Nikiweka Ushabiki wangu kwa marlaw pembeni. Mb dog anatakiwa kuwekwa na G.O.A.T wenzake maana alikuja na sound yake ambayo nadhani ndio foundation ya hizi nyimbo za mapenzi unazosikia leo,
hata Ukiiweka bongo flava katika Major Eras ,
1. (Kabla ya 2005)
Era ya Different tunes yaani kila mmoja aliimba kwa tune yake Dully sykes, Lady jay dee,TID, Q chief, Ray C , Juma nature, Stara thomas etc (Bongo flava halisi, Zouk, Rhumba, Rnb).. hili ndo kundi la waasisi "Era ya passion na muziki mzuri"
2. (2004 - mwanzoni mwa 2010)
Era ya Mb dog maana watu wote waliofuatia kama kama Kassim, Z anto, Ali kiba, Rich mavoko, Diamond (wa mwanzoni) walipita katika njia zake. Hata tune nyingi za leo ni kama zimetokea kwake
3. (Mwanzoni mwa 2010 hadi 2015)
Era ya T.H.T ama Ruge mutahaba, huyu hakuwa msanii ila alikuja na wasanii kama Barnaba, Ditto, Mwasiti, Amini, Marlaw, Maunda Zorro, Vumilia.. Ambao walikuja na muziki ambao ni rafiki zaidi kwa live band tofauti na ala ya Mb Dog
4. (2015 hadi sasa)
Tupo Kwenye Era Ya Commercial music ikiongozwa na Diamond platnumz.. Kinaimbwa kinachouza, haiangaliwi ladha ya muziki inaangaliwa investment and return. Watu wanatengeneza makundi na labels ili wasurvive maana muziki umekuwa expensive.. Watu kama marioo wenye multiple talents kubwa na back up ndio wanaweza kusurvive
Kwa kuangalia hili, Mb Dog anahitaji competition na watu walioleta impact kwenye muziki kwa ujumla kwa hiyo marlaw sio fit kwake.. Anahitaji Hall of fame