ATC Sasa Yaanza Kuleta Heshima ya Nchi, Yapunguza Tanzania Kufanywa Shamba la Bibi, FastJet Yapumulia Mashine, Soon Itafungasha Virago!.

Mkuu Pascal Mayalla

Kuna mambo mawili matatu tusiyoyazingatia kwa kuangalia mada yako

1. ATCL kwasasa inaendeshwa kwa ruzuku, haijaweza kutoa ''quota' yoyote kwa mahesabu

2. Kuondoka kwa sekta binafsi kunatengeneza monopoly ya ATCL .
Monopoly inatengeneza 'volition' katika kuamua nauli, ubora wa huduma n.k.

Nauli unazoona ni kwasababu ya competitions, kusherehekea kifo cha sekta binafsi ni sawa na 'kula peremende' kwa kudhani ni mlo. Mbele ya safari ni tatizo

Unakumbuka Tritel? Ilikuwa kampuni ya simu ya wenye nazo.

Kampuni zingine ziliporuhusiwa bei ikaanza kushuka na sasa competition ni kali miongoni mwao japo kuna kaunafuu ukilinganisha na zama za Tritel za ''1 minute 5 dollar''

Bei za simu zingekuwa nafuu kama serikali ingeondoa 'price gouging' inayotokana na 'price fixing' ya mashirika makubwa

3. Competitor wa ATCL siyo Fast jet , ni KQ na wenzake na huko ndiko aelekeze nguvu. Akishindwa kupambana na KQ, gharama za uendeshaji zitamshukia Mtz na sudden death

4. ATCL ikiwa ATC iliwahi kupewa monopoly ya soko ikashindwa.
Unadhani ni kitu tofauti kimefanyika tofauti na zamani?

Mang'ula machine tools, Tanganyika Packers , Magunia Morogoro, Polyster, Chuma Tanga, Mbolea Tanga, Mutex , Mwatex, UFI, Swala, n.k. vilikuwa havina washindani wa ndani
Kwanini vilikufa? Iko wapi Kamata? Iko wapi UDA? Iko wapi Tacoshil?

Mag3 JokaKuu
 
Uliwashauri wapi na nani haswa

Naona nilipitwa

Ila kushushuka mnashushuka kwenye mengi na bado

yani umesoma mstari mmoja ukamaliza, ukaanza mipasho😁😁

ile link hata hukutaka kujua alishauri nini?? wakati siku nyingi Pasco alisema ikiwezekana bei zishushwe ndege ijae tusikomalie tuu ma rate makubwa n.k iwekwe kampeni kitaifa

Magufuli oyeeeeee
 
paskali....ninachojuwa kuwa ndege ya taifa kama ilivyo huduma nyingine ni kudhibiti bei ya huduma sokoni...so bado sio poa ndege nyingine kufwariki....au zitakuwa zimebadilushwa rangi na kuipisha ATCL kuunga mkono juhudi za mheshimiwa?
 
Dar Kahama, Mwanza Kahama, Kigoma kahama....hizi route ziko poa. Precision anapiga Dar Kahama...nyie chukueni hiyo ya mwanza na kigoma mpige ela
 
...kwa sababu nimeisha safiri na Dreamliner safari 8, na hakuna hata safari moja ndege ilijaa... lakini kutokana na zile mbwembwe za mapokezi ya ndege hii, no one can dare say that!, hivyo hasara hiyo itabebwa kimya kimya kufa kizungu na tai shingoni...
Asalaam Aleykhum, Ustaadhi Paskali!!
 
Paskali inaelekea unafurahia na kushangilia endapo Fastjet watafungisha virago. Endapo hilo litatokea, na hili litakuwa jambo la kusikitisha kabisa. Kwa kuwa litakalotokea baada ya Fastjet "kufunga virago" ni kwamba ATCL itakuwa haina ushindani. Hapo ndipo watakapoweza kupandisha nauli kwa kiwango kikubwa bila kuwa na hofu ya ushindani. Kwa upande mwingine fahamu kwamba Fastjet na Precision Air zina-operate katika hali ya "unfair competition". ATCL inapata ruzuku (subsidy) ya serikali lakini private operators hawapati. Hivyo ndivyo ninavyolitazama suala hili.
Wajue tu hayo mashirika binafsi hayabebwi na kodi zetu.

Huko kimataifa hali ni tofauti kabisa na Fastjet walikuwa wana-operate katika nchi kadhaa za Afrika lakini biashara imekuwa ngumu hivyo na sisi tujiandae tunapokusudia kuruka kimataifa.

