ATC Sasa Yaanza Kuleta Heshima ya Nchi, Yapunguza Tanzania Kufanywa Shamba la Bibi, FastJet Yapumulia Mashine, Soon Itafungasha Virago!.

Wanabodi,

Japo mimi ni miongoni mwa wale tuliopinga ununuzi wa ndege kwa cash money, na serikali yetu kufanya matumizi makubwa kama haya ya manunuzi makubwa kwa kutumia fedha za umma bila idhini ya Bunge, kwa sababu fedha za umma zinaongozwa na sheria, taratibu na kanuni, mtu hata ukiwa nani, huwezi tuu kujichotea fedha za umma na kuzitumia kununulia chochote bila kufuata sheria, taratibu na kanuni ikiwemo idhini ya bunge, unless matumizi hayo ni ya dharura, lakini mimi ni mmoja wa massuporter wakubwa wa hatua mbalimbali zinazochukuliwa na rais Magufuli kufufua uchumi wa taifa letu, ikiwemo kulifufua Shirika la Ndege la ATCL.

Baada ya kuwasili kwa Bombadier, nikashauri serikali yetu, tutumie political will kuinusuru ATC na ushindani usio sawia.
Je, ATCL inahujumiwa kibiashara? Tutumie a political will kuinusuru au tuiache iangamizwe na ushindani? - JamiiForums

Fast Jet nao wakapunguza sana nauli zao na kuamua kupeleka ndege zao routes zile zile za ATC kwa bei poa zaidi, kwa vile Fast Jet wanatumia JET, na ATC wanatumia pangaboi, Fast Jet aliendelea kuipiga bao ATC.

Ujio wa Dreamliner umekuja kufunga kazi. Japo siungi mkono kurusha dege kubwa kama dreamliner kwa domestic routes ambazo ni route fupi fupi, sio tuu tunaichosha bure dreamliner yetu, bali pia tunaichakaza kwa paa shuka paa shuka ndani ya muda mfupi, lakini baada ya kuipokea taarifa hii kutoka humu humu jf, African airline Fastjet reveals urgent need for more cash - JamiiForums
kiukweli sasa ndio naungana na Watanzania wengine kumpongeza rais Magufuli kwa ununuzi wa ndege hizi. Pia sasa nalipongeza shirika la Ndege la Tanzania, ATCL kulirusha hili lidude routes za ndani za Mwanza na Kilimanjaro, kwa sababu kufuatia ujio wa Dreamliner, sasa Fast Jet, inapumulia mashine, na sio tuu itasitisha huduma zake Tanzania na kufungasha rasmi, bali Fast Jet, itakufa rasmi kwasababu roho ya Fast Jet, ni biashara ya Tanzania.

Kufuatia Dreamliner ya ATCL kuruka Mwanza na Kilimanjaro, Fast Jet na Precision zimekosa abiria wa Mwanza na Kilimanjaro, hivyo sasa Fast Jet, ni soon atakubali matokeo na kunyanyua mikono yake juu, atabaki Precision, hivyo kama anataka usalama na kuendelea ku survive, asarender routes za Mwanza na Kilimanjaro kwa ATCL, yeye aende routes nyingine za mikoa mingine ambayo haina ndege kama Singida, Shinyanga, Songea etc.

Kufa kufaana, hivyo taarifa za Fast Jet kupumulia mashine ni habari njema kwa Watanzania wazalendo na ATC yetu, kwa sababu nimeisha safiri na Dreamliner safari 8, na hakunahata safari moja ndege ilijaa, hivyo nikaogopa kama ni hii, then nikajisemea kimoyo moyo kuwa hii Dreamliner inaoparate kwa hasara, lakini kutokana na zile mbwembwe za mapokezi ya ndege hii, no one can dare say that!, hivyo hasara hiyo itabebwa kimya kimya kufa kizungu na tai shingoni, hivyo kifo cha Fast Jet ni neema kwa ATC ambapo sasa dreamliner yetu itajaa.

