ATCL yadaiwa Tsh 369 Bilioni wakati ndege zimeegeshwa miaka 7 bila kuruka

Kwanini Precision Air wananunua ndege used na hazipaki? kuna ufisadi mkubwa sn kwenye huu mradi
Shirika la ndege halifufuliwi kwa kununua ndege mpya tena kwa cash. Wala tatizo la ATC halijawahi kuwa kukosekana kwa ndege. Serikali inajua vizuri sana miaka mingi tu kilichofanya ATC ishindwe kufanya biashara.

Watu wanajitoa fahamu ili waongeze spidi ya kleptocracy kupitia "ununuzi wa ndege" bila aibu kwa vile tu raia wengi hawana uelewa na hawapendi kujua mambo ya kitaaluma. Wana mfano wa Precision Air lakini hawataki kujiuliza inakuwaje? Badala yake imekuwa ni mambo ya ushabiki kwa viongozi wa kisiasa na porojo zao za kitapeli.
 
Watakuwa wanaitafuna haswa ATCL
 
Wabongo tunaitwa nyani waliopo kwenye process ya kuelekea ubinadamu miaka ijayo ujue! Hamna hata mtu anajali ndani ya serikali na sisiem zaidi ya watu wachache wa JF

Watasema ilileta watalii so ni faida kubwa imepata indirect kwa kuwa hawahitaji faida wanataka kodi, nyumbu kabisa
 
Hilishitik lingeendeshwa kwa PPP , gov imefeli kabisa operashion za hili shirika
Ukitaka kuleta PPP wahafidhina watkuambia unauza ATCL kwa DP WORLD au kwa waarabu.

Watanzania hatujiwezi
 
Zitto alisema zinahusishwa na umtumba terrible teens
 
Watakuwa wanaitafuna haswa ATCL
Na kuzitumia ndege kama mali binafsi (private jets) bila kujali hasara kwa vile hakuna wa kuhoji wala kujali.

Ethiopian Airlines wana fleet ya ndege mpya za kisasa zaidi ya 150 na wanazidi kuleta mpya na kuondoa za zamani kila wakati bila kutumia hela nyingi bali kwa biashara iliyochangamka sana.

Wanabadilisha fleet kila wakati kutegemeana na biashara inavyoenda. Wana mikataba na mabenki makubwa na makampuni ya ndege (Boeing & Airbus) inayowapa unafuu sana wa kupanga fleet yao kulingana na mahitaji ya business plan yao. Wanaingia mikataba na nchi mbalimbali za Afrika kutumia route zao za kimataifa (traffic rights) na kupanua business plan yao. Hapa kwetu wanahudumia JNIA, KIA na Zanzibar kila siku na kuleta idadi kubwa ya watalii.

Tanzania haya ni mambo ambayo yamepuuzwa na wahusika na hayawezi kueleweka kabisa kwa wananchi waliojaa ushabiki wa kisiasa. Tunazidi kupata aibu ya watu kujazana viwanjani eti kupokea ndege mpya ambazo matumizi yake hayaeleweki. Ethiopia ndege mpya zinapokelewa na watendaji wa shirika. Wizara husika na ikulu wanapewa taarifa rasmi basi. Wananchi wanafahamishwa na vyombo vya habari na press releases za shirika.
 
Huku kwetu nchi ipo kwenye kampeni kila siku
 
Tunafufua shirika Kwa kuna ndege 🀣🀣

Hilo ni deni la serikali Kwa Serikali ila Kuna hasara pia 😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…