ATC Sasa Yaanza Kuleta Heshima ya Nchi, Yapunguza Tanzania Kufanywa Shamba la Bibi, FastJet Yapumulia Mashine, Soon Itafungasha Virago!.

ATC Sasa Yaanza Kuleta Heshima ya Nchi, Yapunguza Tanzania Kufanywa Shamba la Bibi, FastJet Yapumulia Mashine, Soon Itafungasha Virago!.

AKILI ZA KITANZANIA BWANA.SASA FASTJET IKIFA NDIO ATCL ITAFANIKIWA SANA.BADALA YA KUSHAJIISHA USHINDANI KATIKA SOKO.KUCHOCHEA HUDUMA BORA NA GHARAMA NAFUU.SASA AKIBAKI PEKE YAKE UNAFIKIRI NAULI ITABAKI HIVYOHIVYO AU HUDUMA ZITABAKI HIVYOHIVYO?

FIKIRIENI SANA MNAOSHABIKIA SEKTA BINAFSI KUMINYWA NA KUFANYIWA FITNA.TULITOKA HUKO KWA SERIKALI KUMILIKA NJIA ZA UCHUMI.TULIISHIA WAPI?

KAMA KUSOMA HUWEZI,ATA PICHA HUONI MCHANGO WA SEKTA BINAFSI KATIKA UCHUMI.

UNATAKA TURUDI KWENYE THE SOCIETY EAT NOTHING!AMA.KUPANGA FOLENI KWENYE MADUKA KUNUNUA BIDHAA.HELL NO!

TUMETUMIA MIAKA 20 NA USHEE KUJENGA UCHUMI HURIA NA KURUHUSU SOKO KUMILIKI NJIA ZA UCHUMI.MTU MMOJA ASITUYUMBISHE.KAMA YEYE HAPENDI.SISI TUNATAKA USHINDANI KATIKA SOKO.
 
Unaposhangilia mashirika binafsi kua na hali ngumu au kuyaombea yafe sio kwamba itawaumiza wao tu bali na sisi pia maana utakosekana ushindani na ATCL itajiwekea bei yoyote itakayo ona inafaa kwake.
Nauli ya Ijumaa kutoka Dar kwenda Dodoma kwa ATCL ni 295,000 (one way) na hii route ATCL wako almost peke yao.

Lakini nina uhakika hizo nauli wakija kuzipandisha hizo ndege zitakosa abiria maana hata leo bado unakuta siti kibao hazina watu.

Na wajue tu kwa route ya Dar to Dodoma, treni ya kisasa ikianza, ni lazima abiria watapungua maana nauli za ndege ziko juu sana unless ukate ticket mwezi mmoja au miwili kabla ya safari ndio utapata unafuu.
 
wewe unajua wapi mambo ya aviation na hicho kidiploma chako cha ustawi wa jamii
Mbona hutoi mfano kwa Qatar au Emirates
Kumbuka bado ndege tatu zinakuja kwa kazi hiyo ya kukamata soko la ndani na kikanda
Hayo mashirika hujui na yenyewe huwa yanabebwa na serikali zao?

Hiyo Dreamliner pamoja na kuweka bei za offer ilikuwa inajaa?

Alafu kwa akili yako wanaopata faida kwenye hii biashara unadhani wanategemea mauzo ya ticket tu?
 
Wewe unachojua ni NDIYOOOOOO
wewe unajua wapi mambo ya aviation na hicho kidiploma chako cha ustawi wa jamii
Mbona hutoi mfano kwa Qatar au Emirates
Kumbuka bado ndege tatu zinakuja kwa kazi hiyo ya kukamata soko la ndani na kikanda
 
Tiamaji tiamaji
Acheni kujifariji na vitu ambavyo havipo.Huo ndio ukweli.ATCL ina-survive ni kwasababu tunaibeba lakini sio kwasababu kuna biashara nzuri.

Route ya Dar to Dodoma ATCL iko yenyewe lakini bado ndege haijai na hata menu wanayotoa kwa abiri inaashiria hali si nzuri.
 
Nazani una jaribu kufikisha ujumbe kuwa biashara ya ndege... Ina hasara huko mbele hivyo tukae mkao wa tayari...