Japo sio ustaarabu kufurahia matatizo ya mwenzako, kama kifo cha Fast Jet kwa sababu, ni Fastjet ndio walituokoa wakati ATC ilipokufa na PAA wakawa wanatukomoa!. Besides wafanyakazi ni Watanzania wenzetu, na Fast Jet, ilikuwa inafanya biashara halali na kuchangia uchumi wa taifa, hivyo tusiibeze Fastjet au kufuraia kifo chake, lakini tukubali tukatae, mgeni alineemeka wakati mwenyeji akichechemea, sasa mwenyeji kapona, inabidi mgeni arudi kwao.

Tena kwa muda mrefu Tanzania imekuwa ikifanywa ni shamba la bibi, kwa kila mtu kutoka anakotoka na kuja kujichumia na kujivunia as if Tanzania haina wenyewe, kwa vile Fastjet ni shirika la kigeni, then faida yote inapelekwa huko nje kwa wenye hisa, hivyo ATC sasa imeonyesha, kwenye usafiri wa anga, Tanzania ina wenyewe. Hivyo hata Fast Jet wakifungasha, abiria bado wataendelea kupanda ATCL, hivyo taifa kuendelea kupata mapato, na kwa vile ATC bado inaleta ndege nyingine 4, itaweza kuwameza wafanyakazi wote wa Fast Jet.

Kuna mwanajf huyu alisema jambo la maana sana hapa, Hakuna abiria wa kushindanisha kwa "afya" mashirika matatu ya ndege kwa safari za ndani - JamiiForums
Hivyo naamini PAA watajiandaa yasiwakute ya Fastjet.

Hivyo sasa ATC sio tuu itatawala soko, bali sasa ndio itarudisha heshima ya nchi, inarudisha heshima Taifa, na huu utaratibu wa kuwafungasha virago watu, uendelee kwa routes za Afrika Mashariki, tuje routes za Ghuba, India na China, kisha tufunge kazi na New York na London.

Poleni sana Fast Jet, Hongera ATCL
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza Wafanyakazi 136! - JamiiForums

Ushauri wa Bure kwa ATC: Anzisheni frequently fliers na fanyeni over booking kwa waiting list. - JamiiForums
Ndege ya ATCL yachelewa kuondoka ndani ya muda; watoa ufafanuzi! - JamiiForums

Tupunguze "kuisimanga" ATCL, haijengi zaidi ya kukatisha tamaa - JamiiForums

Zitto Zuberi Kabwe Ni Mchochezi, Akamatwe, Ashitakiwe Kwa ...
Pascal Mayalla usiwachuze ndg zako wa ATCL wanapotea vibaya mnoo..
haya tuambie UZINGUZI wa safari ya mojakwamoja india unazinguliwa lini?? maana najiuliza ikifika hiyo safari yake india yakatokea yaliyotukuta hapa MWANZA wakati tunaisubiria DILIMULAINI mpaka tumebadilishiwa na kuletewa ndge ya PRECISION na flyJET ambazo wewe unaziponda lkn ATCL kujiokoa na sintofaham yao ilibidi wazitumie hizo ndege m'badala kuokoa jahazi je hali itakuwaje.. usishbikie tu kuwa na kandege kamoja hako ndo kabebe watu kwenda masafa yambali wakati hapa DAR to MZA ni majanga MTAUMBUKA ACHA WANAOJUA WAMZOMEE TU SIZONJE KWA UKURUPUKAJI WAKE. .
 
kazi iko kwa ndege za FISIEM kwanza hazina hata ushirikiano kimataifa halafu JIWE anataka ziruke mpaka india.. haya ni majanga na hu ndio mwanzo wa kuiacha huko afu watuambie iko kwenye matengenezo ya WIFI
 
Wajue tu hayo mashirika binafsi hayabebwi na kodi zetu.

Huko kimataifa hali ni tofauti kabisa na Fastjet walikuwa wana-operate katika nchi kadhaa za Afrika lakini biashara imekuwa ngumu hivyo na sisi tujiandae tunapokusudia kuruka kimataifa.

