PreGE2025 Askofu Shoo: Wanaosimamia uchaguzi mkuu sikilizeni sauti za wananchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Frederick Shoo, ametoa wito kwa viongozi na mamlaka zinazohusika na uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuhakikisha wanazingatia maoni ya wananchi pamoja na ushauri kutoka kwa viongozi wa juu na wadau mbalimbali wenye nia njema kwa taifa.

Katika ujumbe wake wa Pasaka alioutoa jana wakati wa ibada iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Usharika wa Moshi Mjini, Askofu Shoo alisisitiza kuwa ni haki ya kila raia kumchagua kiongozi anayemtaka kwa hiari, na akaonya dhidi ya kuingiliwa kwa mchakato huo na mamlaka yoyote.

Pia soma > Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC): Wote waliokamatwa kwa kudai haki, wakiwemo viongozi wa vyama vya kisiasa, waachiwe haraka na bila masharti

"Waacheni watu wachague kwa uhuru viongozi wanaowataka. Tunaomba sana uchaguzi huu usifanane na chaguzi nyingine zilizopita. Ule wa 2019, 2020 na huu uliofanyika mwaka jana (2024), Hatutaki kuona yale yaliyotokea katika chaguzi nilizozitaja.

"Hatutaki kuona yanajirudia ndugu zangu. Tunaomba wananchi wote msikilize sauti hii. Wenye mamlaka na wahusika wote katika zoezi zima hili la uchaguzi mkuu wazingatie hayo.

...niwaombe wenye mamlaka na wanaosimamia uchaguzi huu, kusikiliza sauti za wananchi. Sikilizeni sauti za viongozi wa juu na wadau wengine wanaoitakia nchi hii mema.


Msizibe masikio, mlitutaka tutoe ushauri, tutoe maoni, tumetoa maoni, heshimuni maoni ya Watanzania. Tutaendelea kusema na mwenye kusikia asikie."

​
 
Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Frederick Shoo, amewataka wenye mamlaka na wahusika wote wanaosimamia uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kusikiliza sauti za wananchi na viongozi juu na wadau wengine wanaoitakia mema Tanzania.

​
Akitoa salamu za ujumbe wa Pasaka jana katika Kanisa Kuu la Usharika wa Moshi Mjini, Askofu Shoo, amesema viongozi wa dini wameshatoa wito kwamba, ni haki na wajibu wa raia kuchagua viongozi wanaowataka, huku akihimiza uchaguzi huo usiingiliwe na mamlaka iwayo yote.

"Waacheni watu wachague kwa uhuru viongozi wanaowataka. Tunaomba sana uchaguzi huu usifanane na chaguzi nyingine zilizopita. Ule wa 2019, 2020 na huu uliofanyika mwaka jana (2024), Hatutaki kuona yale yaliyotokea katika chaguzi nilizozitaja.

"Hatutaki kuona yanajirudia ndugu zangu. Tunaomba wananchi wote msikilize sauti hii. Wenye mamlaka na wahusika wote katika zoezi zima hili la uchaguzi mkuu wazingatie hayo.

Niwaombe wenye mamlaka na wanaosimamia uchaguzi huu, kusikiliza sauti za wananchi. Sikilizeni sauti za viongozi wa juu na wadau wengine wanaoitakia nchi hii mema.

Msizibe masikio, mlitutaka tutoe ushauri, tutoe maoni, tumetoa maoni, heshimuni maoni ya Watanzania. Tutaendelea kusema na mwenye kusikia asikie."
 
Safi sana
 

Tatizo la hawa Maadkofu, wakiletewa zile million hamsini 50 na Land Cruzer wanachukua na kutoa sifa. Hii ndiyo knayosabsbisha CCM wawadharau wanapokuja na hizi hoja zao. No wonder Makonda anawafundisha nini cha kuhubiri kwenye madhawabu yao wenyewe.
 
Ni muhimu zaidi kwa mgombea uongozi ambae atapata kura sif Gentleman,
ni muhimu zaidi,
kwa mgombea uongozi atakaepata kura sifuri kukubali matokeo kwani hiyo ni ishara kwamba wananchi hawajamuelewa, ajipange kwa Uchaguzi mwingine.

pasiwepo na mgombea kudai kuibiwa asichokua nacho, na itapendeza zaidi 🐒
 
Tatizo la hawa Maadkofu, wakiletewa zile million hamsini 50 na Land Cruzer wanachukua na kutoa sifa. Hii ndiyo knayosabsbisha CCM wawadharau wanapokuja na hizi hoja zao. No wonder Makonda anawafundisha nini cha kuhubiri kwenye madhawabu yao wenyewe.
Wamemsikiliza Makonda? Wao wanatimiza wajibu wao.
 
Kila mtu ana HAKI na UHURU wa kutoa maoni yake lakini sio lazima yafuatwe, kwa sasa uchaguzi mkuu wa October 2025 upo palepale hakuna mwenye nguvu ya kuusimamisha wala kuturudisha nyuma.
Kama Chadema hawakusaini kanuni za maadili kwa kiburi yao basi watambue imekula kwao. Wasubiri uchaguzi wa 2030.
 
Wananchi kila mmoja na maoni yake asichukue maoni yake akahisi ni ya wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…