Atakayeweza kuniloga nitamlipa Milioni 25

Kama unaamini uchawi haupo it means unaamini Mungu hayupo pia, swala la kutorogeka ni jingine huenda nawe ni mchawi gwiji au mtu wa dini sana.
 
Huwajui walimwengu vizuri.. yaani nimecheka sana leo kwa upumbavu ulioandika.. lool Tanzania sirudi
 
Sijakuoana ila ni bonge la mnaaaafiki aiseee! Uo unafiki tayari umelogwa wewe!
 
Kawaida ni nini na tofauti na kawaida ni nini na unajuaje hii ni kawaida na hii ni tofauti na kawaida?

Mababu zetu waliona redio inatoa sauti ya mtu, wakaona hii si kawaida, ni uchawi.

Redio kutoa sauti ya mtu ni uchawi?
 
[emoji23][emoji23]


Ngoja nione kama Bufa na Kiranga bado wapo au kishawakuta kitu[emoji23][emoji23]
Kama hatupo, na kitu kimetukuta, hilo litamaanisha nini?

Je, hilo litamaanisha uchawi unafanya kazi?

Mbona watu wanakufa kila siku kwa sababu tofauti na uchawi?

Logical non sequitur.
 
Kama unaamini uchawi haupo it means unaamini Mungu hayupo pia, swala la kutorogeka ni jingine huenda nawe ni mchawi gwiji au mtu wa dini sana.
Kwangu mimi, sababu zilezile zonazonifanya nisikubali kuwepo kwa uchawi, ndiyo hizo hizo zinanifanya nisikubali kuwepo kwa Mungu.
 
Kawaida ni nini na tofauti na kawaida ni nini na unajuaje hii ni kawaida na hii ni tofauti na kawaida?

Mababu zetu waliona redio inatoa sauti ya mtu, wakaona hii si kawaida, ni uchawi.

Redio kutoa sauti ya mtu ni uchawi?
asante, nashukuru kwa swali zuri na kwa sababu mimi ni mwislamu nitakujibu kiislamu... unaweza kupoteza/kuibiwa kitu kisha ukaenda kwa mganga na mganga yule kupitia ramli akakuambia namna kitu chako kilivyopotea ima kwa kuibiwa akakutajia aliyekuibia na namna alivyoiba au kwa kudondosha akakutajia mahala kilipokutupika (ulipodondoshea). hiyo kwenye uislamu tunaita umetumia kuagua ili kujua siri (ghaib). tunaita siri/ghaib kwkuwa huyo anayejiita kuijua hakuwepo na wala hakutegesha kinasa sauti, video camera, wala micro cheap yoyote kuyanasa mambo hayo wala hakuna mtu yeyote anayemwambia. jambo hilo na mengi mfano wa hayo siyo ya kawaida

mambo ya kawaida nitakupa mifano kwa yale ya kutendwa na binadamu mfano ni kuona kwa kutumia macho, mtu kusikia kwa usikivu wa kibinadamu, kutembea ardhini, kupenya kwenye maada ya hewa tu, kula na kunywa vyakula vya kibinadamu, na kadhalika

akitokea leo mtu akasema yeye anaona hata akifumba macho (siyo kwa hisia bali kuona hasa na kuainisha mwonekano) au anaona vitu/watu hata walio nyuma ya ukuta wa nyumba basi hilo jambo tutasema siyo la kawaida katika kuona

akitokea mtu akasemaanasikia vishindo vya mwingine anayetembea kilomita kadhaa mbali na hapo alipo yeye au yupo sokoni na akasikia sauti/kishindo ya sisimizi anayepita chini basi mtu huyo tutamwona ana hali isiyo ya kawaida katika kusikia

ikitokea mtu anatembea bila kukanyaga chini (anatembea hewani) au mtu anakula machuma anayatafuna kabisa au mtu anapenya kwenye kioo bila kioo kupasuka basi hapo tutasema hayo yote na mfano wa kama hayo siyo mambo ya kawaida... eidha ni uchawi wa kutumia majini au mashetani ama uchawi wa mazingaombwe na kiinimacho

swala lako la redio linaelezeka kisayansi na kivyovyote vile lakini swala ambalo si la kawaida maana yake halipimiki kisayansi. kwa waislamu hayo mambo yasiyoelezeka kisayansi yanagawika katika makundi mawili yaani kuna mengine ni miujiza/ilham/karama/n.k na mengine ni uchawi/mazingaombwe/kiinimacho/n.k
 
Hujaeleza kawaida ni nini na isiyo kawaida ni nini, na unatofautishaje mawili hayo, na utajuaje hii ni kawaida tu, ila wewe hujawahi kuiona, hivyo unaweza kufikiri si kawaida, na hii hujawahi kuiona, kwa sababu si kawaida.

Maana mtu asiyejua mchezo wa karata tatu, akiona siku ya kwanza, anaweza kuona hii si kawaida, ni uchawi.

Wakati wanaocheza kila siku wanajua ni trick tu. Si uchawi.

Sasa wewe unatofautishaje kitu cha kawaida ambacho hujawahi kukiona na kitu ambacho hujawahi kukiona kwa sababu si cha kawaida?
 
Wewe kilaza bado niko na wewe. Jifunze kuandika. Kuloga ndio nini?
Ukiona mtu haelewi muda mrefu Anza kutia shaka juu ya afya ya akili yake. Na ukiona mtu Kila wakati anajibu hoja kupitia matusi na lugha mbovu basi elewa kuwa hakuna mtu pale.
 
Mbona usharogwa zamani mwanangu?
 
Kesho ukiamkia ndani kwako na mkoa unaoishi labda sio mimi, na hiyo mil 25 yako siitaki ila nataka nikuoneshe tu mauwezo ili upunguze dharau kwa sisi washirikina professional
 
Kwangu mimi, sababu zilezile zonazonifanya nisikubali kuwepo kwa uchawi, ndiyo hizo hizo zinanifanya nisikubali kuwepo kwa Mungu.
Aminisha dunia nzima kuwa Mungu hayupo kuangaika humu JF inaonekana wewe una uelewa mdogo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…