Askofu wa kanisa la Ufunuo ashutumu viongozi wa Kanisa Katoliki kwa kuingilia masuala ya siasa

Haya makanisa ya machawa, wavhumia tumbo, wanafiki, mafarisayo, manabii wa uongo yafutwe. Hawa wezi wasio kuwa faida na hata elimu ya dini hawana wakae kimya
ASKOFU Mkuu wa Makanisa ya Ufunuo, Paul Bendera ameongoza jopo la Maaskofu 6 na kutoa tamko Sakata la Bandari.

Askofu Charles Fortunatus aliekuwa miongoni mwa Maaskofu hao amewashutumu viongozi wa dhehebu la Kikatoliki kwakile alichodai kuwa wao ndio wamekuwa chanzo cha vurugu kwenye maeneo mengi duniani kutokana na wao kuingilia masuala ya Siasa.

"...MUNGU aliziamini sana dini, Lakini hizi hizi dini zimekuwa wa kwanza kuleta mvurugo katika Dunia hii.

Bila kuogopa kwa sababu tupo kwenye tamko la Kiaskofu, Sisi Wakristo na Waislamu tunaelewana lakini kwenye Wakristo tumegawanyika madhehebu mengi lakini ukisikia Nchi nyingi zilizovurugika Duniani dini kuu Mama ambayo ni Katoliki imekuwa ya kwanza kuanzisha vurugu Duniani kila mahali.

Mimi niiombe Serikali waishauri Katholiki wasijiingize kwenye masuala ya Siasa,washikilie kwenye upande mmoja tu wa Dini."

[emoji2424] Askofu Charles FortunatusView attachment 2725068
 
Askofu kavaa Gwanda la Chadema halafu anakemea Kuchanganya Dini na Siasa

Bure kabisa!

Maoni yao kama ni HURU bila kushinikizwa na CCM behind the scenes basi maoni yao tuyaheshimu
Pale Rwanda mauji ya halaiki wahusika ni hao wanaolalamikiwa,.
JamiiForums-1233605711.jpeg
Mpwayungu village ni shahidi
 
Ni mpongeze kwa kuutimiza ule Unabii wa Bwana Yesu wa Siku za mwisho. Watakuja kwa jina langu na Mbwamwitu waliovaa umbo la kondoo.

Wamesema ukweli wote maana Kanisa Katoliki linaleta tishio la amani ya nchi yetu kwa kuingia huu Nkataba/haya makubaliano ya awali na dp world wenye vifungu vinavyopigiwa kelele kila kona ya nchi. Kanisa Katoliki ni chanzo cha vurugu. Ni wape tahadhari hakuna mtu yeyote ataugawa Mwili wa Kristo Yesu kwa manufaa yake ya kisiasa.
 
ASKOFU Mkuu wa Makanisa ya Ufunuo, Paul Bendera ameongoza jopo la Maaskofu 6 na kutoa tamko Sakata la Bandari.

Askofu Charles Fortunatus aliekuwa miongoni mwa Maaskofu hao amewashutumu viongozi wa dhehebu la Kikatoliki kwakile alichodai kuwa wao ndio wamekuwa chanzo cha vurugu kwenye maeneo mengi duniani kutokana na wao kuingilia masuala ya Siasa.

"...MUNGU aliziamini sana dini, Lakini hizi hizi dini zimekuwa wa kwanza kuleta mvurugo katika Dunia hii.

Bila kuogopa kwa sababu tupo kwenye tamko la Kiaskofu, Sisi Wakristo na Waislamu tunaelewana lakini kwenye Wakristo tumegawanyika madhehebu mengi lakini ukisikia Nchi nyingi zilizovurugika Duniani dini kuu Mama ambayo ni Katoliki imekuwa ya kwanza kuanzisha vurugu Duniani kila mahali.

Mimi niiombe Serikali waishauri Katholiki wasijiingize kwenye masuala ya Siasa,washikilie kwenye upande mmoja tu wa Dini."

[emoji2424] Askofu Charles FortunatusView attachment 2725068
KAMA MNAPINGA WARAKA WA TEC HEBU NA NYINYI TOENI WARAKA WENU ACHENI KUIJADILI TEC JADILINI BANDARI NA MKATABA
 
Hapa wachungaji ndo pa kupatia umaarufu msiache lipite hili 😂😂😂
 
mwenye kanisa mzee gwajima ndio wa kwanza kuchanganya dini na siasa sasa huyu kwann asimkemee boss wake ajiuzulu na ubunge arud kuchapa injili
 
Back
Top Bottom