Assad kawatesa Sana Wasyria kwenye gereza la Sednaya

Aisee... nimeona yale Mapipa ya Acid ambayo Mtu akishanyongwa anatiwa ili mabaki ya Mwili yayeyuke..aloo...yule Dikteta kaua sana Watu wake kwa tamaa ya Madaraka.
 
Nina fuatilia hapa Al Jazeera kuhusu yaliyokuwa yanafanyika kwenye gereza la Sednaya nadhani Assad alikuwa mtu katili Sana. Ndio maana wasyria wameshangilia Sana. Leo halaiki ya watu walifika kwenye gereza la Sednaya kuona kama ndugu zao bado wapo. Ila kwa masikitiko wengi hawapo aidha walikufa kwa mateso au waliuawa na askari wa Assad. Nimejiuliza kwa Nini waarabu wanachukiana hivi?. Unabadilisha gereza kuwa machinjio ya raia wako. Kweli Assad hafai kabisa.

Ukisikiliza shuhuda za hapo utashangaa Sana. Watu walikatwa miguu na wengine kuuawa. Kuna wengine wamepotea kabisa . Inadaiwa wafungwa karibia 1000 waliuawa kwenye kipindi Cha Assad. Huyu hakuwa binadamu wa kawaida .
Wewe unafikiri itokee CCM madarakani, hata hapa Tanzania si itakuwa hivyo hivyo? Watu itabidi wazunguke magereza yote na zile kambi za mateso za TISS kwenda kuwatafuta akina Ben Sanane, Azory Gwanda, Kanguye, akina Soka, n.k.

Utawala wa kwetu hapa una tofauti ndogo sana na huo wa Assad. Huko Syria, shetani ilikuwa ukoo wa Assad, hapa kwetu shetani wetu mkubwa ni CCM.
 
Umesahau hao wafungwa unaowaona ni zaidi ya 30,000.karibu wote walikuwa kwenye makundi ya kigaidi hasa Isis na alqaida/alnusra front. Umesahau wao walivyokuwa wanachinja watu kikatili, walikuwa wakiwaua wengine kinyama sana, ingia youtube kuanzia 2012 hadi 2016 ndio utawajua hao ni kina nani? Bila Russia kuingilia kati kuna vizazi vingekuwa vimeshafutwa na hao unaowaona.
Kumbuka kule kwa Yazid Irak waliua wanaume na watoto wa kiume wote nasema wote lengo ni kufuta kizazi cha wayazidi ambao wanasemekana ndio watu wenye muonekano mzuri kuliko wote Duniani.
Pia ndio kizazi pekee cha kikristo kilicho survive kwa zaidi ya miaka 2000.Wakawateka wanawake wote na kuwabaka ili wazae kizazi kipya kisicho cha wayazidi na mpaka sasa ipo hivyo. Kila mwanamke au binti wa kiyazidi amezalishwa kwa nguvu mbegu mpya.
Marekani inayokuonyesha hao wafungwa wa Syria yenyewe kwa kuwatumia Wakurdi kule kaskazini inashikiria wafungwa wa ISiS 50,000 hapo hapo ndani ya Syria. Can you imagine hali zao zipoje? Uturuki imeuteka jana mji wa Wakurdi wa Manbij marekani inahofu endapo uturuki ikiendeleza oparesheni zake watawaachia hao wafungwa wote zaidi ya 50,000 ambao Marekani imewafunga kwa kuwatumia Wakurdi.
Kwa hiyo Serikali ya Assad iliwafunga 30,000 lakini Marekani huyo huyo anayejifanya mwema anawashikiria kwenye magereza yake yaliyopo Syria hiyo hiyo more than 50,000 kule kaskazini ambako ameng'ang'ania hataki kuachia kwe visima vya mafuta anakojichotea tuu kama yake.
Hii Dunia ni ya kinafiki kinafiki kinafiki hasa western zaidi ya unayoyajua au kuyaona.
Dah watu wa MUNGU huwindwa kila siku
 
Unafikiri mtoa mada ana ubongo wa kuelewa ulichoandika?
 
Aisee... nimeona yale Mapipa ya Acid ambayo Mtu akishanyongwa anatiwa ili mabaki ya Mwili yayeyuke..aloo...yule Dikteta kaua sana Watu wake kwa tamaa ya Madaraka.
Nipe link mkuu, nikajionee ukatili kama wa serikali ya CCM
 
Na hutasikia wakiandamana wao wanasubiri myahudi na mmarekani atuhumiwe kuua na kutesa ndiyo wapige kelele, Assad kaua sana waislamu
 
Mimi sishangai hata kidogo, waarabu ni jamii ya watu wakatili sana duniani na hilo halina ubishi.

Kumbuka wakati wa biashara yao haramu ya utumwa ukatili waliofanyiwa mababu zetu kama kutobolewa visigino na kuingiziwa minyororo ili wasiweze kutoroka kwenye msafara wa kupelekwa Bagamoyo.

Kibaya zaidi watumwa vijana wa kiume walihasiwa mithili ya ng'ombe ili wasiweze kuzaa huko uarabuni na Asia walikokuwa wakipelekwa utumwani.

