Nina fuatilia hapa Al Jazeera kuhusu yaliyokuwa yanafanyika kwenye gereza la Sednaya nadhani Assad alikuwa mtu katili Sana. Ndio maana wasyria wameshangilia Sana. Leo halaiki ya watu walifika kwenye gereza la Sednaya kuona kama ndugu zao bado wapo. Ila kwa masikitiko wengi hawapo aidha walikufa kwa mateso au waliuawa na askari wa Assad. Nimejiuliza kwa Nini waarabu wanachukiana hivi?. Unabadilisha gereza kuwa machinjio ya raia wako. Kweli Assad hafai kabisa.
Ukisikiliza shuhuda za hapo utashangaa Sana. Watu walikatwa miguu na wengine kuuawa. Kuna wengine wamepotea kabisa . Inadaiwa wafungwa karibia 1000 waliuawa kwenye kipindi Cha Assad. Huyu hakuwa binadamu wa kawaida .
Umesahau hao wafungwa unaowaona ni zaidi ya 30,000.karibu wote walikuwa kwenye makundi ya kigaidi hasa Isis na alqaida/alnusra front. Umesahau wao walivyokuwa wanachinja watu kikatili, walikuwa wakiwaua wengine kinyama sana, ingia youtube kuanzia 2012 hadi 2016 ndio utawajua hao ni kina nani? Bila Russia kuingilia kati kuna vizazi vingekuwa vimeshafutwa na hao unaowaona.
Kumbuka kule kwa Yazid Irak waliua wanaume na watoto wa kiume wote nasema wote lengo ni kufuta kizazi cha wayazidi ambao wanasemekana ndio watu wenye muonekano mzuri kuliko wote Duniani.
Pia ndio kizazi pekee cha kikristo kilicho survive kwa zaidi ya miaka 2000.Wakawateka wanawake wote na kuwabaka ili wazae kizazi kipya kisicho cha wayazidi na mpaka sasa ipo hivyo. Kila mwanamke au binti wa kiyazidi amezalishwa kwa nguvu mbegu mpya.
Marekani inayokuonyesha hao wafungwa wa Syria yenyewe kwa kuwatumia Wakurdi kule kaskazini inashikiria wafungwa wa ISiS 50,000 hapo hapo ndani ya Syria. Can you imagine hali zao zipoje? Uturuki imeuteka jana mji wa Wakurdi wa Manbij marekani inahofu endapo uturuki ikiendeleza oparesheni zake watawaachia hao wafungwa wote zaidi ya 50,000 ambao Marekani imewafunga kwa kuwatumia Wakurdi.
Kwa hiyo Serikali ya Assad iliwafunga 30,000 lakini Marekani huyo huyo anayejifanya mwema anawashikiria kwenye magereza yake yaliyopo Syria hiyo hiyo more than 50,000 kule kaskazini ambako ameng'ang'ania hataki kuachia kwe visima vya mafuta anakojichotea tuu kama yake.
Hii Dunia ni ya kinafiki kinafiki kinafiki hasa western zaidi ya unayoyajua au kuyaona.