Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Frederick Shoo, ametoa wito kwa viongozi na mamlaka zinazohusika na uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuhakikisha wanazingatia maoni ya wananchi pamoja na ushauri kutoka kwa viongozi wa juu na wadau mbalimbali wenye nia njema kwa taifa.
Katika ujumbe wake wa Pasaka alioutoa jana wakati wa ibada iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Usharika wa Moshi Mjini, Askofu Shoo alisisitiza kuwa ni haki ya kila raia kumchagua kiongozi anayemtaka kwa hiari, na akaonya dhidi ya kuingiliwa kwa mchakato huo na mamlaka yoyote.
Pia soma > Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC): Wote waliokamatwa kwa kudai haki, wakiwemo viongozi wa vyama vya kisiasa, waachiwe haraka na bila masharti
"Waacheni watu wachague kwa uhuru viongozi wanaowataka. Tunaomba sana uchaguzi huu usifanane na chaguzi nyingine zilizopita. Ule wa 2019, 2020 na huu uliofanyika mwaka jana (2024), Hatutaki kuona yale yaliyotokea katika chaguzi nilizozitaja.
"Hatutaki kuona yanajirudia ndugu zangu. Tunaomba wananchi wote msikilize sauti hii. Wenye mamlaka na wahusika wote katika zoezi zima hili la uchaguzi mkuu wazingatie hayo.
...niwaombe wenye mamlaka na wanaosimamia uchaguzi huu, kusikiliza sauti za wananchi. Sikilizeni sauti za viongozi wa juu na wadau wengine wanaoitakia nchi hii mema.
Msizibe masikio, mlitutaka tutoe ushauri, tutoe maoni, tumetoa maoni, heshimuni maoni ya Watanzania. Tutaendelea kusema na mwenye kusikia asikie."