Angalia leo wanavyoweza kujilipua na mabomu na kuua watu hovyo kisa tu kutimiza malengo yao ya kiimani na kwa kweli ni jamii moja ya watu wa hovyo sana.

Wao kwa fikra yao finyu wanatamani kila mtu duniani awe anafuata utamaduni wao wa karne ya saba na kama unakataa adhabu yako iwe ni kukatwa kichwa kwa jina la mungu wao anayeitwa allah. Bure kabisa.
Waliotoboa visigino mababu zako ni haohao mababu wakiuzana wenyewe kwa wenyewe na kutoboana..... Mwarabu munamsingizia tu.
 
Kule si huwa kunapelekwa wale magaidi

Kwa mfano kale kagaidi ka kitanzania kalikoshiriki kulipua ubalozi wao hapa Bongo, si kako huko?

Halafu na kenyewe kana jina la dini yetu,

Hivi, dini yetu na ugaidi vinauhusiano gani?

Ki ukweli, nipo kwenye njia panda, sielewi iwapo siku za usoni nitakuwa tena wa dini hii
Soma kitabu katiba I mean Quran siku hizi zipo za kiswahili na kiingereza pia Uislam ni simpo sana shika nguzo 5 hakuna atakae kuyumbisha na kijidhehebu chochote uchwara, lakini ukimsikiliza kila shekh umepotea
 
Nina fuatilia hapa Al Jazeera kuhusu yaliyokuwa yanafanyika kwenye gereza la Sednaya nadhani Assad alikuwa mtu katili Sana. Ndio maana wasyria wameshangilia Sana. Leo halaiki ya watu walifika kwenye gereza la Sednaya kuona kama ndugu zao bado wapo. Ila kwa masikitiko wengi hawapo aidha walikufa kwa mateso au waliuawa na askari wa Assad. Nimejiuliza kwa Nini waarabu wanachukiana hivi?. Unabadilisha gereza kuwa machinjio ya raia wako. Kweli Assad hafai kabisa.

Ukisikiliza shuhuda za hapo utashangaa Sana. Watu walikatwa miguu na wengine kuuawa. Kuna wengine wamepotea kabisa . Inadaiwa wafungwa karibia 1000 waliuawa kwenye kipindi Cha Assad. Huyu hakuwa binadamu wa kawaida .
Ila hutasikia wenzao wa huku TZ wakitoa tamko!wako kimyaàaaa!ila angekua kafanya mmarekani au muisrael hapo ungesikia yowe kila mahali!BATAWAHED
 
— 🇮🇷 🇮🇷 🇸🇾 Deputy Commander-in-Chief of the IRGC 'Khatam al-Anbiyaa' Headquarters: 'Bashar al-Assad did not request Iranian help – in fact he actibely prevented us from coming and helping'

General Mohammad Jafar Asadi, deputy commander of Khatam al-Anbiyaa HQ:

– Bashar al-Assad said to one of our (Iranian) officials: 'My soldiers have truly become either smugglers or thieves, they only defend those who offer them bribes and privileges. They could not defend me, and when I wanted to protect at least Damascus, I realized that they were not able to protect Damascus either.'

– Bashar al-Assad did not allow us (the IRGC) to go help the Syrian Arab Army, although he asked us for assistance in the past, but this time he not only did not ask, but he was worried about us leaving, and said that 'if you come, Israel will probably attack us'.

– Turkey is a part of NATO, and we should not see or accept this country anywhere outside of America and Europe. Turkey is a part of them, and with this attitude, it serves America. America is active behind the scenes.

– It seems that the factions present in Syria will clash with each other based on their own different interests. Maybe separating Syria is Turkey's desire, because they have been coveting a part of Syria for a long time.

@Middle_East_Spectator
 
HUYUU WANGEMPELEKA AKAONA WALE BIKIRA 72 HANA ADABU SIO WA KUONDOKA HIVIHIVI
 
Waliotoboa visigino mababu zako ni haohao mababu wakiuzana wenyewe kwa wenyewe na kutoboana..... Mwarabu munamsingizia tu.
Wewe unawatetea kwa sababu kwa fikra zako potofu unaamini kwamba wenyewe ndio wamekufanya umjue mungu wao anayeitwa allah.
 
Biashara ya utumwa ilifanywa na waarabu tu.?
Babu zako walienda U.S.A, U. K kutafuta maisha..?
......... Lakini huko Ulaya na Marekani hawakuteswa kama walivyoteswa wale waliochukuliwa na waarabu na ushahidi upo kabisa.
 
Nilipita huko miaka ya nyuma yaani Syria na Jordan nchi mbili tofauti kabisa
Syria ni wakomunist ukiingia kutoka ni kazi maana hata $ hupati ni mwendo wa kuruka tu
Ubabe mwingi hata Iraq ina unafuu sana enzi hizo
Kote nimeishi
Ndg yangu sisi tumeishi Iran Kwa muda sasa. Kama miaka 11. Kwa sasa kuna taharuki kubwa Sana huku. Waafrika wengi wameanza kung'oa hususan wanaotoka nchi zinazoongea kingereza. Nikipata muda nitawaeleza NI Kwa nn. Mtashangaa Sana. Kuna mengi wanaafrika hawajui
 
Ni kweli he was a dictator

Back
Top Bottom