Yaani route za ndani sijui kama zitaweza kuibeba ATCL iwapo zitakuwa na unafuu ili hali kimataifa tutakuwa tunakabiliwa na ushindani.

Hata route za humu ndani ambapo ATCL iko yenyewe, mfano Dar to Dodoma; ndege bado haijai na hiyo menu yao huko ndani inaashiria kitu fulani.

Pia ni lazima tujiulize je, nauli za hizi ndege zina uhalisi na hali halisi ya kibiashara mfano nauli za Dreamliner?

Binafsi hili halinishangazi kwani nilishaliona tangu siku nyingi na nililisema kupitia huu uzi:

Hakuna abiria wa kushindanisha kwa "afya" mashirika matatu ya ndege kwa safari za ndani - JamiiForums
Nawashangaa watu kufurahia Fastjet kufungasha virago ......... tatizo watu inaelekea hawajui kuwa hii ni dalili mbaya kwa uchumi wetu.

Tatizo watanzania kila siku tunalilia wawekezaji ........ halafu wakiwekeza tunadai ni wezi. Kwa kweli HANGOVER YA UJAMAA bado inatusumbua na inaelekea itakuwa ndani ya vichwa vyetu kwa muda mrefu sana.

Hivi karibuni nimesikia South African Airways wamepunguza safari za Dar-JHB, sasa sijui hii nayo watu wataiita ni fursa kwa ATC u ni nini sijui....!!?
 
Mayalla naye naona njaa inamuuma tu tangu aitwe pale mjengoni na Ndugai amehamua kuwa muongo,mnafiki,na mtu wa kushindana na nafsi yake.
Serikali haipaswi kushindanishwa na taasisi binafsi kwa mfano ATCL na Fastjet
Pascal zungumzia Kenya Airways,Ethiopian Airways na hiyo ATCL....
Anyways hata wenzako akina Jerry Muro walijifanya kupoteza uelewa sasa hivi wameula!
Kichaa mwenzako atakusoma tu tena wewe ni Kanda pendwa ulichelewa tu
 
Mr. Zero,
Hao South Africa Airways wafute kabisa hizo route za Dar. Maana mibei yao si rafiki kwa sisi "wanyonge". Mbona Rwandair anachanja mpaka 199 usd (return) dar-jhb-dar...wakati kq=220usd yeye 400-600usd ana nn cha zaidi? Au ndo direct flight tofauti ya masaa mawili?
**ATC aanze JHB-Zanzibar-Dar
 
Mkuu Mwalla swala lako sio ATCl bali ni CCM. Sio rahisi kulielezea kitaalam swala la Mayala.

kazi iko kwa ndege za FISIEM kwanza hazina hata ushirikiano kimataifa halafu JIWE anataka ziruke mpaka india.. haya ni majanga na hu ndio mwanzo wa kuiacha huko afu watuambie iko kwenye matengenezo ya WIFI
 
Biashara ya ushindani ndio biashara ambayo inaweza kumnufaisha mwananchi wa kawaida,Mtu ukimsikia anaanza kufurahia shirika fulani au Biashara fulani inakufa inapumulia mashine kwavile kuna mtu mwengine mwenye uwezo amefungua biashara kama hizo,ujuwe huyu kapungukiwa na akili hana akili timamu..

"Monopoly" ni dhambi,inakaribisha wenye nguvu za pesa kuamua maamuzi yote ya biashara,kuanzia bei na service nyengine..Nchi ya Marekani "Monopoly" ni kesi ya jinai,kwasababu mfumo huo wa biashara unawadulumu na kuwaonea wanunuzi wa biashara husika,Ningeliishauri Serikali ukipiga tafu FastJet na mashirika mengine madogo ya biashara hiyo kwa hali na mali
 
Ujio wa Dreamliner umekuja kufunga kazi. Japo siungi mkono kurusha dege kubwa kama dreamliner kwa domestic routes

Kufuatia Dreamliner ya ATCL kuruka Mwanza na Kilimanjaro, Fast Jet na Precision zimekosa abiria wa Mwanza na Kilimanjaro, hivyo sasa Fast Jet, ni soon atakubali matokeo na kunyanyua mikono yake juu.