Yaani route za ndani sijui kama zitaweza kuibeba ATCL iwapo zitakuwa na unafuu ili hali kimataifa tutakuwa tunakabiliwa na ushindani.

Hata route za humu ndani ambapo ATCL iko yenyewe, mfano Dar to Dodoma; ndege bado haijai na hiyo menu yao huko ndani inaashiria kitu fulani.

Pia ni lazima tujiulize je, nauli za hizi ndege zina uhalisi na hali halisi ya kibiashara mfano nauli za Dreamliner?

Binafsi hili halinishangazi kwani nilishaliona tangu siku nyingi na nililisema kupitia huu uzi:

Hakuna abiria wa kushindanisha kwa "afya" mashirika matatu ya ndege kwa safari za ndani - JamiiForums
in
 
Wanabodi,

Japo mimi ni miongoni mwa wale tuliopinga ununuzi wa ndege kwa cash money, na serikali yetu kufanya matumizi makubwa kama haya ya manunuzi bila idhini ya Bunge, lani mimi ni mmoja wa massuporter wakubwa wa hatua mbalimbali za rais Magufuli kufufua uchumi wetu, ikiwemo kulifufua Shirika la Ndege la ATCL.

Baada ya kuwasili kwa Bombadier, nikashauri serikali yetu, tutumie political will kuinusuru ATC na ushindani usio sawia.
Je, ATCL inahujumiwa kibiashara? Tutumie a political will kuinusuru au tuiache iangamizwe na ushindani? - JamiiForums

Fast Jet nao wakapunguza sana nauli zao na kuamua kupeleka ndege zao routes zile zile za ATC kwa bei poa zaidi, kwa vile Fast Jet wanatumia JET, na ATC wanatumia pangaboi, Fast Jet aliendelea kuipiga bao ATC.

Ujio wa Dreamliner umekuja kufunga kazi. Japo siungi mkono kurusha dege kubwa kama dreamliner kwa domestic routes ambazo ni route fupi fupi, sio tuu tunaichosha bure dreamliner yetu, bali pia tunaichakaza kwa paa shuka paa shuka ndani ya muda mfupi, lakini baada ya kuipokea taarifa hii kutoka humu humu jf, African airline Fastjet reveals urgent need for more cash - JamiiForums
kiukweli sasa ndio naungana na Watanzania wengine kumpongeza rais Magufuli kwa ununuzi wa ndege hizi. Pia sasa nalipongeza shirika la Ndege la Tanzania, ATCL kulirusha hili lidude routes za ndani za Mwanza na Kilimanjaro, kwa sababu kufuatia ujio wa Dreamliner, sasa Fast Jet, inapumulia mashine, na sio tuu itasitisha huduma zake Tanzania na kufungasha rasmi, bali Fast Jet, itakufa rasmi kwasababu roho ya Fast Jet, ni biashara ya Tanzania.

Kufuatia Dreamliner ya ATCL kuruka Mwanza na Kilimanjaro, Fast Jet na Precision zimekosa abiria wa Mwanza na Kilimanjaro, hivyo sasa Fast Jet, ni soon atakubali matokeo na kunyanyua mikono yake juu, atabaki Precision, hivyo kama anataka usalama na kuendelea ku survive, asarender routes za Mwanza na Kilimanjaro kwa ATCL, yeye aende routes nyingine za mikoa mingine ambayo haina ndege kama Singida, Shinyanga, Songea etc.

Kufa kufaana, hivyo taarifa za Fast Jet kupumulia mashine ni habari njema kwa Watanzania wazalendo na ATC yetu, kwa sababu nimeisha safiri na Dreamliner safari 8, na hakunahata safari moja ndege ilijaa, hivyo nikaogopa kama ni hii, then nikajisemea kimoyo moyo kuwa hii Dreamliner inaoparate kwa hasara, lakini kutokana na zile mbwembwe za mapokezi ya ndege hii, no one can dare say that!, hivyo hasara hiyo itabebwa kimya kimya kufa kizungu na tai shingoni, hivyo kifo cha Fast Jet ni neema kwa ATC ambapo sasa dreamliner yetu itajaa.

Japo sio ustaarabu kufurahia matatizo ya mwenzako, kama kifo cha Fast Jet kwa sababu, ni Fastjet ndio walituokoa wakati ATC ilipokufa na PAA wakawa wanatukomoa!. Besides wafanyakazi ni Watanzania wenzetu, na Fast Jet, ilikuwa inafanya biashara halali na kuchangia uchumi wa taifa, hivyo tusiibeze Fastjet au kufuraia kifo chake, lakini tukubali tukatae, mgeni alineemeka wakati mwenyeji akichechemea, sasa mwenyeji kapona, inabidi mgeni arudi kwao.

