ATCL watolea ufafanuzi kuhusu hali ya tairi la ndege iliyosambaa Katika Mitandao ya Kijamii

ATCL watolea ufafanuzi kuhusu hali ya tairi la ndege iliyosambaa Katika Mitandao ya Kijamii

Hiyo ndege TC106 a.k.a KITULO, karibia kila siku inaenda Mbeya, me nilipanda tarehe 19 kwenda Mbeya na tairi lilikuwa kipara hivyo hivyo nadhani wamefunika kombe tu mwanaharamu apite maana hiyo miruko 8 wanayodai itakuwa imeshapita na kiukweli linatakiwa kubadilishwa kabisa.
Hapa tunaomba wajibu hii fact. Ina maana toka tar 19 Hadi tar 23 ndege imefanya mruko mmoja tuu? Na mdau unasema tairi lilikuwa hivyo hivyo. Sasa maana yake kipara kipo kabla ya tar 19.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Wamejibu vizuri hasa hapa kwa kumshukuru aliyetoa taarifa😀😀

Baada ya kushukuru hapo huko kwengine wamepuyanga.Hasa hapa walipoona kutueleza sisi walipa kodi bila ushahidi kuwa tairi lile lina mruko mmoja?

Kwa akili zao wataanza kuwaambia watu kuzima simu...kama watu flani pale Kigongo-Busisi.
 
Hapa tunaomba wajibu hii fact. Ina maana toka tar 19 Hadi tar 23 ndege imefanya mruko mmoja tuu? Na mdau unasema tairi lilikuwa hivyo hivyo. Sasa maana yake kipara kipo kabla ya tar 19.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Hata mimi nimejiuliza.Tunamshukuru sana Member mwenzetu kulitupia hilo.
 
Picha ya tairi tafadhali.
Pitia huu uzi hapo chini:-
 
Kwa kulika kule, sio kwamba ndo imebainika, ile ni muda mrefu tu.
Badilisheni tyres. Vipara mtuachie wenye corolla
... tena kwa matumizi ya taxi bubu mjini au kubebea majani ya mifugo!
 
Salaam,

Shirika la ndege Tanzania, ATCL watolea ufafanuzi kuhusu hali ya tairi ya ndege iliyosambaa Katika Mitandao ya Kijamii ambayo inaonesha tairi iliyoisha.

UFAFANUZI KUHUSU HALI YA TAIRI LA NDEGE YA KAMPUNI YA NDEGE TANZANIA (ATCL) ILIYOSAMBAA KATIKA MITANDAO YA JAMii


ATCL inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na habari iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu hali ya matairi ya ndege zake. Tarehe 23 Aprili , 2022 katika mitandao mbalimbali ya kijamii zilisambaa picha zikionesha hali ya matairi ya ndege aina ya Dash 8 0400 ambayo ilikuwa inadaiwa kuwa hali yake inahatarisha usalama wa ndege na abiria .

ATCL inamshukuru kwa dhati abiria huyu kwa kuonesha umakini kwa usalama wa abiria na ndege. Umakini wake umesababisha kutolewa kwa ufafanuzi juu ya matumizi ya matairi ya ndege na usalama wake ambao utafafanua hali halisi na utawaondolea hofu abiria na wadau wote.

ATCL inapenda kutoa ufafanuzi kwa umma kuhusiana na madai hayo kama ifutavyo: Katika kuhakikisha usalama abiria na ndege yenyewe , ATCL hufanya ukaguzi wa lazima wa ndege zake zote katika maeneo yote ya ndege yakiwemo matairi kama ifutavyo:

Ukaguzi wa ndege baada ya safari zote za siku (Daily Check) ;

Ukaguzi wa ndege kabla ya kuanza safari zake za siku (Departure Check) ; na

Ukaguzi wa ndege baada ya kila safari (Transit Check).

Kuhusiana na madai yaliyotolewa kuhusu hali ya matairi, ATCL inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

1. Miongozo ya ufuatiliaji wa hali ya matairi na ubadilishaji wake hutolewa na waundaji wa ndege husika. Ndege iliyofanya safari namba TC106 aina ya Dash 8 0400 kati ya Dar es salaam na Mbeya siku ya tarehe 22 Aprili, 2022 maelekezo na miongozo yake yametolewa na Kampuni ya De Havilland. Maelekezo na miongozo hiyo inabainisha kwamba, uchunguzi wa hali ya matairi utafanyika kila siku iii kubaini kama tabaka la juu limelika na kufikia nyuzi (reinforcement cord) kuonekana . Baada ya nyuzi hizo kuonekana kwa mara ya kwanza, miongozo inaagiza tairi hilo kutumika kwa miruko isiyozidi minane (08) kabla ya kubadilishwa (rejea kiambatisho cha muongozo kutoka kwa waundaji);

