ATC Sasa Yaanza Kuleta Heshima ya Nchi, Yapunguza Tanzania Kufanywa Shamba la Bibi, FastJet Yapumulia Mashine, Soon Itafungasha Virago!.

ATC Sasa Yaanza Kuleta Heshima ya Nchi, Yapunguza Tanzania Kufanywa Shamba la Bibi, FastJet Yapumulia Mashine, Soon Itafungasha Virago!.

Paskali
Sikujua kama na wewe una fikra za kuhodhi na ukiritimba. Kama ulihoji taratibu mbaya za manunuzi, iweje kitu kilichonunuliwa kwa taratibu mbovu sasa ukiunge mkono? Hujapona bado!

Ngoja sasa nikuunge mkono unavyotaka:
-Funga Fastjet, Precision, ibaki ATC tu
-Funga Vyuo Vikuu vya binafsi vibaki vya serikali
-Funga shule zote binafsi, zibaki za serikali
-Funga biashara zote
-Funga mahoteli ili mikutano yote tufanyie chini ya miti na madarasani
-Funga vivuko vyote na boat zote binafsi ibaki MV Nyerere tu
-Funga maduka yote ya madawa ibaki MSD tu
-Funga magazetu yote ibakie Uhuru, Mzalendo na Tanzanite
-Funga TV zote ibaki TBC
-Magari yote barabarani shusha speed limit mpaka km 20 lakini STK zote ziende 120
-Magari yote binafsi yawe na insurance tatu - mbele, kati na nyuma - lakini ya serikali hata mafuta yasinunue
-Funga vyama vyote vya kisiasa kibaki kimoja chenye nguvu kuliko "mungu"
-Funga NGO zote ibaki moja inayoitwa CCM
-Funga mabenki yote ibaki Benki Kuu tu
-Funga hata barabara zote ibaki Makonda Flyover
-Funga Halmashauri zote nchini ibaki ya Chato tu ndiyo inafanya vizuri

Wewe funga tu, si Kufuli unalo Paskali. Hata makaburi yetu funga isije kuwa kuna aliyezikwa hai akaja kufufuka na kutoka. Miili yote twakupa, mioyo si halali yako.
Hamjui mnachotamani na kufunga kwenu. Huku mnashadidia kutengeneza ajira lakini kufunga kila kitu mnapenda?! Duh! hata kifo kinawashangaa.
 
Karibia Dola itapanda tena na bei ya vipuri vya dreamliner zitapanda, hii ndege jamani itafutiwe route ya nje kabla haijapitwa na wakati..
 
Nazani una jaribu kufikisha ujumbe kuwa biashara ya ndege... Ina hasara huko mbele hivyo tukae mkao wa tayari...

Mashirika mengi yame firisika... Na fastjet kupata ugumu wa biashara ni muendelezo wa kielelezo...
 
1537984715680-png.878813
..............
1537984959402-png.878817

Huyu jamaa na mswaki wake wa kisasa wa bei mbaya!​
 
Kama hali hii itaendelea Fastjet wakafunga virago na Precision air wakafa au wakabaki taabani, watakaoumia ni wananchi.

Mwenyewe umekiri kwamba hizi mbio za ATC ni za sakafuni, siku zikifika ukingoni. Huduma za ndege zitakua ghali mno.

Bombadier ziko wapi? Kwa vyovyote vile Dreamliner inaendeshwa kwa hasara.
Tatizo ccm imesaga akili za watu kiasi kwamba hata jambo linalowaletea Mauti wao wanarukaruka kwa Shamgwe....hawataki kuamini kuwa hilo Dude linaendeshwa kwa hasara lengo nikulaghai wajinga kesho na keshokutwa unaambiwa ulipe kodi yakukanyaga Ardhi ili wafidie hizo Gharama anyways
 
Uliwashauri wapi na nani haswa

Naona nilipitwa

Ila kushushuka mnashushuka kwenye mengi na bado

Magufuli oyeeeeee
Mkuu, Kuna mada ni heri kukaa kimya kuliko kuchangia halafu ukaleta maneno
kama upo kwenye vijiwe vya kusukana. Kuna vitu siyo vya kuingiza UKADA hivi
unapomtathimini Pascal Mayala unaweza kusema yupo CHADEMA au CCM
Punguza mapenzi yasio na maana eti "Kushushuka"
 
Back
Top Bottom