ATCL watolea ufafanuzi kuhusu hali ya tairi la ndege iliyosambaa Katika Mitandao ya Kijamii

ATCL watolea ufafanuzi kuhusu hali ya tairi la ndege iliyosambaa Katika Mitandao ya Kijamii

Taili liwe la ndege,gari au baskeli, kashata zake zinapofutika na kubaki kipara ni LAZIMA libadirishwe !! Huu utetezi wa kitoto haukubaliki kokote na nina hakika hata Bombardier wenyewe watawashangaa Air Tanzania kwa kutetea uzembe na kuhatarisha maisha ya abiria. Huu utetezi fyongo haukubaliki kabisa.... bora wangekiri tu kuwa hawana pesa za kununua taili jipya.
 
Unajua kwa hapa TZ ukiwa na cheo kidogo unaweza badili maji ukasema divai na watu wakaamini tqiri inaonekqna kabisa ina kipara Leo hii unadangqnya uma kwakusema haina shida .....seriously... kama ile tairi nliyona na kipara chake basi hata tairi za daladala ambazo traffic anasema ni kipara zina qfadhqli mara 100
 
Picha ya tairi tafadhali.

Mkuu, Piçha hizi hapaView attachment 2200335
JamiiForums-1472571806.jpg
 
Hilo swali hata mimi nimejiuliza... ingetakiwa tairi libadirishwe haraka sana kabla ya nyunzi kuonekana kuliko kusingizia manufactures guidance.
Hawa umbwa bwana yaani tairi limekwisha wao wanasubiri manufacturer guidance
 
Ni nani anasimamia kwa Karibu kuhakikisha hayo yote yanafanyika kila siku kwa ufanisi?

Uhai wa watu ni muhimu kuliko maelezo jamani
 
Badilisheni tyre bana, ndege hazina blah blah kama daladala
 
Hawa wanahatarisha maisha ya wasafiri ili waendelee kupata fedha zaidi. Tairi linaonekana lipo kipara lakini kwa vile watengenezaji walisema basi wanashindwa kuchukua hatua. Siku zote tunaambiwa akili za hao mbayuwayu changanya na zako lakini hatusikii hadi yatukute. Je, wajua kiwango cha njia ya kurukua ndege huko kwao kikoje ukilinganisha na hiki cha kwetu?

20220424_192046.jpg


DSC_0437.JPG
 
Salaam,

Shirika la ndege Tanzania, ATCL watolea ufafanuzi kuhusu hali ya tairi ya ndege iliyosambaa Katika Mitandao ya Kijamii ambayo inaonesha tairi iliyoisha.

UFAFANUZI KUHUSU HALI YA TAIRI LA NDEGE YA KAMPUNI YA NDEGE TANZANIA (ATCL) ILIYOSAMBAA KATIKA MITANDAO YA JAMii


ATCL inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na habari iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu hali ya matairi ya ndege zake. Tarehe 23 Aprili , 2022 katika mitandao mbalimbali ya kijamii zilisambaa picha zikionesha hali ya matairi ya ndege aina ya Dash 8 0400 ambayo ilikuwa inadaiwa kuwa hali yake inahatarisha usalama wa ndege na abiria .

ATCL inamshukuru kwa dhati abiria huyu kwa kuonesha umakini kwa usalama wa abiria na ndege. Umakini wake umesababisha kutolewa kwa ufafanuzi juu ya matumizi ya matairi ya ndege na usalama wake ambao utafafanua hali halisi na utawaondolea hofu abiria na wadau wote.

ATCL inapenda kutoa ufafanuzi kwa umma kuhusiana na madai hayo kama ifutavyo: Katika kuhakikisha usalama abiria na ndege yenyewe , ATCL hufanya ukaguzi wa lazima wa ndege zake zote katika maeneo yote ya ndege yakiwemo matairi kama ifutavyo:

Ukaguzi wa ndege baada ya safari zote za siku (Daily Check) ;

Ukaguzi wa ndege kabla ya kuanza safari zake za siku (Departure Check) ; na

Ukaguzi wa ndege baada ya kila safari (Transit Check).

Kuhusiana na madai yaliyotolewa kuhusu hali ya matairi, ATCL inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

1. Miongozo ya ufuatiliaji wa hali ya matairi na ubadilishaji wake hutolewa na waundaji wa ndege husika. Ndege iliyofanya safari namba TC106 aina ya Dash 8 0400 kati ya Dar es salaam na Mbeya siku ya tarehe 22 Aprili, 2022 maelekezo na miongozo yake yametolewa na Kampuni ya De Havilland. Maelekezo na miongozo hiyo inabainisha kwamba, uchunguzi wa hali ya matairi utafanyika kila siku iii kubaini kama tabaka la juu limelika na kufikia nyuzi (reinforcement cord) kuonekana . Baada ya nyuzi hizo kuonekana kwa mara ya kwanza, miongozo inaagiza tairi hilo kutumika kwa miruko isiyozidi minane (08) kabla ya kubadilishwa (rejea kiambatisho cha muongozo kutoka kwa waundaji);

Kwa kufuata miongozo hiyo, ATCL hurekodi taarifa za miruko kwa tairi hilo tangu lilipo bainika kulika kwa mara ya kwanza;

Kwa mujibu wa rekodi zilizowekwa na ATCL, tairi ya ndege tajwa lilikuwa na mruko mmoja (01) tangu kubainika kulika kwa tabaka la kwanza, hivyo kulikuwa na miruko saba (07) zaidi hadi kufikia ukomo wa matumizi yake kwa mujibu wa miongozo ya matumizi ya matairi;

Kwa msingi huo, tairi hilo lilikuwa bado ni salama kutumika kwa mujibu wa miongozo iliyowekwa na waundaji na kufuatwa na ATCL.

Kutokana na miongozo hiyo, hali ya tairi kuwa katika hali hatarishi haiwezi kubainika kwa kuangalia kulika kwa tabaka la juu la tairi bila kurejea kumbukumbu za matumizi ya tairi kufuatana na miongozo ya utumiaji.

Kwa maelezo haya, ATCL inapenda kuutoa wasiwasi umma wa watanzania na abiria wote kwa ujumla kwamba ndege zetu zipo salama kabisa na kwamba suala la usalama wa abiria na ndege kwetu ni namba moja. Hivyo, tunaomba wateja wetu waendelee kutumia ndege za ATCL kwa safari zao bila hofu.

Msemaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania.​


View attachment 2200136View attachment 2200137View attachment 2200138View attachment 2200139
Focus ni miongozo au Hali Halisi iliyopo, Leo wanakwambia ulikuwa mruko wa kwanza, jaman huu si uongo mkubwa Kabsa.. tunakuaminije?? Mnapokosea kubalin na kurekebisha tatizo, mnasubir miruko 7, hya abiria Kazi kwenu
 
Ingekuwa enzi zetu Melo angekuwa anayea ndoo Keko hadi amlete Member aliyedukua magurudumu ya muundombinu was kitaifa

Dunia inakwenda kasi sana.
 
Sawa, wabadilishe tairi basi, wasisubiri matatizo yatokee ndio waunde timu ya uchunguzi.
 
Kwa maelezo hayo,means hilo tairi ni bado jipya,litatumika mpaka lifike michubuko 8!
 
Back
Top Bottom