Kwa kufuata miongozo hiyo, ATCL hurekodi taarifa za miruko kwa tairi hilo tangu lilipo bainika kulika kwa mara ya kwanza;

Kwa mujibu wa rekodi zilizowekwa na ATCL, tairi ya ndege tajwa lilikuwa na mruko mmoja (01) tangu kubainika kulika kwa tabaka la kwanza, hivyo kulikuwa na miruko saba (07) zaidi hadi kufikia ukomo wa matumizi yake kwa mujibu wa miongozo ya matumizi ya matairi;

Kwa msingi huo, tairi hilo lilikuwa bado ni salama kutumika kwa mujibu wa miongozo iliyowekwa na waundaji na kufuatwa na ATCL.

Kutokana na miongozo hiyo, hali ya tairi kuwa katika hali hatarishi haiwezi kubainika kwa kuangalia kulika kwa tabaka la juu la tairi bila kurejea kumbukumbu za matumizi ya tairi kufuatana na miongozo ya utumiaji.

Kwa maelezo haya, ATCL inapenda kuutoa wasiwasi umma wa watanzania na abiria wote kwa ujumla kwamba ndege zetu zipo salama kabisa na kwamba suala la usalama wa abiria na ndege kwetu ni namba moja. Hivyo, tunaomba wateja wetu waendelee kutumia ndege za ATCL kwa safari zao bila hofu.

Msemaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania.​


View attachment 2200136View attachment 2200137View attachment 2200138View attachment 2200139
Duh, yani ndege inaruka na tairi kipara kwa mujibu wa miongozo ya watenngenezaji!!! Maajabu ya Dunia hayo
 
Kwa wale ambao hamkubahatika kuona hio tairi kipara
IMG_2624.jpg

IMG_2625.jpg
 
Hapa ndio leo nimegundua kuwa hatuna vyombo vinavyoshugulikia .
Ile picha ilipigwa na abiria akiwa anaenda safari yake.
Je wanahakikishaje ulikuwa mruko wa kwa kwanza. Yaani wanasema kabla ya huo mruko haikuwa kipara, means asubuhi au jana yake haikuwa kipara?
Yaani ilipotaka kuruka ikiwa kipara . Then waka count one.
Nonsense
 
Majibu yao yanashangaza sana
Hili swali fikirishi, yaani tayari tairi limeshaonekana kwa macho limeisha , wao wanasema maximum bado.!
Ndege inapotua Kuna ule mguso wa kwanza wa tairi kwenye njia yake, huwa unasugua Sana lami, Sasa kama viwanja vyetu lami Ina makoko bado tunataka tufike maximum kwa lazima hiyo ni hatari.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Hii nchi hajawahi kuwa serious, yaan unafiki kila kona. Gurudumu ni kipara, suluhisho ni kubadilisha na sio kuja propaganda kama hizo, hakuna gari ya kiongozi ina Gurudumu kipara kwenye ndege wanaona ni sawa tu. ATCL kuwen serious basi badililisheni hilo tyre wote tunajua huo n mruko wa 800
 
Ile tairi inaonekana imesharuka miezi hata mitatu maana imekua kipara sana
Walikua wanamwambia dereva ibembeleze bembeleze hivyo hivyo maana wanajua wa Tz na Kama ng'ombe hata wakifa wao wataitisha kamati ya uchunguzi wale posho alaf badae inaishia hewan maana wana ile kauli yao ya "wa TZ wataongea lakin watazoea"
Aisee unaongea maneno makali sana mkuu,yanachoma mpaka kumoyo, na kweli viongozi ndio wanavyotuchukulia,embu ona huyu msemaji wa ATCL amekuja na majibu mepesi kwa maswali magumu
 
Wamejibu vizuri hasa hapa kwa kumshukuru aliyetoa taarifa😀😀

Baada ya kushukuru hapo huko kwengine wamepuyanga.Hasa hapa walipoona kutueleza sisi walipa kodi bila ushahidi kuwa tairi lile lina mruko mmoja?

Kwa akili zao wataanza kuwaambia watu kuzima simu...kama watu flani pale Kigongo-Busisi.
Kifuatacho ITV ndio hicho,switch your phone off,kazi kwao wapanda ndege
 
Hakuna traffic wa kuwakagua vipara ndiyo maana...
 
Acheni ukanjanja. Badilisheni hilo tairi. Msilete U-miky mouse hewani. Mchubuko umevuka hata hizo nyuzi.
Accept responsibility and change the tyre immediately before the unknown happens.
 
Back
Top Bottom