Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 18,875
- 29,427
DODOMA — Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) inakabiliwa na changamoto kubwa baada ya ndege nne za Airbus A220 kutokutumiwa kwa siku 279 hadi 721 kutokana na matatizo ya kiufundi na upatikanaji wa vipuri.
Pia, ndege aina ya DASH 8 Q300 haijatumika kwa zaidi ya miaka saba licha ya kugharimu zaidi ya bilioni 20 kwa matengenezo.
Kwa miaka sita mfululizo, ATCL imeshindwa kulipa tozo za ukodishaji wa ndege, na sasa inadaiwa shilingi bilioni 369.13 na Wakala wa Ndege wa Serikali.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amependekeza hatua za haraka za kukabiliana na changamoto hizi kwa kufanya mapitio ya mikataba, tathmini ya aina ya ndege, na mpango wa urejeshaji wa madeni.
Zaidi tembelea //habarileo.co.tz
Maoni yangu:-
Tatizo walianza kununua ndege ndipo wakaandika business plan (mpango kazi).