Askofu Shoo asisitiza NEC kusimamia uchaguzi huru, wa haki na wenye ukweli

Askofu Shoo asisitiza NEC kusimamia uchaguzi huru, wa haki na wenye ukweli

Askofu Mkuu Ruwaichi hakugusia kabisa siasa. Ameongea mambo yake na uhalisia wa maisha yetu. Umuhimu wa viongozi wa kidini ni kutusaidia waamini tuwe wema kwa kutumiza wajibu wetu kwa Mwenyezi Mungu na wenzetu. Haya ya kuleta kiongozi wa dhehebu langu au dini yangu ni mambo ya wanadamu wanaovaa majoho ya viongozi wa dini.
Askofu Ruwaichi leo ametukumbusha kwamba waisraeli walikuwa Taifa teule la Mwenyezi Mungu. Lakini ndio walimlazimisha Pilato, mrumi, amsulibishe Yesu, tena kwa kujitoa mhanga kwamba damu yake ni juu yao na watoto wao.
Yangu macho
Sasa nan hapa n mnafiki sababu kuna mmoja anayepamba pamba na mwingine anayetoboa na kupasua miamba [emoji57][emoji57]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watumishi wa Mungu hatupaswi kuwa waoga, tupo pamoja baba askofu tutasema kweli daima kwamba tume huru ya uchaguzi inahitajika sana TZ
 
Tatizo kubwa ni 'mfumo wa corruption', vinginevyo Bunge, Mahakama na Polisi wasingeulinda mfumo huu na TAKUKURU ingefanya kazi yake na muundo wa Tume ungebadilishwa. Na ndiyo maana huwezi kusikia TAKUKURU ikiiingilia mfumo wa Tume au mahakama na polisi.
Vyombo vyote hivyo ni sehemu au viungo, 'tentacles' za system.

Ukiangalia kwa undani sana utona kwamba hata JPM inawezekana alijaribu kuubadili mfumo huu akashindwa. Ndiyo maana awali alikuwa anasema tumuombee lakini sasa huenda bila kupenda amelazimishwa kufuata mstari.

Rais Obama wa USA alisema African needs "strong institutions" and not strong leaders.

Badala take sisi tunazo weak institutions na strong leaders.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moshi/Mwanza. Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limeisihi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani kwa uaminifu, uhuru na haki.
KTK UCHAGUZI TUSINGEPENDA TAFADHALI KUONA DINI ZINATUMIKA KUINGILIA SIASA. ACHENI WATU WA SIASA WAFANYE SIASA, NA WATU WA DINI WAFANYE DINI.
((RAI BINAFS))
 
Abarikiwe kwa ujumbe mzuri. Wadau naomba mnisaidie kitu, hivi KKKT ina Maaskofu watatu tuu? Yaan Dkt. Shoo, Dkt. Bagonza na Munga? Maana wengine hawasikiki. Ndo kusema wengine wanafurahia yanayoendelea nchini au wanazingatia ule usemi wa kutokuchanganya siasa na dini? Mwisho, niombe kama kuna anayefahamu siku Maaskofu Hawa walipoikosoa CHADEMA anijulishe na Mimi nipate kujua la sivyo nitabaki na Imani kuwa CHADEMA ni chama Cha malaika wanaoishi Duniani ambao hawakosei.
 
Ukitaka kuwaudhi CCM na kuwaharibia Pasaka yao wewe ongelea kuhusu Uchaguzi Huru na haki & Tume Huru....

Sijui kwa nini hawapendi kusikia habari hii njema...
 
Tume ni chombo huru na ambacho kwa miaka yote ya uwepo wake kimeonesha kutenda haki kwa kuhakikisha kwamba washindi wanatangazwa bila zengwe na ndio maana tumekuwa na Wabunge wengi wa kambi ya upinzani Bungeni. Bila shaka Tume itaendelea kutenda haki ila sasa ikitokea wapinzani wamepoteza viti vingi isiwe nongwa kwa sababu sio kwamba uhuru wa Tume ni wapinzani kushinda, uhuru wa Tume ni kuhakikisha haki inatendeka kwa maana hata upinzani wakikosa kiti hata kimoja na ikawa ni maamuzi ya wananchi huo nao uchukuliwe kuwa ni uhuru pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kkt+pic.jpg

Moshi/Mwanza. Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limeisihi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani kwa uaminifu, uhuru na haki.

