ATC Sasa Yaanza Kuleta Heshima ya Nchi, Yapunguza Tanzania Kufanywa Shamba la Bibi, FastJet Yapumulia Mashine, Soon Itafungasha Virago!.

ATC Sasa Yaanza Kuleta Heshima ya Nchi, Yapunguza Tanzania Kufanywa Shamba la Bibi, FastJet Yapumulia Mashine, Soon Itafungasha Virago!.

Wanabodi,

Japo mimi ni miongoni mwa wale tuliopinga ununuzi wa ndege kwa cash money, na serikali yetu kufanya matumizi makubwa kama haya ya manunuzi bila idhini ya Bunge, lani mimi ni mmoja wa massuporter wakubwa wa hatua mbalimbali za rais Magufuli kufufua uchumi wetu, ikiwemo kulifufua Shirika la Ndege la ATCL.

Baada ya kuwasili kwa Bombadier, nikashauri serikali yetu, tutumie political will kuinusuru ATC na ushindani usio sawia.
Je, ATCL inahujumiwa kibiashara? Tutumie a political will kuinusuru au tuiache iangamizwe na ushindani? - JamiiForums

Fast Jet nao wakapunguza sana nauli zao na kuamua kupeleka ndege zao routes zile zile za ATC kwa bei poa zaidi, kwa vile Fast Jet wanatumia JET, na ATC wanatumia pangaboi, Fast Jet aliendelea kuipiga bao ATC.

Ujio wa Dreamliner umekuja kufunga kazi. Japo siungi mkono kurusha dege kubwa kama dreamliner kwa domestic routes ambazo ni route fupi fupi, sio tuu tunaichosha bure dreamliner yetu, bali pia tunaichakaza kwa paa shuka paa shuka ndani ya muda mfupi, lakini baada ya kuipokea taarifa hii kutoka humu humu jf, African airline Fastjet reveals urgent need for more cash - JamiiForums
kiukweli sasa ndio naungana na Watanzania wengine kumpongeza rais Magufuli kwa ununuzi wa ndege hizi. Pia sasa nalipongeza shirika la Ndege la Tanzania, ATCL kulirusha hili lidude routes za ndani za Mwanza na Kilimanjaro, kwa sababu kufuatia ujio wa Dreamliner, sasa Fast Jet, inapumulia mashine, na sio tuu itasitisha huduma zake Tanzania na kufungasha rasmi, bali Fast Jet, itakufa rasmi kwasababu roho ya Fast Jet, ni biashara ya Tanzania.

Kufuatia Dreamliner ya ATCL kuruka Mwanza na Kilimanjaro, Fast Jet na Precision zimekosa abiria wa Mwanza na Kilimanjaro, hivyo sasa Fast Jet, ni soon atakubali matokeo na kunyanyua mikono yake juu, atabaki Precision, hivyo kama anataka usalama na kuendelea ku survive, asarender routes za Mwanza na Kilimanjaro kwa ATCL, yeye aende routes nyingine za mikoa mingine ambayo haina ndege kama Singida, Shinyanga, Songea etc.

Kufa kufaana, hivyo taarifa za Fast Jet kupumulia mashine ni habari njema kwa Watanzania wazalendo na ATC yetu, kwa sababu nimeisha safiri na Dreamliner safari 8, na hakunahata safari moja ndege ilijaa, hivyo nikaogopa kama ni hii, then nikajisemea kimoyo moyo kuwa hii Dreamliner inaoparate kwa hasara, lakini kutokana na zile mbwembwe za mapokezi ya ndege hii, no one can dare say that!, hivyo hasara hiyo itabebwa kimya kimya kufa kizungu na tai shingoni, hivyo kifo cha Fast Jet ni neema kwa ATC ambapo sasa dreamliner yetu itajaa.

