Athari za kubeti

DJ SEPETU

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2017
Posts
8,413
Reaction score
12,336
Mwanzoni mwa mwaka huu kama masihara nilijikuta naingia ktk huu mchezo baada ya kujiunga kampuni mojawapo sitoitaja jina.

Kwa kifupi ni kwamba kushinda huwa nashinda ila kuliwa ni zaidi.

Pili nimepoteza fedha ndogo ndogo nyingi ktk huu mchezo ambazo ukijumlisha ni pesa ya maana.

Vile vile upotevu mkubwa wa muda.

Kwa hiyo nimeamua kuachana na hii kitu
 
Pole mkuu msifanye kubet kazi. Kama ilikuwa unywe bia mbili, kunywa moja pesa ya bia nyingine kabetie.

Ungekuwa umefanya kama kitu tu cha ziada usinge lalamikia muda.
 
Dah...mbona Mimi sibeti na wala hiyo pesa ya maana sina? [emoji44]
 



Mkuu kubet ni kamari, kuna madhara mengi ya kijamii katika kucheza kamari---- kifupi kamari ni mchezo ambamo mtu mmoja anapata na mwingine anakosa yaani kupata kwa mmoja ni huzuni kwa mwingine na kukosa kwa mmoja n furaha kwa mwingine, sasa jamii ikifikia hali hiyo hapo roho za hiyo jamii "hukomaa" yaani polepole jamii inakosa roho ya utu katika mambo mengi sana kwa sababu ya hiyo kamari kwasababu ni hulka mbaya sana mtu kunufaika kutokana na shida na taabu za wengine (kumbuka kamari siyo huduma kama kuchonga majeneza).

Jambo jingine katika jamii ya wacheza kamari ni kwamba kamari inayo (addiction) uraibu, ukisha anza kucheza na ikatokea siku moja umeshinda basi utanogewa na ndiyo baadhi utasikia wamefilisika kwa kuuza mali zao kwa ajili ya kamari na hata wengine hufikia kujinyonga kutokana na hasara kwa kucheza kamari, na hata kumepata kutokea baadhi ya watu kuuawa kwa sababu tu walihongwa na wacheza kamari ili wafanikishe ili upande mmoja wa wwchezaji kamari ushinde dhidi ya upande mwingine.

Madhara mengine ya kamari katika jamii ni kuharibika shughuli za uzalishaji kutokana na fedha nyingi isiyozalisha kuingizwa kwenye mfumo wa kamari hivyo shughuli nyingi za uzalishaji huzorota hivyo kuharibu uzalishaji kama kilimo nk.kwa sababu watu watakuwa wameona kwamba kamari ndiyo njia nyepesi ya kujipatia kipato kama DECI.

Hivyo michezo ya kubahatisha, betting, bahati nasibu nk zote hizo ni Kamari a ni haramu.
 
Hapa nilipo nabet,uku naangalia mpira.Kwa Tsh25,000 nimeweka egypt to win 1st half (odd 2.25-live betting).Trezeguet katupia na tayari nimeingiza 56,250.Nawithdraw sasa hv kubet tena mpk kesho.Tatizo lenu mnafanya betting km kazi jombaa lazma uwe unalia kila siku.OVER
 
Asante
 
Vipi ikiwa asingetupia!
 
Umeongea kila kitu mkuu ila hiki kizazi cha dot.com sidhani kama kitakuelewa.
 
Na vipi kama asingetupia Egypt hilo goli la 1st half ungetuambia nini? au ndio ungesikilizia maumivu kimya kimya tuu?
 
Ningekuwa nimeliwa na story ingekuwa imeishia hapo.Maisha yenyewe ni kubet tosha,kwan wee ukiomba kazi sehem sio betting iyo mana hujui km utaitwa au vp,betini kwa kiasi na jmn dunia ndo inavoenda hv😵VER
Story isingeishia hapo, Mimi nimebet kwa miezi 6 nimejua madhara yake.
 
Na vipi kama asingetupia Egypt hilo goli la 1st half ungetuambia nini? au ndio ungesikilizia maumivu kimya kimya tuu?
Mbona simpo tu,km hasingetupia ningekuwa nimepigwa.Ila sasa ndo hvyo katupia na nimempiga UNASEMAJE HAPO!!!
BET WHAT YOU CAN AFFORD TO LOSE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…