ATCL yadaiwa Tsh 369 Bilioni wakati ndege zimeegeshwa miaka 7 bila kuruka

20250417_124845.jpg

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ameeleza kuwa hadi kufikia Juni 30, 2024, Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) inadaiwa jumla ya Shilingi bilioni 595, ambapo kati ya hizo, Shilingi bilioni 369.13 ni madai kutoka taasisi za Serikali.

Ripoti hiyo ya CAG kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imebainisha kuwa fedha hizo zinahusiana moja kwa moja na malipo ya ukodishaji wa ndege kutoka Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), kupitia masharti nafuu yaliyowekwa kwenye mikataba ya ukodishaji.

Hata hivyo, ucheleweshaji wa ulipaji wa madeni hayo umetajwa kuchangiwa na mapato hafifu ya kampuni kutoka vyanzo vya ndani, pamoja na changamoto katika usimamizi wa mkataba wa ukodishaji. Aidha, ripoti imeeleza kuwa Kampuni ya Ndege Tanzania imeshindwa kulipa kodi na tozo za akiba ya matengenezo ya ndege kwa kipindi cha miaka sita mfululizo, hali iliyosababisha deni hilo kuongezeka kutoka Shilingi bilioni 27.89 mnamo Juni 30, 2018, hadi kufikia Shilingi bilioni 369.13 mwaka 2024.

CAG ameonya kuwa kiasi hicho kinatokana na gharama kubwa za uendeshaji na matengenezo ya ndege, pamoja na hasara ya kifedha ambayo kampuni hiyo imekuwa ikiipata kwa miaka sita mfululizo. Hali hiyo imeongeza mzigo wa kifedha kwa Shirika, hali inayohatarisha ustawi wake wa muda mrefu.

Katika mapendekezo yake, CAG ameshauri ATCL na Wakala wa Ndege wa Serikali kukaa pamoja na kukubaliana mpango wa malipo wa kodi na tozo hizo. Mpango huo unapendekezwa kujumuisha urekebishaji wa deni, kuongeza muda wa ulipaji, na kupunguza kiwango cha tozo za kila mwezi ili kuwezesha kampuni hiyo kumudu mzigo wa madeni na kujiendesha kwa ufanisi zaidi.

Source: Jambo Online
 
Ushawasikiliza uelewa wa mawaziri wenu wengi vijana.

Aargh, like which institution teaches the nonsense that comes out of their mouth. Hawana uwezo hata chembe.

Let it go
Aliyenunua ndege alinunua bila mipango, ila alinunua ili kuwaziba midomo wapinzani. Na mlikuwa mnamuona ana akili kwelikweli. Toka awali manunuzi ya hizo ndege yalipigiwa kelele kuwa ni wizi, na ilikuwa mwiko kuandika ukweli ufike kwa umma.
 
Na kuzitumia ndege kama mali binafsi (private jets) bila kujali hasara kwa vile hakuna wa kuhoji wala kujali.

Ethiopian Airlines wana fleet ya ndege mpya za kisasa zaidi ya 150 na wanazidi kuleta mpya na kuondoa za zamani kila wakati bila kutumia hela nyingi bali kwa biashara iliyochangamka sana.

Wanabadilisha fleet kila wakati kutegemeana na biashara inavyoenda. Wana mikataba na mabenki makubwa na makampuni ya ndege (Boeing & Airbus) inayowapa unafuu sana wa kupanga fleet yao kulingana na mahitaji ya business plan yao. Wanaingia mikataba na nchi mbalimbali za Afrika kutumia route zao za kimataifa (traffic rights) na kupanua business plan yao. Hapa kwentu wanahudumia JNIA, KIA na Zanzibar kila siku na kuleta idadi kubwa ya watalii.

Tanzania haya ni mambo ambayo yamepuuzwa na wahusika na hayawezi kueleweka kabisa kwa wananchi waliojaa ushabiki wa kisiasa. Tunazidi kupata aibu ya watu kujazana viwanjani eti kupokea ndege mpya ambazo matumizi yake hayaeleweki. Ethiopia ndege mpya zinapokelewa na watendaji wa shirika. Wizara husika na ikulu wanapewa taarifa rasmi basi. Wananchi wanafahamishwa na vyombo vya habari na press releases za shirika.
CEO wa ATCL ni Peter Ulanga. Hivi unategemea nini kwa mtu ambaye alitoka TTCL ?? Hana jipya la kuibadilisha ATCL.

