Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Salaam,
Shirika la ndege Tanzania, ATCL watolea ufafanuzi kuhusu hali ya tairi ya ndege iliyosambaa Katika Mitandao ya Kijamii ambayo inaonesha tairi iliyoisha.
ATCL inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na habari iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu hali ya matairi ya ndege zake. Tarehe 23 Aprili , 2022 katika mitandao mbalimbali ya kijamii zilisambaa picha zikionesha hali ya matairi ya ndege aina ya Dash 8 0400 ambayo ilikuwa inadaiwa kuwa hali yake inahatarisha usalama wa ndege na abiria .
ATCL inamshukuru kwa dhati abiria huyu kwa kuonesha umakini kwa usalama wa abiria na ndege. Umakini wake umesababisha kutolewa kwa ufafanuzi juu ya matumizi ya matairi ya ndege na usalama wake ambao utafafanua hali halisi na utawaondolea hofu abiria na wadau wote.
ATCL inapenda kutoa ufafanuzi kwa umma kuhusiana na madai hayo kama ifutavyo: Katika kuhakikisha usalama abiria na ndege yenyewe , ATCL hufanya ukaguzi wa lazima wa ndege zake zote katika maeneo yote ya ndege yakiwemo matairi kama ifutavyo:
Ukaguzi wa ndege baada ya safari zote za siku (Daily Check) ;
Ukaguzi wa ndege kabla ya kuanza safari zake za siku (Departure Check) ; na
Ukaguzi wa ndege baada ya kila safari (Transit Check).
Kuhusiana na madai yaliyotolewa kuhusu hali ya matairi, ATCL inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:
1. Miongozo ya ufuatiliaji wa hali ya matairi na ubadilishaji wake hutolewa na waundaji wa ndege husika. Ndege iliyofanya safari namba TC106 aina ya Dash 8 0400 kati ya Dar es salaam na Mbeya siku ya tarehe 22 Aprili, 2022 maelekezo na miongozo yake yametolewa na Kampuni ya De Havilland. Maelekezo na miongozo hiyo inabainisha kwamba, uchunguzi wa hali ya matairi utafanyika kila siku iii kubaini kama tabaka la juu limelika na kufikia nyuzi (reinforcement cord) kuonekana . Baada ya nyuzi hizo kuonekana kwa mara ya kwanza, miongozo inaagiza tairi hilo kutumika kwa miruko isiyozidi minane (08) kabla ya kubadilishwa (rejea kiambatisho cha muongozo kutoka kwa waundaji);
Kwa kufuata miongozo hiyo, ATCL hurekodi taarifa za miruko kwa tairi hilo tangu lilipo bainika kulika kwa mara ya kwanza;
Kwa mujibu wa rekodi zilizowekwa na ATCL, tairi ya ndege tajwa lilikuwa na mruko mmoja (01) tangu kubainika kulika kwa tabaka la kwanza, hivyo kulikuwa na miruko saba (07) zaidi hadi kufikia ukomo wa matumizi yake kwa mujibu wa miongozo ya matumizi ya matairi;
Kwa msingi huo, tairi hilo lilikuwa bado ni salama kutumika kwa mujibu wa miongozo iliyowekwa na waundaji na kufuatwa na ATCL.
Kutokana na miongozo hiyo, hali ya tairi kuwa katika hali hatarishi haiwezi kubainika kwa kuangalia kulika kwa tabaka la juu la tairi bila kurejea kumbukumbu za matumizi ya tairi kufuatana na miongozo ya utumiaji.
Kwa maelezo haya, ATCL inapenda kuutoa wasiwasi umma wa watanzania na abiria wote kwa ujumla kwamba ndege zetu zipo salama kabisa na kwamba suala la usalama wa abiria na ndege kwetu ni namba moja. Hivyo, tunaomba wateja wetu waendelee kutumia ndege za ATCL kwa safari zao bila hofu.

UFAFANUZI KUHUSU HALI YA TAIRI LA NDEGE YA KAMPUNI YA NDEGE TANZANIA (ATCL) ILIYOSAMBAA KATIKA MITANDAO YA JAMii