Mashirika mengi yame firisika... Na fastjet kupata ugumu wa biashara ni muendelezo wa kielelezo...
Nikiwaza hivi ulivyosema, ndio kabisa huwa naishiwa matumaini na hii biashara.
 
Wewe wahaya wenzako hivi sasa wanatwanga Balimi na nyama choma wewe unakondeana na ki tecno ulicho nunuliwa na chakubanga
Mkuu paskal hizi ndo habari za kusikia,sio Wale jamaa wa....., kila kukicha ,asubuhi mpaka linatobela ni stry za mkulu tu,mbaya zaidi wanabadilisha heading ,maudhui ni yale yale
 
Je ushindani unaondelea baina ya hizo ndege zetu ni ushindani wa uwezo au wa upendeleo. Maana kama ni wa upendeleo ni dhahiri tutajenga mazingira ya kuja kukwama huko mbele. Huenda ndege zetu zinaendeshwa kwa mapato toka nje ya pato lake halisi. Je hali hiyo ni afya iwapo ndege za binafsi zitafunga shughuli zake? Naogopa sana mahali pasipo na ushindani sawia kwani ni kujidanganya wenyewe.
 
Je ushindani unaondelea baina ya hizo ndege zetu ni ushindani wa uwezo au wa upendeleo. Maana kama ni wa upendeleo ni dhahiri tutajenga mazingira ya kuja kukwama huko mbele. Huenda ndege zetu zinaendeshwa kwa mapato toka nje ya pato lake halisi. Je hali hiyo ni afya iwapo ndege za binafsi zitafunga shughuli zake? Naogopa sana mahali pasipo na ushindani sawia kwani ni kujidanganya wenyewe.
Hili ndio swali la msingi la kujiuza kwa sasa na nauli hizo ndio tutaendelea nazo mashirika mengine yakijitoa?

Alafu tumejiuliza ni kodi kiasi gani tunakwenda kuikosa kwa haya mashirika kujitoa na zaidi tujiulize iwapo ATCL ikibaki peke yake itafidia kodi hiyo?
 
Kama maisha ya dar ndiyo hayo ya kutgemea buku 7 za lumumba nakushauri rudi kwenu bukoba ukalime mutwishi na fia hata nauri nitakulipia
Inatakiwa mpaka ku blow huo utoko kichwani mwako ndo utakua ahueni,vinginevyo ni janga,hili gonjwa lako ni la kurithi toka kwa wazazi wako
 
Hatutaki kuchekwa
Je ushindani unaondelea baina ya hizo ndege zetu ni ushindani wa uwezo au wa upendeleo. Maana kama ni wa upendeleo ni dhahiri tutajenga mazingira ya kuja kukwama huko mbele. Huenda ndege zetu zinaendeshwa kwa mapato toka nje ya pato lake halisi. Je hali hiyo ni afya iwapo ndege za binafsi zitafunga shughuli zake? Naogopa sana mahali pasipo na ushindani sawia kwani ni kujidanganya wenyewe.
 
Wanabodi,

Japo mimi ni miongoni mwa wale tuliopinga ununuzi wa ndege kwa cash money, na serikali yetu kufanya matumizi makubwa kama haya ya manunuzi bila idhini ya Bunge, lani mimi ni mmoja wa massuporter wakubwa wa hatua mbalimbali za rais Magufuli kufufua uchumi wetu, ikiwemo kulifufua Shirika la Ndege la ATCL.

Baada ya kuwasili kwa Bombadier, nikashauri serikali yetu, tutumie political will kuinusuru ATC na ushindani usio sawia.
Je, ATCL inahujumiwa kibiashara? Tutumie a political will kuinusuru au tuiache iangamizwe na ushindani? - JamiiForums

Fast Jet nao wakapunguza sana nauli zao na kuamua kupeleka ndege zao routes zile zile za ATC kwa bei poa zaidi, kwa vile Fast Jet wanatumia JET, na ATC wanatumia pangaboi, Fast Jet aliendelea kuipiga bao ATC.