Mkuu Pascal sijakuelewa maana najua wewe ni mtu makini. Inakuwaje unataka tufanye conclusion kwenye kitu ambacho ni cha muda? FastJet hawezi kunyosha mikono akijua Dreamliner katika hizo route ni ya muda tu.

Labda suala la msingi ni kujadili ushindani kati ya Bombardier za ATCL na FastJet. Lakini hili la kushindanisha Dreamliner na FastJet halitakuwapo tena Dreamliner ikianza safari za nje.Au mambo yamebadilika Dreamliner haitaenda tena Mumbay?

Lakini pia ATCL wanashughulikaje na ushindani kati ya ndege zao wenyewe? Kwa mfano, baada ya Dreamliner kuwa inaenda Mwanza na KIA, Bombardier zilizokuwa zinafanya hizo safari zimeathirikaje?
 
Wanabodi,

Japo mimi ni miongoni mwa wale tuliopinga ununuzi wa ndege kwa cash money, na serikali yetu kufanya matumizi makubwa kama haya ya manunuzi makubwa kwa kutumia fedha za umma bila idhini ya Bunge, kwa sababu fedha za umma zinaongozwa na sheria, taratibu na kanuni, mtu hata ukiwa nani, huwezi tuu kujichotea fedha za umma na kuzitumia kununulia chochote bila kufuata sheria, taratibu na kanuni ikiwemo idhini ya bunge, unless matumizi hayo ni ya dharura, lakini mimi ni mmoja wa massuporter wakubwa wa hatua mbalimbali zinazochukuliwa na rais Magufuli kufufua uchumi wa taifa letu, ikiwemo kulifufua Shirika la Ndege la ATCL.

Baada ya kuwasili kwa Bombadier, nikashauri serikali yetu, tutumie political will kuinusuru ATC na ushindani usio sawia.
Je, ATCL inahujumiwa kibiashara? Tutumie a political will kuinusuru au tuiache iangamizwe na ushindani? - JamiiForums

Fast Jet nao wakapunguza sana nauli zao na kuamua kupeleka ndege zao routes zile zile za ATC kwa bei poa zaidi, kwa vile Fast Jet wanatumia JET, na ATC wanatumia pangaboi, Fast Jet aliendelea kuipiga bao ATC.

Ujio wa Dreamliner umekuja kufunga kazi. Japo siungi mkono kurusha dege kubwa kama dreamliner kwa domestic routes ambazo ni route fupi fupi, sio tuu tunaichosha bure dreamliner yetu, bali pia tunaichakaza kwa paa shuka paa shuka ndani ya muda mfupi, lakini baada ya kuipokea taarifa hii kutoka humu humu jf, African airline Fastjet reveals urgent need for more cash - JamiiForums
kiukweli sasa ndio naungana na Watanzania wengine kumpongeza rais Magufuli kwa ununuzi wa ndege hizi. Pia sasa nalipongeza shirika la Ndege la Tanzania, ATCL kulirusha hili lidude routes za ndani za Mwanza na Kilimanjaro, kwa sababu kufuatia ujio wa Dreamliner, sasa Fast Jet, inapumulia mashine, na sio tuu itasitisha huduma zake Tanzania na kufungasha rasmi, bali Fast Jet, itakufa rasmi kwasababu roho ya Fast Jet, ni biashara ya Tanzania.

Kufuatia Dreamliner ya ATCL kuruka Mwanza na Kilimanjaro, Fast Jet na Precision zimekosa abiria wa Mwanza na Kilimanjaro, hivyo sasa Fast Jet, ni soon atakubali matokeo na kunyanyua mikono yake juu, atabaki Precision, hivyo kama anataka usalama na kuendelea ku survive, asarender routes za Mwanza na Kilimanjaro kwa ATCL, yeye aende routes nyingine za mikoa mingine ambayo haina ndege kama Singida, Shinyanga, Songea etc.