Tena kwa muda mrefu Tanzania imekuwa ikifanywa ni shamba la bibi, kwa kila mtu kutoka anakotoka na kuja kujichumia na kujivunia as if Tanzania haina wenyewe, kwa vile Fastjet ni shirika la kigeni, then faida yote inapelekwa huko nje kwa wenye hisa, hivyo ATC sasa imeonyesha, kwenye usafiri wa anga, Tanzania ina wenyewe. Hivyo hata Fast Jet wakifungasha, abiria bado wataendelea kupanda ATCL, hivyo taifa kuendelea kupata mapato, na kwa vile ATC bado inaleta ndege nyingine 4, itaweza kuwameza wafanyakazi wote wa Fast Jet.

Kuna mwanajf huyu alisema jambo la maana sana hapa, Hakuna abiria wa kushindanisha kwa "afya" mashirika matatu ya ndege kwa safari za ndani - JamiiForums
Hivyo naamini PAA watajiandaa yasiwakute ya Fastjet.

Hivyo sasa ATC sio tuu itatawala soko, bali sasa ndio itarudisha heshima ya nchi, inarudisha heshima Taifa, na huu utaratibu wa kuwafungasha virago watu, uendelee kwa routes za Afrika Mashariki, tuje routes za Ghuba, India na China, kisha tufunge kazi na New York na London.

Poleni sana Fast Jet, Hongera ATCL
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza Wafanyakazi 136! - JamiiForums

Ushauri wa Bure kwa ATC: Anzisheni frequently fliers na fanyeni over booking kwa waiting list. - JamiiForums
Ndege ya ATCL yachelewa kuondoka ndani ya muda; watoa ufafanuzi! - JamiiForums

Tupunguze "kuisimanga" ATCL, haijengi zaidi ya kukatisha tamaa - JamiiForums

Zitto Zuberi Kabwe Ni Mchochezi, Akamatwe, Ashitakiwe Kwa ...
Mayalla Mayalla mada zako wakati mwingine ni kizungumkuti. Sijajua maana ya hii mada
 
Ahsante Bwana Paskali. Hivi kweli mkuu unaweza ukanunua Dreamliner kwa safari ya Dar MZ achilia Dar KIA???????
Kama ni kweli basi TZ imefanya mageuzi makubwa sana duniani katika biashara ya usafiri wa anga!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Simabwachi
Kujifanya na ujuaji.. moja kunukuu hujui.. umeishia kurundika mineno yako kwangu😀😀😀

Lingine kama hujui JF yaendaje na wengi kuficha yao bila hata kuongeza kwa chini na kuandika updated or hata pale aliongeza link baada.. wote mpo mpo tu.. kutaka tu kujionyesha mna akili huku ujuzi wa mliosomea hamna.. eeeh dongo kwako Kaka.. uwe unaandika chini kama umeupdate na muda basi kurahisisha mamboz

Hamujui vitu vidogo ndivyo vinaonyesha mukoje😉

Jione jinsi hujui kufikiria nje ta boksi..🤣🤣🤣
 
Tuko kwenye "raiti traki" naona idadi ya wanaomwelewa huyu bwana paskali inaongezeka, wasiwasi wangu ni pale uvumilivu utakapowashinda wale jamaa wanaovaa chuichui sijui nini kitamtokea ndugu yetu paskali
 
Yaleyale ya ccm kuogopa upinzani,sasa wewe unavyofurahia Fast jet kufungasha vilago unataka hao ATCL wajitawale na kufanya biashara as usually?hawachelewi hao kukanseli route na kuwapeleka wajumbe wa ccm mkutanoni
Kuna ubaya gani wajumbe wa Sekretarieti kuu wakawaishwa mkutanoni? Sisi wengine tutasubiri tu.
NB: ilani imetekelezwa kwa 89% mpaka sasa. Mtabaki na kupinga-pinga tu
 
Uliwashauri wapi na nani haswa

Naona nilipitwa

Ila kushushuka mnashushuka kwenye mengi na bado

Magufuli oyeeeeee
eh eh mama unajua kitu kinachoitwa sacarsm...naomba uwe unamsoma paskali kwa zaidi ya unachoona kwenye maandishi
 
Back
Top Bottom