Ujio wa Dreamliner umekuja kufunga kazi. Japo siungi mkono kurusha dege kubwa kama dreamliner kwa domestic routes ambazo ni route fupi fupi, sio tuu tunaichosha bure dreamliner yetu, bali pia tunaichakaza kwa paa shuka paa shuka ndani ya muda mfupi, lakini baada ya kuipokea taarifa hii kutoka humu humu jf, African airline Fastjet reveals urgent need for more cash - JamiiForums
kiukweli sasa ndio naungana na Watanzania wengine kumpongeza rais Magufuli kwa ununuzi wa ndege hizi. Pia sasa nalipongeza shirika la Ndege la Tanzania, ATCL kulirusha hili lidude routes za ndani za Mwanza na Kilimanjaro, kwa sababu kufuatia ujio wa Dreamliner, sasa Fast Jet, inapumulia mashine, na sio tuu itasitisha huduma zake Tanzania na kufungasha rasmi, bali Fast Jet, itakufa rasmi kwasababu roho ya Fast Jet, ni biashara ya Tanzania.

Kufuatia Dreamliner ya ATCL kuruka Mwanza na Kilimanjaro, Fast Jet na Precision zimekosa abiria wa Mwanza na Kilimanjaro, hivyo sasa Fast Jet, ni soon atakubali matokeo na kunyanyua mikono yake juu, atabaki Precision, hivyo kama anataka usalama na kuendelea ku survive, asarender routes za Mwanza na Kilimanjaro kwa ATCL, yeye aende routes nyingine za mikoa mingine ambayo haina ndege kama Singida, Shinyanga, Songea etc.

Kufa kufaana, hivyo taarifa za Fast Jet kupumulia mashine ni habari njema kwa Watanzania wazalendo na ATC yetu, kwa sababu nimeisha safiri na Dreamliner safari 8, na hakunahata safari moja ndege ilijaa, hivyo nikaogopa kama ni hii, then nikajisemea kimoyo moyo kuwa hii Dreamliner inaoparate kwa hasara, lakini kutokana na zile mbwembwe za mapokezi ya ndege hii, no one can dare say that!, hivyo hasara hiyo itabebwa kimya kimya kufa kizungu na tai shingoni, hivyo kifo cha Fast Jet ni neema kwa ATC ambapo sasa dreamliner yetu itajaa.

Japo sio ustaarabu kufurahia matatizo ya mwenzako, kama kifo cha Fast Jet kwa sababu, wafanyakazi ni Watanzania wenzetu, na Fast Jet, ilikuwa inafanya biashara halali na kuchangia uchumi wa taifa, lakini kwa muda mrefu Tanzania imekuwa ikifanywa ni shamba la bibi, kwa kila mtu kujichumia na kujivunia as if Tanzania haina wenyewe, kwa vile Fastjet ni shirika la kigeni, then faida yote inapelekwa huko nje kwa wenye hisa, hivyo ATC sasa imeonyesha, kwenye usafiri wa anga, Tanzania ina wenyewe. Hivyo hata Fast Jet wakifungasha, abiria bado wataendelea kupanda ATCL, hivyo taifa kuendelea kupata mapato, na kwa vile ATC bado inaleta ndege nyingine 4, itaweza kuwameza wafanyakazi wote wa Fast Jet.

Hivyo sasa ATC sio tuu itatawala soko, bali sasa ndio itarudisha heshima ya nchi, inarudisha heshima Taifa, na huu utaratibu wa kuwafungasha virago watu, uendelee kwa routes za Afrika Mashariki, tuje routes za Ghuba, India na China, kisha tufunge kazi na New York na London.

Poleni sana Fast Jet, Hongera ATCL
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza Wafanyakazi 136! - JamiiForums

Ushauri wa Bure Kwa ATC Fanyeni Over Booking name Kuweka Waiting List. - JamiiForums

Ndege ya ATCL yachelewa kuondoka ndani ya muda; watoa ufafanuzi! - JamiiForums

Tupunguze "kuisimanga" ATCL, haijengi zaidi ya kukatisha tamaa - JamiiForums

Zitto Zuberi Kabwe Ni Mchochezi, Akamatwe, Ashitakiwe Kwa ...
Private sector siyo adui wetu.Fastjet walitufaa sana wabongo wakati huo,sasa kwa sababu za ushindani usio wa haki tena artificial,mnawabeza.Hii ina gharama zake huko mbele Kwani tunazunguka katika vicious cycle ileile ya ATC ya awali tukitaraji Matokeo tofauti.
 
Back
Top Bottom