Kufa kufaana, hivyo taarifa za Fast Jet kupumulia mashine ni habari njema kwa Watanzania wazalendo na ATC yetu, kwa sababu nimeisha safiri na Dreamliner safari 8, na hakunahata safari moja ndege ilijaa, hivyo nikaogopa kama ni hii, then nikajisemea kimoyo moyo kuwa hii Dreamliner inaoparate kwa hasara, lakini kutokana na zile mbwembwe za mapokezi ya ndege hii, no one can dare say that!, hivyo hasara hiyo itabebwa kimya kimya kufa kizungu na tai shingoni, hivyo kifo cha Fast Jet ni neema kwa ATC ambapo sasa dreamliner yetu itajaa.

Japo sio ustaarabu kufurahia matatizo ya mwenzako, kama kifo cha Fast Jet kwa sababu, ni Fastjet ndio walituokoa wakati ATC ilipokufa na PAA wakawa wanatukomoa!. Besides wafanyakazi ni Watanzania wenzetu, na Fast Jet, ilikuwa inafanya biashara halali na kuchangia uchumi wa taifa, hivyo tusiibeze Fastjet au kufuraia kifo chake, lakini tukubali tukatae, mgeni alineemeka wakati mwenyeji akichechemea, sasa mwenyeji kapona, inabidi mgeni arudi kwao.

Tena kwa muda mrefu Tanzania imekuwa ikifanywa ni shamba la bibi, kwa kila mtu kutoka anakotoka na kuja kujichumia na kujivunia as if Tanzania haina wenyewe, kwa vile Fastjet ni shirika la kigeni, then faida yote inapelekwa huko nje kwa wenye hisa, hivyo ATC sasa imeonyesha, kwenye usafiri wa anga, Tanzania ina wenyewe. Hivyo hata Fast Jet wakifungasha, abiria bado wataendelea kupanda ATCL, hivyo taifa kuendelea kupata mapato, na kwa vile ATC bado inaleta ndege nyingine 4, itaweza kuwameza wafanyakazi wote wa Fast Jet.

Kuna mwanajf huyu alisema jambo la maana sana hapa, Hakuna abiria wa kushindanisha kwa "afya" mashirika matatu ya ndege kwa safari za ndani - JamiiForums
Hivyo naamini PAA watajiandaa yasiwakute ya Fastjet.

Hivyo sasa ATC sio tuu itatawala soko, bali sasa ndio itarudisha heshima ya nchi, inarudisha heshima Taifa, na huu utaratibu wa kuwafungasha virago watu, uendelee kwa routes za Afrika Mashariki, tuje routes za Ghuba, India na China, kisha tufunge kazi na New York na London.

Poleni sana Fast Jet, Hongera ATCL
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza Wafanyakazi 136! - JamiiForums

Ushauri wa Bure kwa ATC: Anzisheni frequently fliers na fanyeni over booking kwa waiting list. - JamiiForums
Ndege ya ATCL yachelewa kuondoka ndani ya muda; watoa ufafanuzi! - JamiiForums

Tupunguze "kuisimanga" ATCL, haijengi zaidi ya kukatisha tamaa - JamiiForums

Zitto Zuberi Kabwe Ni Mchochezi, Akamatwe, Ashitakiwe Kwa ...
NO ONE CAN FIGHT WITH ATCL OGGA

JAMAAA WAMEGOMA KUWEKEZA FJET KUANZIA JANA
 
Si sawa kufurahia kuanguka kwa shirika hilo maana kuna watanzania watakosa kazi
Ni akili ya mwafrika chini ya jangwa la sahara ndio ana akili kama hizo za kufurahia mambo bila ya kuangalia "consequences" bila kufikiria nini kitawakuta wafanyajazi,vipi kuhusu ukusanyaji wa Kodi .......nk..

"Only in Sub Sahara African Countries" tuna safari refu sana mpaka tuwafikie wengine
 
IMG-20180927-WA0013.jpg
 
Back
Top Bottom