Mkuu kubet ni kamari, kuna madhara mengi ya kijamii katika kucheza kamari---- kifupi kamari ni mchezo ambamo mtu mmoja anapata na mwingine anakosa yaani kupata kwa mmoja ni huzuni kwa mwingine na kukosa kwa mmoja n furaha kwa mwingine, sasa jamii ikifikia hali hiyo hapo roho za hiyo jamii "hukomaa" yaani polepole jamii inakosa roho ya utu katika mambo mengi sana kwa sababu ya hiyo kamari kwasababu ni hulka mbaya sana mtu kunufaika kutokana na shida na taabu za wengine (kumbuka kamari siyo huduma kama kuchonga majeneza).
Jambo jingine katika jamii ya wacheza kamari ni kwamba kamari inayo (addiction) uraibu, ukisha anza kucheza na ikatokea siku moja umeshinda basi utanogewa na ndiyo baadhi utasikia wamefilisika kwa kuuza mali zao kwa ajili ya kamari na hata wengine hufikia kujinyonga kutokana na hasara kwa kucheza kamari, na hata kumepata kutokea baadhi ya watu kuuawa kwa sababu tu walihongwa na wacheza kamari ili wafanikishe ili upande mmoja wa wwchezaji kamari ushinde dhidi ya upande mwingine.
Madhara mengine ya kamari katika jamii ni kuharibika shughuli za uzalishaji kutokana na fedha nyingi isiyozalisha kuingizwa kwenye mfumo wa kamari hivyo shughuli nyingi za uzalishaji huzorota hivyo kuharibu uzalishaji kama kilimo nk.kwa sababu watu watakuwa wameona kwamba kamari ndiyo njia nyepesi ya kujipatia kipato kama DECI.
Hivyo michezo ya kubahatisha, betting, bahati nasibu nk zote hizo ni Kamari a ni haramu.