Kanisa hilo limesema haki na kweli ikitamalaki katika taasisi au taifa lolote, umoja, mshikamano na amani ya kweli hujengwa na kwamba palipo na mambo hayo matatu maendeleo ya watu huwa ni dhahiri.

Ushauri huo umetolewa na mkuu wa KKKT, Askofu Fredrick Shoo katika salamu zake za Pasaka kwa waumini wao ambazo zimesambazwa katika sharika zote nchini.

Uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba 2020 na tayari NEC imeanza mchakato wa uchaguzi kwa kuboresha daftari la kupigia kura na tayari Rais John Magufuli ameahidi uchaguzi huru na wa haki.

Rais alitoa ahadi hiyo alipokutana na mabalozi na wawakilishi wa taasisi za kimataifa kuuaga mwaka uliopita.

Katika salamu hizo za Pasaka, mkuu huyo wa KKKT ametoa wito kwa raia wote kujiandikisha na kushiriki kupiga kura na kutaka kazi hiyo itendeke katika mazingira ya upendo, ukweli, uhuru na haki.

“Watakaogombea nafasi za uongozi au uwakilishi wafanye hivyo bila kuchukiana, uadui, kugombana na kutendeana hila,” alisema Askofu Shoo, ambaye pia ni mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini.

“Ninaisihi sana Tume ya Taifa ya Uchaguzi isimame katika zamu yake kwa uaminifu wote. Tukumbuke kuwa haki na kweli ndio matunda yaupasao upatanisho tulioupata kwa njia ya Yesu Kristo.
“Sote tunaitwa kutenda haki na kusimama katika kweli, pasipo haya, amani haipo. Haki na kweli ikitamalaki katika taasisi au taifa lolote, basi umoja, mshikamano na amani ya kweli hujengwa.

Kama Kristo alivyosukumwa na upendo akaja kutupatanisha na Mungu, kupitia kifo chake pale msalabani, basi na sisi Wakristo na taifa zima tutafute kupatanishwa kati yetu.”
Alisema kabila, cheo, rangi, jinsi wala itikadi visitufanye kugawanyika wala kutengana na kudhalilishana.

“Upendo, upatanisho, haki, amani na kweli uwe wimbo wetu kama taifa,” alisema.
“Kanisa kama taifa la Mungu tunapaswa kuwa mfano na kielelezo katika haya yote, ndipo tunaweza kuwa sauti ya kinabii na ya utetezi kwa wale wanaoonewa na kuteswa.”

Pia Askofu Shoo alizungumzia ugonjwa wa virusi vya corona ambao umeshaua zaidi ya watu 91,000 kote duniani, kwa mujibu wa worldometer.com.

“Wakristo wanaadhimisha Sikukuu ya Pasaka wakati dunia nzima imejaa hofu na mahangaiko kutokana na janga la ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona,” amesema.

“Hakika janga hili limeitikisa dunia. Sote tumeguswa na tutaguswa na janga hili kwa namna moja ama nyingine. Tunatakiwa kuendelea kuchukua kila tahadhari na kufuata maelekezo ya wataamu wa afya.”

Alisema Mungu anao ujumbe kwa Wakristo kujinyenyekeza na kumrudia Mungu kwa toba, akisema kujinyenyekeza si udhaifu bali kinyume chake ni kiburi, majivuno na matumizi mabaya ya madaraka.

Salamu za Pasaka pia zilitolewa na maaskofu wengine wawili wa KKKT, Dk Benson Bagonza wa Dayosisi ya Karagwe na Dk Stephen Munga wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ambao wamesihi Watanzania kutumia maadhimisho hayo kama alama ya tendo la kuponya maisha ya kila mtu na jirani yake.

“Tunaitwa kuvumilia mateso tunapokuwa katika kutetea haki kwa sababu Bwana yu upande wetu. Hakumwacha mwana wake, hawezi kutuacha sisi,” amesema.
Noted
 
Back
Top Bottom