Nafasu zenyewe wanapeana tu wala hazitangazwi kushindanisha ili kumpata CEO wa ukweli
 
Hilishitik lingeendeshwa kwa PPP , gov imefeli kabisa operashion za hili shirika
Wataendesha vingapi kwa PPP? Wako kwenye madaraka ili kufanya nini? Kitu ambacho wataacha kuendesha kwa PPP au kumpa mwekezaji ni madaraka yao tu! Hawa wanatakiwa kuondolewa kwa namna yoyote.
 
PPP ndiyo modern solutions kwa kuborehsa public institutions. Hata ukiwatoa hawa kwenye madaraka mkaja nyinyi CHADEMA mtafeli hivyo hivyo kwa kuwa mtawatumia Watanzania hawahawa wanaotumiwa na CCM
 
Wavivu wa CCM kazini bongo zao kisoda. 1. Kila anayeonyesha CCM ilivyoishiwa ni CHADEMA anayetaka kuingia madarakani 2. Serikali haiwezi kufanya chochote bila msaada. Pumbavu! Hizi nchi za hii dunia chungu nzima zilizoendelea kwa viongozi wake kuwajibika walipata misaada kutoka wapi? Akili fupi kama za rais wako.
 
Nenda ukanye pumba ulizokula baada ya kuvuta bangi
 
Pumba anakunya yule mjinga aliyemwambia mama mjamzito arudi nyumbani mumewe akamzalishe. Pumba anakunya yule mjinga aliyesema kuna chama kinaingiza ebola nchini. Pumba anakunya yule mjinga aliyesema katiba ni kijitabu tu. Pumba anakunya yule mjinga aliyewaambia wanaolalamika ukosefu wa ajira waende VETA.
 
Nenda VETA
 
View attachment 3306981

DODOMA — Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) inakabiliwa na changamoto kubwa baada ya ndege nne za Airbus A220 kutokutumiwa kwa siku 279 hadi 721 kutokana na matatizo ya kiufundi na upatikanaji wa vipuri.

Pia, ndege aina ya DASH 8 Q300 haijatumika kwa zaidi ya miaka saba licha ya kugharimu zaidi ya bilioni 20 kwa matengenezo.

Kwa miaka sita mfululizo, ATCL imeshindwa kulipa tozo za ukodishaji wa ndege, na sasa inadaiwa shilingi bilioni 369.13 na Wakala wa Ndege wa Serikali.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amependekeza hatua za haraka za kukabiliana na changamoto hizi kwa kufanya mapitio ya mikataba, tathmini ya aina ya ndege, na mpango wa urejeshaji wa madeni.

Zaidi tembelea //habarileo.co.tz

Maoni yangu:-
Tatizo walianza kununua ndege ndipo wakaandika business plan (mpango kazi).
Miaka 7 maana yake hata era ya JPM zilikuwa hazitumiki???
Is it make sense hasa ukizingatia JPM alivokuwa Strictly??
 
Ni kichekesho, Mfuko wa kushoto wa suruali unaudai mfuko wa kulia wa suruali hiyo hiyo kwa kukaa na hela mwezi mmoja halafu iwe story ya kuwahadithia watu wenye akili? Je tutegemee Taasisi hizo kufikishana Mahakamani? Wandishi kuweni serious bhana🤣
 
Miaka 7 maana yake hata era ya JPM zilikuwa hazitumiki???
Is it make sense hasa ukizingatia JPM alivokuwa Strictly??
Alikuwa strict kwa kuwa fool tu wajinga, ila yeye ndiyo chanzo cha yote hayo
 
View attachment 3306981

DODOMA — Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) inakabiliwa na changamoto kubwa baada ya ndege nne za Airbus A220 kutokutumiwa kwa siku 279 hadi 721 kutokana na matatizo ya kiufundi na upatikanaji wa vipuri.

Pia, ndege aina ya DASH 8 Q300 haijatumika kwa zaidi ya miaka saba licha ya kugharimu zaidi ya bilioni 20 kwa matengenezo.

Kwa miaka sita mfululizo, ATCL imeshindwa kulipa tozo za ukodishaji wa ndege, na sasa inadaiwa shilingi bilioni 369.13 na Wakala wa Ndege wa Serikali.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amependekeza hatua za haraka za kukabiliana na changamoto hizi kwa kufanya mapitio ya mikataba, tathmini ya aina ya ndege, na mpango wa urejeshaji wa madeni.

Zaidi tembelea //habarileo.co.tz

Maoni yangu:-
Tatizo walianza kununua ndege ndipo wakaandika business plan (mpango kazi).
Mifuko ya suruali inadaianaje sasa. Hebu waache usanii wa kuibiana hela.
 
CCM wameshindwa kukiendesha kiwanda cha kandambili(Bora Shoes) wataweza biashara ya kurusha ndege!
 
Back
Top Bottom