatua sasa, tusifanye mzaha na maadili ya msingi yanayolinda utu wetu.
Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app