Atakayeweza kuniloga nitamlipa Milioni 25

Atakayeweza kuniloga nitamlipa Milioni 25

Twende ukakabizishe hizo hela kabisa kwa makubaliano ya kusainishana kisheria alafu nipe majina yako matatu na uzi kutoka kwenye nguo yako.... Niruke pale tunduma chap kwa mzee mmoja anaitwa Nyang'anya Wananyungi Filtahai Bin Nyang'anya, Wewe week tu unabaka mwanafunzi na ndo unakuwa mwanzo wa matatizo yako.
🤣🤣🤣 asifanye mchezo..na mbaya zaidi mtu akilogwa anakua hajijui ila watu wa pembeni ndo watamsaidia..unaweza pigwa kitu kesho huioni hiyo siku..asicheze na hizo mambo
 
Yeye si ametaka kurogwa? Au mada yake inasemaje,

Una dare kitu halafu unalinda privacy basi uzi wake utakua hauna maana tena
Sababu ili aweze kulogwa watahitaji vina saba kutoka kwake..mfano jina lake ndo limebeba roho yake, e.t.c hapo akitaja jina tu la kwake na mama yake..ndo mwisho wake..asicheze na hizo imani ambazo hata katika vitabu vitakatifu zimeandikwa
 
alete aone kuna mwamba since 2007 kapigwa tukio kisa kuiba maandazi na huyo mhusika ajawahi kuonekana mpaka kesho.
Mm pia nimeshukuhudia mtu ni chiz had Leo alipewa matunda mzee mmoja akauza hakupeleka ela akamdhulumu mwenye Shamba Yani ni chizi anavua nguo had hadharani
Mwingine aliiba simu nae anaokota makopo
 
Kuna kitu sielewi.

Nitatoa mfano.

Humu kuna watu tulikua tunatambiana juu ya kujua drafti, tukakubaliana tukakutana sehemu tukawa tunacheza sana drafti.

Lakini ikifikia kwenye kulogana unashangaa ghafla hicho kitu kinazunguka tu na hakiwi. Umeambiwa taja jina? Usianze kwanini hujalitafuta mwenyewe mtajie mpe kila anachotaka.

Halafu tuone nini kitakua, haya mambo ya kuzungushana ni utoto. Na kwenu wachawi na mnaowajua wachawi 25M siyo pesa ndogo. Fuata huyu mtu PM kutaneni nyie tuambieni mmekutana na steps mlizochukua na tuambiwe tutarajie nini. Piga tukio baki na 20+ M iliyobaki mpe mganga.

Haya mabishano ya mbona huwezi kuona na huyu anakomaa ukitaka nikuloge nipe hiki au kile ni kupotezeana muda.
 
Back
Top Bottom