At their peaks,nani alikuwa mkali zaidi...Marlaw Vs Mb Dogg?

Hivi Mb maana yake ni Member of Parliament au mimi tu na akili zangu za kukariri
 
MB dog... kwa mara ya kwanza natafuna papuchi ngoma ya ratifa iko radio inabang.... siwezi kusahau hili asee
 
Kuna muda nilikua najiuliza uyu jamaa anawezaje kutunga nyimbo kias kile mb dogg sio tu kwamba marlow au nan mpaka leo hii ni msanii mkubwa sana ambae aliutendea haki mzik wa bongo fleva tutawashindanisha wasanii kimapenz ya kibinadam ila mb dogg ni hatar zaid
 
Nlikua form 2 kipindi hicho tulikua tuna enda kusoma magetoni kwa brother wake classmate wetu pale Getho kulikua na radio yule bro alikua kanunua album ya MB Doggy inagongwa asubuh hadi jioni nlikua nikitoka tu shule nawahi Getho kujisomea huku nasikiliza madini ya huyu nguli wa mziki, salute kwake, kilinge chetu kilikua cha watu wa hip hop ila kwa MB doggy tuli legea
 
kuna moja anadai ya kwamba mademu wengi wanamshobokea sababu ana jina ila yule demu anayemuelewa hamtaki
hii ngoma nasikia ilikuwa dedication kwa nancy sumari,kwa mujibu wa wana JF waliokuwepo Daslamu miaka hiyo
Mapenzi ni kitu gani ft chelea man kama sikosei.
 
Ingekimbiza sana, manake hatuelewi Mapiano yanayoimbwa na wasanii wa sasa...

Hivi mapiano ilitokea wapi? Lol
Nafikiri itakuwa biti zake zinatengezwa na piano nyingii, ndio maana yakaitwa MAPIANO

[emoji23]
 
Hadi sasa,,, MB Dog kazoa kura zote!
Mb dog ni mkali zaidi!
Jamaa alikuwa anajua sana
Majuzi tu hapa nilijikuta nazitafuta nyimbo zake nazipakua kwenye sim yangu,, nikiwa nmetulia zangu napiga ngoma moja baada ya nyingine najiskia poa sana
 
Iv marlaw alikua anaimba nini,
Na dog man kweli at his peak ebu tuache utani bora ata ungemuweka tonya kidg
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…