Japo sio ustaarabu kufurahia matatizo ya mwenzako, kama kifo cha Fast Jet kwa sababu, wafanyakazi ni Watanzania wenzetu, na Fast Jet, ilikuwa inafanya biashara halali na kuchangia uchumi wa taifa, lakini kwa muda mrefu Tanzania imekuwa ikifanywa ni shamba la bibi, kwa kila mtu kujichumia na kujivunia as if Tanzania haina wenyewe, kwa vile Fastjet ni shirika la kigeni, then faida yote inapelekwa huko nje kwa wenye hisa, hivyo ATC sasa imeonyesha, kwenye usafiri wa anga, Tanzania ina wenyewe. Hivyo hata Fast Jet wakifungasha, abiria bado wataendelea kupanda ATCL, hivyo taifa kuendelea kupata mapato, na kwa vile ATC bado inaleta ndege nyingine 4, itaweza kuwameza wafanyakazi wote wa Fast Jet.

Hivyo sasa ATC sio tuu itatawala soko, bali sasa ndio itarudisha heshima ya nchi, inarudisha heshima Taifa, na huu utaratibu wa kuwafungasha virago watu, uendelee kwa routes za Afrika Mashariki, tuje routes za Ghuba, India na China, kisha tufunge kazi na New York na London.

Poleni sana Fast Jet, Hongera ATCL
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza Wafanyakazi 136! - JamiiForums

Ushauri wa Bure Kwa ATC Fanyeni Over Booking name Kuweka Waiting List. - JamiiForums

Ndege ya ATCL yachelewa kuondoka ndani ya muda; watoa ufafanuzi! - JamiiForums

Tupunguze "kuisimanga" ATCL, haijengi zaidi ya kukatisha tamaa - JamiiForums

Zitto Zuberi Kabwe Ni Mchochezi, Akamatwe, Ashitakiwe Kwa ...
Paskali hebu tuambie wamiliki wa Fast Jet ni kina nani. Inawezekana wakawa ni hao wawekezaji tu bila kuwa na wenyeji kama ilivyo desturi yetu?
 
Mkuu, Kuna mada ni heri kukaa kimya kuliko kuchangia halafu ukaleta maneno
kama upo kwenye vijiwe vya kusukana. Kuna vitu siyo vya kuingiza UKADA hivi
unapomtathimini Pascal Mayala unaweza kusema yupo CHADEMA au CCM
Punguza mapenzi yasio na maana eti "Kushushuka"


hata kwenye kusukana hua tunaongea kwa kusikilizana... hyo mwezi ushaisha..dawa zi namhusu!
 
Sifurahii mashirika mengine kufa, lakini natapata furaha sana kuona shirika la ndege Tanzania linakuwa chaguo namba moja kwa watanzania na wasio watanzania...
Humu ndani tunaweza kutumia political will tangu kwenye kupanga nauli ili mradi tu mashirika mengine yasiyotegemea kodi za wananchi yajitoe.Lakini je, kimataifa hali itakuwa hivyo hivyo?

Una uhakika biashara ya humu ndani ndio itafidia loss ya kuruka kimataifa?

Ni lazima kwanza tujiulize ni kwanini mashirika mengi, baadhi yakiwa makongwe kabisa, yanatangaza hasara wakiwemo hawa Fastjet ambao nao sasa wametoa taarifa kuwa hali ni ngumu kabla ya sisi kuanza kujipa matumaini ambayo pengine ni matumaini hewa au ni ya muda mfupi tu.

Vile vile umaliziaji wa Pascal kwenye hii mada umeutafakari vizuri au kwasababu kaanza kwa kumwaga sifa nyingi basi unaona kila kitu kitakuwa rahisi rahisi tu?
 
Humu ndani tunaweza kutumia political will tangu kwenye kupanga nauli ili mradi tu mashirika mengine yasiyotegemea kodi za wananchi yajitoe.Lakini je, kimataifa hali itakuwa hivyo hivyo?

Una uhakika biashara ya humu ndani ndio itafidia loss ya kuruka kimataifa?

Umaliziaji wa Pascal kwenye hii mada umeutafakari vizuri au kwasababu kaanza kwa kumwaga sifa basi unaona kila kitu kitakuwa rahisi rahisi tu?
Mkuu nimesema "nitafurahi ".... Namaanisha siku ikiweza kuwa chaguo namba moja kwa watanzania na walio nje ya Tanzania nitafurahi... Naamini utafurahi pia
 
Back
Top Bottom